Laana ya udini yaiandama ccm

Laana ya udini yaiandama ccm

Status
Not open for further replies.

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
1,270
Reaction score
536
Neno laana ni neno baya na mara nyingi limetumika kuonyesha hali ya kutofanikiwa kwa aliyepatwa na laana hiyo. Laana inaweza toka kwa Mwenyezi Mungu, Mtu aliyekuzidi hasa mzazi, viongozi wa dini nk. Laana mara nyingi husababishwa na mtu kutotenda vema au kufanya hiyana itakayomuumiza mtoa laana. Si mara zote mwenye kutoa laana hutamka bali anaweza akaumia moyoni hata kama hajatamka laana ikakupata.

Kinachoonekana sasa kana kwamba CCM imepata laana hasa kwenye suala la udini. Kuna mambo mengi yanayojitokeza sasa kwenye chama na serikali yake yasiyoenda vizuri. Mifano ni mingi lakini hapa nawatajia michache:
1. Kila wanachosema hakitekelezeki -wanaweka maazimio mengi kwenye chama na serikali lakini kinaishia kuzungumzwa kwenye vikao -hakuna utendaji
2. Kukimbiwa na wananchi hata kwenye mikutano wanayogharimia kwa gharama kubwa kubeba watu kwenye mabasi na malori
3. Kukosa hoja za msingi mpaka bungeni kiaisi cha wapinzani kuwa ndiyo watoa hoja zenye mashiko kwa wananchi
4. Kulazimisha mambo hata ambayo hayalazimishiki -mfano kwa kuwa Chadema wamefanya mkutano, basi na sisi tutafanya mkutano na kuishia kukatishwa tamaa na mahudhurio hafifu
5. Serikali kutumia ubabe kwenye kila jambo wanalotaka kufanya kwa wananchi kiasi cha kuishia kuua watu kwa visingizio mbalimbali
6. Watu kuikataa ccm na serikali yake mpaka vijijini -haijawahi kutokea kwa wananchi mpaka wa vijijini kama Mtwara kuandamana kuipinga CCM
7. Mauaji ya ajabuajabu ya watu wasio na hatia -mifano: Mwandishi Daudi Mwangosi
8. Kuandamwa na mikasa mingi ya ufisadi hata baada ya matamko ya viongozi wakubwa wa chama na serikali nk.

Itakumbukwa kuwa ccm ndiyo walioasisi suala la udini kwenye kampeni na kabla ya hapo kwa kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa ni CHADEMA ndiyo wadini, wakabila na wakanda bila kuwa na ushahidi wowote huku kiongozi Mkuu wa CCM akiwa kinara wa jambo hilo, kisha Nape na sasa wale watoto wawili waliofukuzwa CHADEMA.

Nikitazama kwa makini naona kila dalili za laana zinazopelekea anguko la chama hili tawala na serikali yake.

Je, ni kweli CCM imelaaniwa?

Nawasilisha toka kijijini
 
Ccm n sawa na yai lililooza kwan hutoa harufu mbaya mda wote. Ukisema kimelaaniwa n sawa kwan wapo kwa masilah yao sio kwa wananchi.
 
hata sipendi kusikia hili lichama likafie mbali..kama wananchi wako kupata milo miwili tabu huku wewe ukisomba pesa yao kupeleka uswiss unategemea nini? au wangonjwa unawatengezea madawa fake wewe unadhani Mungu atakuachatena siyo awalaani tu awachukue
 
2015 mbali. Ccm inaangamiza nchi wa juhudi zote. Inasikitisha kwamba mtanzania ndiye anayeangamiza Tanzania. Bila hata kusukumwa. Miaka 7aidi ya 50 inatosha, tunataka mabadiliko.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom