Laana inayoniua (Kisa cha kweli 10/12/1989)

Iringa Native

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
961
3,050
Umri umeenda na kifo kinanijongea...

popote ulipo Natinde elewa nakufa kwa mawazo kama ulivyonilaani!

Leo ni miaka 30 tokea nilipokutana kwa mara ya mwisho na Natinde maeneo ya Monduli 10/12/1989

Natinde ni binti wa Kimasai nilikutana nae ujanani wakati nilipoenda Arusha/Monduli shughuli fulani maalumu ya kikazi iliyonilazimu nikae kule (Ngarashi) kwa zaidi ya miaka miwili. Natinde naweza sema ni moja ya wanawake waliowahi kunipenda sana na mimi pia nikampenda sana ila ujana ukapelekea nimpuuzie! Ndani ya mwaka mmoja tulijenga malengo mengi ya maisha hadi ya kifamilia pia.

Nakumbuka mahusiano yaliingia doa baada ya yeye kuniambia ni mjamzito. Nilijikuta namchukia ghafla na kuanza kumsemea hovyo ikiwamo kumuita kahaba mtoto (alikuwa na miaka 18 tuu wakati huo na mimi nikiwa na 22) na mimba nikaikataa. Natinde akamua kuondoka na kwenda kwa shangazi yake Manyara sehemu iitwayo Galapo kwakuwa alikuwa akiishi peke yake katika mji alioachiwa na wazazi wake, hivyo shangazi yake aliposikia alimuomba aende kwake then akijifungua atarudi kwao na Natinde akakubali.

Akiwa manyara alijalibu kunitumia watu kunisihi ya kwamba yeye anachohitaji ni mimi kutambua ujauzito na sio kwamba anahitaji msaada wowote wa kifedha ila bado nilimkataa.

Baada ya miezi kadhaa niliambiwa amejifungua mapacha. Wakati fulani nikiwa Arusha mjini kikazi niliambiwa Natinde yupo Monduli. Nilifulahi sana maana nilijua nikirudi nitawaona hao mapacha, kila mtu aliyewaaona wale mapacha alisema ni watoto wasichana na ni wangu kabisa hadi mkubwa wangu wa kazi alinilaumu sana baada ya kurudi Monduli akilaumu kuwa nimekataa ujauzito ambao nilijua nimehusika.

Nilipofika kwa Natinde nilikuta kashaondoka Galapo na hapa ndipo moyo wangu ukaanza kukosa amani kwa kuhisi jambo fulani ambalo sikujua ni nini.

Miaka yangu miwili ilipofikia tamati ilikuha barua iliyonihitaji kuelekea Tabora haraka (kesho yake yaani) ila wakati naondoka (nikiwa katika gari ya kazini nikiwa na wenzangu kama 20) pale njia panda ya kwenda mjini na Babati, ghafla gari ilisimama na dereva alitoa maagizo niambiwe kuwa nitazame nje. Ah hapa ndipo nikamuona Natinde amebeba watoto wawili huku machozi yakim'mwagika sana na baada ya sekunde kadhaa gari ikaondoka nilitamani kushuka ila isingewezekana pia nilitamani kulia ila ikabidi nijikaze. Wakati nikiwa kwenye mawazo ndipo rafiki yangu akanipa barua aliyokuwa kapewa na Natinde anipatie siku tukiondoka.

Barua ilisema mengi ila yote yalikuwa ni maumivu kwangu kuanzia ile siku hadi leo, katika barua alisisitiza kwakuwa nilimkataa na kumdhalilisha Monduli nzima basi sitokuja kuwaona watoto mpaka kufa kwangu yaani hata niwatafutaje sitowapata na wao hawatonitafuta kamwe pia akasema kama nilivyomfanya aishi kwa mawazo kipindi chote cha ujauzito basi na mimi ndivyo nitaishi kwa mawazo juu yao mpaka kufa kwangu n.k

Nlipo report Tabora baada ya miezi mitatu niliomba ruhusa ya wiki moja nikakubaliwa ndipo nikaenda Monduli, nilipofika nilichokutana nacho ndio kilimaliza kabisa kwa maana nilikuta Natinde kauza kila kitu alichoachiwa na wazazi wake na akaondoka akiahidi hatokanyaga tena Monduli. Nilienda Galapo, nilizurura kama chizi Galapo nzima na hadi vijiji vya karibu vyote ila hapakuwa na dalili ya Natinde, hadi naondoka sikuwa nimepata chochote. Hapa ndipo laana yake ilipoanza kunitafuna nikawa mlevi wa kutupa kitu ambacho kilinisababishia matatizo kazini pia.

Naandika haya nikiwa Monduli,tokea mwaka 1998 hakuna mwaka umepita bila kuja kumtafuta Natinde na watoto wangu. Nimekuwa nikijitahidi kila 10/12 inikute hapa nikitumaini atanionea huruma kwa kuwa kama yupo hai najua anajua kuwa hakuna mwaka sijaja hapa.

Nawaza yeye watoto zangu wapo hai au washatangulia mbele za haki, nawaza pacha mmoja alipewa jina gani, mwingine najua alipewa jina mama yangu kwakuwa aliwahi kusema kama akijifungua mtoto wa kike atampa jina hilo ila wa kiume atampa jina la baba yake.

