Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
CCM, CDM, ACT,CUF, NCCR nk, mnaotupa karata zenu kuomba ridhaa kuongoza katika nyadhifa zozote zilizopo na sisi wapiga kura, uzi huu unatuhusu, sote kabisa.
Kama ilivyo katika mashindano, hatima ya ushindi au kushindwa kwenye uchaguzi wowote iko mikononi mwa wapiga kura ambao kwao jukumu hilo ni siri sirini - mioyoni mwao.
Viachwe vyama, wagombea na wapiga kura kwa starehe zao kutimiza majukumu yao.
Vitisho, hadaa, janja janja, laghai na vitendo vyovyote vya kutumia nguvu vinapaswa kukemewa na kupigiwa kelele na waungwana wote, kote ndani na hata nje ya nchi.
Haijalishi ni nani anataka kulitumbukiza taifa hili kwenye machafuko. Tusilazimishane. Uchaguzi wa mpiga kura ni uamuzi binafsi.
Wenye wajibu wa kulinda usalama na wafanye kazi yao bila kuwaathiri watia nia, vyama, mashabiki wala wapiga kura.
Tume ya uchaguzi itambue kuwa kazi yake iko kwenye idadi ya kura kama zilivyo pigwa na si vinginevyo.
Asiye kubali kushindwa si mshindani. Hatumhitaji yeye wala matokeo yake ya mfukoni au ya kulazimisha.