johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,695
Namfananisha Lowasa na maalim Seif hawa ni magwiji wa siasa tokea wakiwa CCM.Mwalimu Nyerere alisema upinzani wa kweli utatoka ccm sasa ninapoziangalia siasa za upinzani zilivyodorora na kupoteza mwelekeo ni wazi Lowasa wa bara na Seif wa visiwani ndio pekee waliobaki na ushawishi. Kwa kuwa chadema hawajawahi kufanya siasa za kipinzani zaidi ya kujikita kwenye siasa za kiharakati ni wazi basi Lowasa akikalia kiti cha enzi cha cdm ataibadilisha kabisa na kuwa chama chenye sura ya upinzani halisi.Nasema LABDA kwa kuwa Eddo naye ni binadamu ana mawazo mbadala pia.