Labda tutakuelewa, JK

habibu bakili

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2012
Posts
202
Reaction score
51
tunajua kuwa mkuu wetu wa nchi umeamua kuwa sikio la kufa,
kila siku tunapiga kelele kuwa tunakerwa na ziara zako za ughaibuni, lakini imekeuwa kana kwamba unatukomoa na hujali sisi ''tunaokuonea wivu'', kwani kasi yako iko pale pale.
binafsi naomba utuambie hasa unachofanya kwa kila safari unayokwenda huko..
Mara nyingi tumekuwa tunasoma tu taarifa za ikulu katika vyombo vya habari kwamba raisi amesafiri, lakini kuna blah blah nyingi sana bila kueleza kinagaubaga unacho kwenda kufanya huko.!
waziri wako maghufuli katuambia eti unatafuta misaada ndo maana tuna 'neema' ya barabara nyingi za lami.. but lets be serious, hivi misaada huwa inatafutwa hivi.??? hata sisi ambao tuna kijiexperience ya kufanya kazi katika NGOs tunajua 'misaada' haitafutwi hivi.! na kama ni kweli ni misaada, mbona ni nchi nyingi za kiafrika zinapokea misaada na hatuwaoni maraisi wao wakizurura hivi.???
naomba utueleze mkuu, unaendaga ughaibuni kufanya nini hasa??? labda tutakuelewa na tutaacha kukuonea ''wivu'' kama wanavyotusema wafuasi wako..
 
ni vyema kama wananchi tukawa tunaelezwa malengo mahususi ya ziara zako na si blah blah za maafisa habari zako hizi tulizozizoea..
 
TETESI: naskia jamaa huwa hana ratiba maalumu, yani dakika yoyote anaweza kubadilisha shughuli zilizopangwa katika ratiba yake ya kikazi..
 
ka ona nchi imemshinda bora afanye utalii tu, mbaya zaidi anachonikera sehemu zingine nyeti yenye mijadala yakitaifa utakuta ubavu uko pembeni na yeye anajadili, ivi uyu mama haoni aibu ? usifikiri kila sehemu ni ya kuuza sura, jifunge kwa wenzio walio pita una tia aibu
 
kiukweli hili ni janga la taifa,kwa kweli watanzania tumeonewa sana kuwa na raisi kama huyu,nisiseme saana maana meno yangu yamebaki machache,maana nimeng'oa manne,yaliyobaki yametoboka,yasijemaliziwa bure"ccm juu,raisi oyeee"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…