Kwenye Mchoro huu Kipanya alimaanisha nini?

Kwenye Mchoro huu Kipanya alimaanisha nini?

Mwanamke aliyesimama kwenye tawi linalokatwa na mwanamume "CCM" asiyependa kutambulika anaonekana hana kichwa au hatumii akili zaidi ya kumtegemea mkataji tawi kupitia mnyororo uliowaunganisha.
Mkata tawi ana dhamira thabiti iliyogawanyika kwa kusimika miguu yake mmoja upande wa tawi linalokatwa kuonyesha ushirikiano na mwanamke asiye na kichwa, wakati mguu wa kulia umesimikwa upande wa shina la mti ambao kwa muujiza tu anaweza kuepuka kuanguka.
 
1749022840693.jpeg
 
Mwenye Msumeno akimaliza tu atajifungua.Mwenye amevaa gauni atapaa ataokolewa,wakati huo mwenye Msumeno atajikunyata juu ya Mti,akisubiri kazi mupya

Nimetumia akili wanazotaka wao.
 
Wawili wamekutana juu ya mti alafu kila mtu yuko na timing zake, ila hatari kwamba mmoja ana msumeno alafu anataka akate tawi wanalolitegemea wote wawili
Mtekaji anategemea SEHEMU MBILI isipokuwa yupo connected na joka kuu Kwa Ile kamba .joka kuu akianguka na mtekaji Hana namna .
 
Jamaa aliona mbali ndio kinachoendelea nyuma ya mgongo wake wanafanya mambo yanayomharibia and they will go down with her
 
Angalia halafu Toa Maoni yako

View attachment 3355089
Fasihi inakuwa na tafsiri nyiiingi sana kutegemeana na mlengo au upeo wa mtu. Kwa upande wangu natafsiri ifuatavyo;

Huyo mwenye msumeno ni lissu na hiko kinyago ni siasa anayojifichia katika kupambania madaraka (kama alivyoelekezwa na mabwana zake wa ulaya (mabeberu). Huo msumeno ni sera ya ushoga ambayo lissu na nyumbu wenzake wanaipambania kuieneza hapa nchini (kama walivyoagizwa na mabwana zao huko ulaya).

Hilo tawi ni nchi yetu Mama Tanzania. Kwa mtazamo wao finyu, wanafikiri kwamba wakifanikiwa kuuneza huo ushoga basi watamkomoa mama Samia kumbe wataliharibu taifa kwa ujumla (ambalo ndo hilo tawi) kwa maana wataangamia wananchi wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom