Ndugu zangu,
Wasadikika hawana desturi ya kumsifu aliye madarakani. Watamnanga sana. " Hafagiliwi Mtu!'- Ni mmoja wa msemo maarufu kwenye Nchi ya Kusadikika.
Kiongozi Mkuu kwenye Nchi ya Kusadikika anapaswa kuwa mstahimilivu sana hata pale anapobondwabondwa akiwa madarakani. Katika kipindi hicho, Wasadikika huona mabaya tu ya kiongozi.
Akiondoka madarakani cha kwanza ni kumlinganisha mpya na aliyepita. Utasikia, " Ah, mabaya ya yule bwana yalikuwa machache sana!".
Hivyo, kwenye Nchi ya Kusadikika, Kiongozi Mkuu hata akiorodheshewa mabaya elfu moja na Wasadikika akiwa madarakani, avumilie tu mpaka mwisho, akiondoka yanaweza kubaki kumi tu!
Maggid Mjengwa.