SEACOM ipo down - Nairobi ipo down - MPESA ipo down - Hakuna System!
Mmiliki wa server za M_pesa yupo kenya, sasa voda fone wanunuzi wa leseni ya M-pesa hawawezi kuwa na jibu la moja kwa moja wakati kuikwa na tatizo la m-pesa. ili jua kuwa pesa zako zipo salama.
mimi nimelizwa pesa zangu hadi leo sijazipata, zimetolewa na mtu kaenda bila kitambulisho lakini cha ajabu wakala kampa as simple as that. nafika naambiwa zimeshachukuliwa, kwenye simu bado hata sijapata sms kusema zimetolewa -- watch out this system, hasa unapotuma M-PESA kwenda TIGO pesa hapo kuibiwa ni rahisi sana then wanasingiziana, mara nenda TIGO, mara Nenda M -PESA.
Bora hata muuza duka,wakala hawa kama wauza kalanga
mbali ya hili mie nimelizwa pesa mara2,ya kwanza 30 nilimtumia mama (wa kunizaa),akanambia hata meseji hakuipata na wakati M-pesa wanasema imetumwa,paka leo nilipoteza
mara ya pili kituo tofauti nikatuma 10elfu nikaituma kwingine,hakupata meseji lakini salio linasoma,alivyoongea na voda akaambiwa mimi nirudi kwa wakala a-resend kwa maana wakati inatumwa mtandao ulifeli,kufika kwa wakala akawa mbogo,akawa mkali,akakataa katakata ku-resend,nikamuuliza kwani hajawahi kupata hasara kwa nini anakataa kuresend?akasusa,basi nikaamua kuipotezea nikaondoka
ila frankly speaking,M-PESA ina matatizo sana pamoja na mawakala wao,wanajua kuandika tu,hawawezi kuhandle wala kusolve out contingencies,binafsi sina imani tena na mambo yao
Sure Mkuu!Juzi, jana na hadi hivi sasa huduma ya kutuma na kupokea fedha kwa kutumia M-Pesa imekufa "kwishney' kabisa hapa jijini Dar es salaam, na nadhani nchini kote. Kila wakala wa huduma hiyo niliyemtembelea maelezo yake yalikuwa yaleyale- HAKUNA MTANDAO. Na ukiuliza sababu ya kuwepo kwa tatizo hilo wanasema hawajui na wala hawajaarifiwa kulikoni. Pamoja na usumbufu huo wanaopata wateja cha ajabu ni kuwa hata Voda wenyewe ama kwa kiburi, ukiritimba, ama dharau za maksudi, hawajatoa maelezo yoyote kwa wateja kuhusu tatizo hilo, kiasi cha baadhi ya wateja niliowakuta wakisotea huduma hiyo katika vituo vya mawakala, kuingiwa na hofu kuwa waje wakaingizwa mjini kama ile habari ya DECI. Mmoja alikwenda mbali kwa kusema kuwa kama watu waliaminika katika jamii ndio waliotuingiza mkenge katika mambo mengi ya uchumi, Voda watashindwaje kutu-deci. Voda toeni ufafanuzi kuhusu kadhia hii!:A S cry:
Pole sana, hiyo ni hela nyingi. Mi nakushauri uende TCRA, kuna fomu za malalamiko kwenye website yao (TCRA|Tanzania Communications Regulatory Authority). Jaza hiyo fomu peleka TCRA na nakala wapelekee wao-M-Pesa.Hata kama hutapewa pesa zako, ni lazima uonyeshe unatambua haki yako. Hii itawasaidia hata ndugu na rafiki zako wa karibu wasipatwe na madhila kama yako. Hiyo pesa ni nyingi na kosa ni lao (wamekiuka utaratibu kwa kutoa pesa bila kibali), don't go down without a fight!mimi wamenilamba laki 700,000 sitaki hata kusikia kitu kinaitwa MPESA in my life - kuna vijana wanjanja wanjanja wanachezea network - nimefuatilia makao makuu hapa mlimani city wananizingua na kunipotezea muda wangu. sababu hata message kwamba pesa imetolewa sijawahi ipata, na jamaa kaenda kwa wakala kalamba pesa zote eti bila kitambulisho - inaingia akililini kweli?