Nina watoto wengi kiasi ila wote ni wa kiume. Nimejaribu hadi uzeeni kutafuta mtoto wa kike ila nimekosa na hii yote ni laana ya kukataa ujauzito wa Natinde. Mbaya zaidi laana imeenda mpaka kwa hawa watoto zangu maana na wao hakuna mwenye mtoto wa kike.

Sina mtoto wa kike na sina pia mjukuu wa kike kwa laana yake Natinde!

NATINDE: Kama upo hai naomba unitafute kabla mauti hayajanifika. Nimeishi kwa mawazo sana tokea siku niliyokuona kwa mara ya mwisho na ninakufa kwa mawazo pia; najua kwako sina nafasi tena na pia najua kwa watoto pia sina nafasi ila naomba kuwaona niwaombe msamaha watoto wangu kabla sijafa.

Sifa za huyu Natinde

i. Baba yake alikuwa ni Maasai na mama yake M'mbulu
ii. Mrefu, mweupe sana mwenye nywele ndefu ila hupenda kukata
iii. Kwao walikuwa wafanyabiashara, hivyo na yeye atakuwa hivyo nahisi
iv. Haeneo yake ni Arusha, Manyara na Singida
v. Atakuwa na mapacha na kwa sasa; atakuwa na miaka 48 na mapacha wake watakuwa na miaka 30
vi. Katika kumjua hakuwai kuvaa hereni wala bangili, yaani ni mtu asiye na mambo ya urembo

Ahsanteni.
 
Huyo natinde hana majina matatu na huyo shangazi yake hana majina matatu je watendaji wa serikali wa sehemu husika hukuwapata.

Jaribu kutuliza akili kisha anza upya kufuatilia itakuchukua hata miezi sita kupata footprint yake, uvumilivu tu na subra ndo kila kitu, pia jaribu kuulizia hata majina ya hao mapacha.

Pole kwa unayopitia acha pombe tulia meditate mafanikio yapo mbioni.
 
Kama alishasema huta mpata.Inawezekana kabadili majina kila kitu.Na watoto hawajui chochote kukuhusu wewe ama wameambiwa ulishakufa.

Kama watoto unao inatosha.Kuzaa watoto wa kiume tu na wajukuu sio laana.Ni baraka.

Mungu kakubariki umeeza ona maisha ya wanao na ukaona wajukuu bado huna shukrani?

Kuwa na amani...
 
Unamtafuta kwa sababu gani? Ulikataa mimba kwa sababu gani? Uliogopa malezi ya watoto au uliogopa kulea mimba? Hukutaka kumuoa? Alikuomba sana hahitaji chochote zaidi ya wewe kukubali mimba basi, kwa nini hukufanya hivyo? Unamuhitaji sasa kwa sababu hujapata mtoto wa kike?

Hao mapacha wa Natinde ni wa kike si ndio? Unawahitaji sasa kwa sababu watoto wako wamekosa watoto wa kike?

Au unamuhitaji ili iweje na alikuambia hutamuona yeye wala watoto na ukaona poa tu, yaani umemuona mwanamke analia na ana watoto wako na unajua anapitia wakati mgumu ila hukuona haja ya kushuka kwenye gari kwenda kumfuta machozi halafu unamtafuta mitandaoni kweli? Mkuu pambana na hali yako, omba rehema kwa Mungu.
 
Iringa Native,

Mtu anapofanya makosa halafu guilty burden inapomtafuna hua anasingizia eti laana!
These people are crazy
Hapo ni watoto tu anawatafuta, nothing else!
Hakuna kitu kama laana.

Hayo ni maneno ya kufupisha habari tu.

Ukikataa mtoto, hakikisha utaendelea kumkataa maisha yako yote.

Sio unamkataa leo, halafu kesho unamtafuta.

Ukifikiri utamtafuta miaka ijayo, usimkatae kabisa.

Consistency please.
 
pumbavu zako na pumbavu zenu wte wanaume mnaokataa mimba wakat huo mnajua ni zenu Kufa tu pumbavu
Mkuu lewiathan ni kweli umeonesha hasira zako juu ya jambo na ndugu yetu wakati mwingine lazima tuweze kupunguza hasira zetu, sijui umri wako ila naamin mleta mda pia ni mtu mzima kama ungekuwa unaonana nae sidhani kama ungeweza mwambia hayo maneno.

Najua ujana unachangamoto sana, unaweza fanya jambo sasa ukalijutia uzeeni, vijana wengi wanakataa mimba sababu maisha yanakuwa magumu sana ila ww ulikuwa na kazi ungeweza kumlea Mama na watoto, kwa kiasi fulani unastahili unachokipata kwa sasa, kwanza kabisa mkuu Iringa Native pole sana lakin pia sijui dhamira ya bandiko hili ni kutuonesha hali unayopitia sasa au kumtafuta unaemtafuta.. kama kweli ni kumtafuta, ni vyema ungemwezea zaidi hasa kwa majina yake yote na hata ndugu zake kama unawafahamu kwa majina.. JamiiForums inawatu wengi unaweza pata msaada, mwisho kabisa Omba sana Toba kwa Mungu ili akupatie wepesi.
 
Nami yupo mmoja huu mwaka wa nne hataki kuikubali damu yake kila jitihada nimefanya kumuweka karibu na mwanae ila anampotezea for really inaumiza sana tena mno, Mungu endelea kunipa moyo wa subira nione mwisho wake
 
Back
Top Bottom