Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 27,409
- 26,892
Nini hasa unadhani kimepelekea vyama vya upinzani nchini, kupuuza na kuukalia kimya wito wa kuunganisha nguvu ya upinzani kisiasa na kiongozi mpya wa Chadema Taifa, kuelekea uchaguzi mkuu wa October mwaka huu2025?
Ni hisia za ulaghai na utapeli wa kisiasa dhidi ya mipango ya vyama vyao, na hasa ukizingatia kauli, misimamo, lugha na aina ya siasa zisizoaminika za kiongozi huyo mpya wa Chadema?
Au wamehisi ni mbinu ya kisiasa ya kiongozi mpya wa Chadema kuhujumu misingi ya vyama vingine vya siasa vya upinzani, kuvidhoofisha na kukkinufaisha chama chake cha Chadema?
Au wameona hakuna dhamira wala nia njema kwenye wito huo kwani kwa muda mrefu sana kiongozi huyo amekua akivibeza vyama vya upinzani vyenye malengo na mtazamo ulio kinyume au tofauti na na chama chake, hata kufikia wakati vyama vya upinzani akaviita ni mamluki wa CCM na vingine ni ccmB.
Swali la kujiuliza,
ni lini mamluki na CCMB wamekua wa muhimu kiasi kwamba wanahitajika na alie wabeza kuunganisha nguvu nao kuelekea uchaguzi mkuu wa October?🐒
Mungu Ibariki Tanzania