Labda ni Ajira & Usimamizi Hafifu

Kibunago

JF-Expert Member
Jan 11, 2008
300
122
Nilipoangalia Gwaride rasmi la sherehe ya miaka 49 ya Uhuru pasipo kusita niliwapa alama 6/10 .

Precision & uniformity ni mambo hadimu.

Mwenye video atuwekee turejee tena tuone. Karibu gadi nyingi zilikuwa na kigugumizi wakati wa kumaliza kutoa heshima kulia (mwendo wa haraka) ili kuendelea na mwendo.

Jamani yaani kweli, baada ya mazoezi ya muda mrefu kwa ajili ya Siku kubwa kama hii unaamrishwa 'macho mbele' halafu wewe unaanza kujikanyaga kanyaga.

Sipati picha. Labda ni wakati muafaka wa kufukiria jinsi tunavyowaajiri maaskari wetu siku hizi au pia usimamizi na nidhamu umeshuka; pengine ndio maana hata na vitambi vimeongezeka!

Hata wanaotoa amri wengi wao hawafuati rhythm za bendi na zile sauti za 'simba' zilikuwa na wachache sana.

Tunapozungumzia Precision kwenye Drill nakwambia ni raha maana hubadilika na kuwa sanaa ya aina yake na wengine wakidhani mazingaombwe. Sio Askari anashika bunduki kizembe inamgonga gonga na kutaka kumponyoka.

Ukitaka kuangalia mfano wa ninachosema angalia hapa, tena kwa wazee wa suti.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom