Kwenye hili nahitaji ‘Critical Thinking' tafadhali kama unajijua huna au hujabarikiwa nayo usipoteze muda wako

Kweli umeandika gazeti, sasa ni ipi relation kati ya hiki ulichokiandika hapa kuhusu yanayotokea ndani ya CDM na kilichotokea leo?!

Halafu habari ya Zitto na wengineo sijui imekuja vipi hapa!, kama unamuona ana vision, vipi hiyo ACT yake inaendeleaje?!

Siasa zetu zinalazimisha uanaharakati, huwezi kulazimisha hoja kwenye mazingira ambayo polisi wanatumika kukibeba chama tawala. Utaenda vipi kulinda kura kwa hoja ulizoandika kwenye daftari? Hao wazee uliowataja Lowassa na Sumaye hawakujua ugumu wa kuwa mpinzani tz, mpk walivyoingia ndani ndio wakajionea, Tumemsikia Sumaye analalamika kanyan'ganywa mashamba, hayo ndio malipo ya kuwa mpinzani tz. Mbowe kaharibiwa mali zake zote, ndio malipo yakuwa mpinzani tz.

Hili suala la sumu haijaribiwi kwa kuionja linakuzwa na wajinga tu, hivi hufahamu kama huo ni msemo tu, ni sawa na angesema kina cha maji hakijaribiwi kwa kuingiza mguu, wacheni kupotosha watu, kamuua Chacha Wangwe kama una shahidi si upeleke polisi?, kupotea kwa Saanane kama unaushahidi peleka polisi, sio kuropoka tu.

Unazungumzia CDM kutaka kuiuza nchi, nchi gani hiyo?, na ninani waliotaka kuuziwa hebu wataje hapa tuwajue, sema na bei waliyokubaliana, kichwa chako kimejaa pumba nyingi sana!

Hahahaha! Una haki ya uchambuzi wako, nina haki na uchambuzi wangu. Kama nilivyokwisha sema, ni kawaida sana kwa watetea haki na demokrasia katika nchi hii kukosa uvumilivu, weledi na kushindwa kuishi wayahubiriyo inapifika ZANU yao ya kufanya hivyo, watanzania sio wajinga. Kama unaiamini na kuikubali kauli ya kuambiwa kanyang'anywa mashamba, kwa mini unakataa kauli take ya kutishiwa maisha na kuambiwa sumu haionjwi kwa kwa kulambwa?

Punguza jazba, relax tufanye majadiliano. Chairman wetu kaanzisha mwendo, tuvumiliane hats ndani ya chama kusikilizana tofauti zetu. Mpasuko haiku anza Leo, ulianza muda mrefu,btoka enzi zile Zitto alipoleta hoja ya wabunge wasilipwe posho.

Uanaharakati ulifanya Rais asitambuliwe na chama, tukatoka bungeni katika hotuba yake, leo tunaenda kumuomba maridhiano. Mi nafikiri tungemuomba radhi kwanza, tukamtambua rasmi kisha tuseme yanayotusibu. Siasa za harakati hazina faida, zinamdhalikisha anayezifanya na kumpunguzia thamani kama ilivyo sasa. Huku ni siasa inafanyika siasa, hayo ya polisi na mahakama si siasa, kama hujui siasa rudi kwa mamaako kajifunze siasa.
 
Mtoto akizira chakula unamuacha. Mliobaki mnakula chakula na kinachobaki mnawapa watoto wa jirani. Mnafanya hivyo hivyo na mlo unaofuata na unaofuata. Mwisho wa siku atakuja mwenyewe kula chakula! Ahahahaha!
 
Kwa mkristo anahitaji kuombewa ajue pia kusameheana kinyume cha hayo maombi yako na ya wanaokuombea yanaishia ozone na yatakurudia,hii ya Leo ni changamoto kwa JPM zaidi kuliko kwa wapinzani watu tusubiri atafanya nini?
 
Je, Kujitokeza kwa mara ya Kwanza kwa Mwenyekiti Taifa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe na Chama chake hicho Kumruhusu Kuhudhuria Sherehe za Uhuru wa Nchi yetu tofauti na alivyokuwa akigoma na Chama chake pia Kutomtambua Rais Dkt. Magufuli Kunaashiria nini ndani ya CHADEMA, Demokrasia ya Tanzania, Ustawi wa Kisiasa nchini na Taswira nzima ya Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2020?

ANGALIZO

Kama unajijua huna ' Critical Thinking ' ya Kutukuka acha Kutupotezea muda na waachie Werevu wachangie bakia msomaji.
If you think you r too small to make a difference try to sleep with mosquito!
 
Usiwatishe watu kwamba utajibu ovyo mkuu hapa si gerezani hili ni jukwaa huru na kuna taratibu zake... ndio maana wanachangia watakavyo na si utakavyo. Ikiwa hupendi maoni tofauti kwanini uweke uzi hapa jukwaani?
Huu ni mfano mbaya ingelikuwa una madaraka nadhani ungefanya makubwa kuliko hiki kitisho!!! Ruksa kupovuka na kuonesha utovu wako wa adabu mkuu...
Huyo Genta inaonekana inferiority fulani hivi.
 
Mbona hamruhusu mikutano ya hadhara kama mnajiamini anakubalika, ccm wanazunguka nchi nzima kina Polepole na Bashiru kufanya shughuli za kisiasa, vipi kwa CDM na upinzani kwa ujumla, waruhusuni na wao muone kama kweli mnakubalika.

Wewe umenda kuposa, mchumba kakukataa, kaolewa na mwingine, wewe unataka kuzungumza nae nini?

Ndio maana ya demokrasia, wananchi wakikichagua chama Fulani basi hicho watakuwa nacho mpaka wakati wa kampeni ujao. Wewe umesikia lini Democrat wanaitisha mkutano was hadhara na wananchi wa marekani? Kipi ambacho wananchi hawakuambiwa wakati was kampeni? Kama kipo kiwekeni kwa ajili ya kampeni. Kila jambo na wakati wake, haiwezekani muda wooote uwe muda wa mikutano ya hadhara
 
Asante sana Genta, huu uzi ni mfano mzuri wa tabia za wapenda na wapigania demokrasia, haki, utu, kuheshimiana na usawa katika nchi yetu. Wanapambana kila siku kuikosoa serikali na taasisi nyingine kutotenda haki wakati wenyewe hawawezi kuishi demokrasia, haki na yote wayapiganiayo.

Tabia hiyo pia ndio inayomfanya Mbowe hii leo ashiriki sherehe za Uhuru na kuomba suluhu.

Hats kabla ya kuja Lowasa, tayari CDM kulikuwa na kilio cha ndani kuwa tufanye siasa, proper siasa badala ya uanaharakati. Arusha walikuwa na malalamiko juu ya siasa za uchonganishi, za vurugu na zenye kutia hasira za lema kuwa zinaua chama. CDM haikusikia,

Zitto alipozikataa siasa za jinsi hiyo na kina Mwigamba na kuja na kauli nchi kwanza chama baadae, wasimamizi wakuu wa siasa za harakati, zenye kutia hasira, siasa za kujenga mpasuko wakamshughulikia.

Lowasa, baada ya CDM kushindwa uchaguzi akaja na mawazo ya kukijenga chama imara. Wazo likiwa lile like, kufanya siasa proper na kuachana na siasa za kiharakati, siasa za kukosoa zaidi kuliko kujenga mipango mbadala na kuuza sera. Lowasa nae akaonekana ameishiwa na bado ni CCM.
Akiwa ndani ya CDM akakosewa heshima na vijana wenye damu ya kiharakati wenye kuweza kusema lolote iwe laivu au kwenye mitandao. CDM kikawa chama cha Kambale kama alivyojionea mzee wangu Juma Duni Haji. Kila mtu ana mamlaka, hakuna utaratibu, hakuna heshima ili mradi tu uwe mwanaharakati na uwe na hamu ya kukamatwa utiwe jela. Sifa kubwa ya CDM ikawa uwezo wa kumtemea mtu mbovu, kuwa tayari kwenda jela au kupigwa na polisi.

Hali ilivyozidi ikabidi mwenyekiti aseme, gharama ya mahakamani, kuwekeana dhamana na mambo kama hayo ikawa kubwa. Chama kinachopigania demokrasia kikawa tayari kutoheshimu haki za watu na utawala wa sheria. Chuki iliyopandwa miongoni mwao ikawa kali kiasi cha kuwa tayari kuiuza nchi kwa maadui wetu eti kisa tu CCM iko madarakani.

Tabia hiyo ya CDM ikalelewa na kuota mizizi. Bahati mbaya sana mazoea yalipojenga tabia, ikatokea nguvu ya kuwashikisha adabu na kuikomesha tabia hiyo. Tabia ilivyodhibitiwa vilivyo wale waliokuwa wanazikataa siasa za uanaharakati na kukuosoa tu wakaanza kuikacha CDM. Utekelezaji wa madai na urekebishaji wa makosa ukaiacha CDM haina hoja ya kisiasa. Watakosoa nini tena? CDM mara ikageuka, ikaanza kuwatetea iliyokuwa inawatuhumu, wananchi wakawashangaa, CDM ikazidi kupoteza muelekeo, dhamira yao haikueleweka miongoni mwa wananchi.

Madai ya CDM kuwa wasanii yakashika. Ikaonekana yale mamilioni aliyokuwa akipewa Mbowe na akina Kinana na Mkono yakapata uhalali, Majibu ya kuwa na uhusiano nje ya siasa na kufahamiana yakashindwa kujibu swali mipaka ya kufahamianà akina Mbowe na akina Kinana. Inawezekana ushamba was jamaa ndio ukazidisha chuki ya Mbowe kwa awamu iliyokataa kumdekeza na kumhonga ikazidi. Wabunge vijana wa Mbowe wakazidisha matusi kwa viongozi was kitaifa na nchi kiujumla.

Uchaguzi was ndani was CDM umekuwa dalili ya kuthibitisha ugonjwa was kuwepo makundi yanayosigana juu ya namna chama kinavyoendeshwa.

Kundi harakati na vurugu linaelekea kushinda kushika nafasi, lakini kundi siasa proper limeshinda kwa kuwaeleza na kuwaelekeza watanzania nini hasa kinaendelea ndani ya chadema.

Mbowe anafahamu madhara na nguvu ya kundi hili ndani ya chama chake. Anawafahamu wanaopinga siasa za namna hiyo waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki na anawafamu wana mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki.

Wale waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao mioyo yao haipo kabisa CCM, kuna uwezekano mkubwa wakamfuata Zitto Zitto Act na wale wengine wakarudi nyumbani kwao.

Ajenda kwenye siasa za Tanzania kwa sasa ni sumu haijaribiwi kwa kuonjwa. Hizi ni tuhuma nzito kutolewa na mtu aliwahi kuwa mwenyekiti wa usalama wa Taifa.

Tuhuma za kumuua Chacha Wangwe, kujaribu kumdhuru Zitto, kumpa nafssi ya personal assistant Saanane kisha kumpoteza kutokana na misimamo take na mawasiliano take na Dr Slaa na hata wasiwasi wa kushiriki katika jaribio LA kutaka umuondoa Lissu sio tuhuma kubwa kama kumtia hofu aliyekuwa mwandamizi wa nchi anayelindwa na nchi.

Mbowe hapa anafanya mawili, kusahulisha tuhuma zake na pili kujaribu kunasua chama chake. Kujifanya kaachana na siasa za ulaghai na utapeli, siasa za harakati na vurugu, siasa za kudhuriana na kupotezana na kujifanya muungwana, siasa za Lazaro Nyalandu.

Lema, Jacob, Halima Mdee na viongozi wake, au genge lake kama alivyoliita Sumaye si wa siasa hizo, kamwe hawawezi kubadilika na hawataki kubadilika lakini wamelazimishwa kuigiza kubadilika na upepo wa kutoaminika na kutokukubalika tena, Mbowe anajaribu kubadili gia kuwatoa kwenye matope. So rahisi kufanikiwa katika siasa za Magufuli
Mkuu naona unajibu kwa niaba ya chama tawala ili kuridhisha mwenyekiti Wa chama chako
 
Kimsingi tayari Mbowe na wenzake wameona kuwa mambo yakienda kama yalivyo Chadema itaangamia bila kujali kuwa njia zinazotumika kuwaangamiza ni za halali au sio za halali. Hivyo, Ishu kubwa pale ilikuwa ni kutaka maridhiano, kutaka waachiwe nafasi kidogo na wao kucheza mchezo wa siasa bila kubanwa kama ilivyo sasa na hili limekuja baada ya yaliyotokea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa!
 
Ingawa kuna angalizo kutoka kwa mtoa mada (mwanzisha uzi huu) mimi sijijui kama nipo katika iyo category ya hao 'great thinkers' ila maoni yangu ni haya hapa;

Mosi, kuna usemi wa kikubwa na wa maana sana unaosema "If u cant beat them, join them".
Hili la wakina Mbowe na wenzake kubariki na kurudisha mpira kwa kipa ni strategy tu ya kutaka mambo yao yaende poa.
Unaungana nao, unasoma mbinu zao, mipango yao na mwisho wa siku inakua rahisi kutaka kufanya lako lolote.

Tunajua kundi hili fika toka mwaka flani baada ya uchaguzi mkuuu ilikua ndo mwisho wao wa kufanya siasa majukwaani na mitindo kama iyo maana hata vikao vya ndani ilikua mbinde sana kuifanya na kuisha bila zengwe.
Sasa kurudi na kukubali kwa namna moja au nyingine ni kurudi kwenye matakwa ya serikali kuu ni kutaka huruma ya Serikali na mwisho wa siku ionekane kundi hili ni watu wao na hata wakitaka kufanya lolote hawatakua hawana madhara (huwezi kumuogopa mwenzako katika hema moja kulala bila kujifunika)

Hapa ni tatizo kabisa kwa aliyekubali kumpokea mwenzake maana amekaribisha adui sebleni na akitaka kulipua yanayotaka kulipuliwa ni rahisi sana maana atajua mbinu za mchezo na mchezo wenyewe (eeeh si wapo sawa sasa hivi) na usishangae hata miezi 6 isipite wakaribishwe nyumba nyeupe.

Pili na la mwisho, 2020 inakuja.
Nani asiyejua jumuiya za watu wa ulaya karata ya mwisho ya kutusema vibaya na kutaka kuthibitisha dunia kwamba kwetu hakuna demokrasia ni uchaguzi mkuu wa 2020?
Uchaguzi wa serikali za mitaa umepita kwa makelele mengi na kigingi iko cha kusemwa hatuna demokrasia na vyama vya upinzani vilikandamizwa tumevuka na mabingwa ni sie. Sasa basi kundi ili limerudi kwa kuchanga karata zake kwa kupitia hoja ya 'tunashirikiana nao ila wao ndio hawatutaki'.

"Tumeridhia kukubali serikali hii na utawala wake ambao tuliukataa tu kama siku ya leo miaka 4 iliyopita ila hawataki kutupa uhuru wa kufanya siasa safi, kusema na wanachama wetu, kutafuta uwakilishi kupitia wabunge wetu na madiwani wetu". Hayo ndo yatakua maneno ya kundi hili baada ya uchaguzi mkuu wa 2020 kwa waangalizi wa kimataifa na jumuiya zao.

Viva Tanzania, Viva Magufuli.
 
katika utawala wa awamu ya tano kumekuwa na hofu kubwa miongoni wadau na wabia wa siasa na serikali kupelekea kupungua kwa kiasi kikubwa hali ya kujiamini na hivyo kufifishwa fikra huru.

na katika miaka minne tu ya utawala huu, chadema kimepata mapigo makubwa huenda kuliko miaka yote ya uhai wa chama. sambamba na ukweli kwamba ustawi wa demokrasia umetetereka lakini pia hofu, wasiwasi na mashaka tele ndani na nje ya ccm. wengine kusotea mahakamani, mahabudu na wengine kwenda kupiga magoti kuomba msamaha kwa baba.

viongozi wa dini walitarajiwa kama ilivyokuwa awamu zilizopita kwa umoja wao kukemea au kusaidia kuweka uwiano kwa ushauri wao pale ambapo mambo yakienda kombo. lakini nao kwa kiasi kikubwa labda kwa makusudi au hofu wameshindwa kutimiza wajibu zao. sasa imekuwa ni kiongozi wa dini mmoja mmoja au dhehebu fulani tu ndio linakemea, inakosa uzito.

nani amfunge paka kengere? baada ya mbinu za mbio, kujificha kushindwa, lakini ungali unahitaji kuishi mazingira anayoishi paka...?

Mbowe ameitumia vema sikukuu ya miaka 58 ya uhuru sio tu kukisaidia chama chake lakini kwa maslahi ya muhstakabali mzima wa siasa za nchi yetu. kuanzia sasa dhoruba zozote za ukandamizaji zitaendelea watanzania wote tukijua nani asiyetaka. UPENDO, MSHIKAMANO, KUHURUMIANA NA UTENGAMANO WA TAIFA LETU. KILA MMOJA AKIHISIAMANI MAHALA POPOTE HALIPO.
 
Ndugu, hizi ni siasa za great thinker and a team of hood planners. Baada ya upinzani kwa muda wa miaka mitatu, na kuona matokea ya plan zao kutozaa katunda, ni lazima kujipanga upya na kujenga mbinu mpya.

I commend Mbowe and his team, kutafakari nankuanza marekebisho, yatakayo weza kukiokoa na kukijengea hadhi ya chama chao. They need to recollect themselves , heel their wounds, streamline the feuds within and strategize for a way forward.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Asante sana Genta, huu uzi ni mfano mzuri wa tabia za wapenda na wapigania demokrasia, haki, utu, kuheshimiana na usawa katika nchi yetu. Wanapambana kila siku kuikosoa serikali na taasisi nyingine kutotenda haki wakati wenyewe hawawezi kuishi demokrasia, haki na yote wayapiganiayo.

Tabia hiyo pia ndio inayomfanya Mbowe hii leo ashiriki sherehe za Uhuru na kuomba suluhu.

Hats kabla ya kuja Lowasa, tayari CDM kulikuwa na kilio cha ndani kuwa tufanye siasa, proper siasa badala ya uanaharakati. Arusha walikuwa na malalamiko juu ya siasa za uchonganishi, za vurugu na zenye kutia hasira za lema kuwa zinaua chama. CDM haikusikia,

Zitto alipozikataa siasa za jinsi hiyo na kina Mwigamba na kuja na kauli nchi kwanza chama baadae, wasimamizi wakuu wa siasa za harakati, zenye kutia hasira, siasa za kujenga mpasuko wakamshughulikia.

Lowasa, baada ya CDM kushindwa uchaguzi akaja na mawazo ya kukijenga chama imara. Wazo likiwa lile like, kufanya siasa proper na kuachana na siasa za kiharakati, siasa za kukosoa zaidi kuliko kujenga mipango mbadala na kuuza sera. Lowasa nae akaonekana ameishiwa na bado ni CCM.
Akiwa ndani ya CDM akakosewa heshima na vijana wenye damu ya kiharakati wenye kuweza kusema lolote iwe laivu au kwenye mitandao. CDM kikawa chama cha Kambale kama alivyojionea mzee wangu Juma Duni Haji. Kila mtu ana mamlaka, hakuna utaratibu, hakuna heshima ili mradi tu uwe mwanaharakati na uwe na hamu ya kukamatwa utiwe jela. Sifa kubwa ya CDM ikawa uwezo wa kumtemea mtu mbovu, kuwa tayari kwenda jela au kupigwa na polisi.

Hali ilivyozidi ikabidi mwenyekiti aseme, gharama ya mahakamani, kuwekeana dhamana na mambo kama hayo ikawa kubwa. Chama kinachopigania demokrasia kikawa tayari kutoheshimu haki za watu na utawala wa sheria. Chuki iliyopandwa miongoni mwao ikawa kali kiasi cha kuwa tayari kuiuza nchi kwa maadui wetu eti kisa tu CCM iko madarakani.

Tabia hiyo ya CDM ikalelewa na kuota mizizi. Bahati mbaya sana mazoea yalipojenga tabia, ikatokea nguvu ya kuwashikisha adabu na kuikomesha tabia hiyo. Tabia ilivyodhibitiwa vilivyo wale waliokuwa wanazikataa siasa za uanaharakati na kukuosoa tu wakaanza kuikacha CDM. Utekelezaji wa madai na urekebishaji wa makosa ukaiacha CDM haina hoja ya kisiasa. Watakosoa nini tena? CDM mara ikageuka, ikaanza kuwatetea iliyokuwa inawatuhumu, wananchi wakawashangaa, CDM ikazidi kupoteza muelekeo, dhamira yao haikueleweka miongoni mwa wananchi.

Madai ya CDM kuwa wasanii yakashika. Ikaonekana yale mamilioni aliyokuwa akipewa Mbowe na akina Kinana na Mkono yakapata uhalali, Majibu ya kuwa na uhusiano nje ya siasa na kufahamiana yakashindwa kujibu swali mipaka ya kufahamianà akina Mbowe na akina Kinana. Inawezekana ushamba was jamaa ndio ukazidisha chuki ya Mbowe kwa awamu iliyokataa kumdekeza na kumhonga ikazidi. Wabunge vijana wa Mbowe wakazidisha matusi kwa viongozi was kitaifa na nchi kiujumla.

Uchaguzi was ndani was CDM umekuwa dalili ya kuthibitisha ugonjwa was kuwepo makundi yanayosigana juu ya namna chama kinavyoendeshwa.

Kundi harakati na vurugu linaelekea kushinda kushika nafasi, lakini kundi siasa proper limeshinda kwa kuwaeleza na kuwaelekeza watanzania nini hasa kinaendelea ndani ya chadema.

Mbowe anafahamu madhara na nguvu ya kundi hili ndani ya chama chake. Anawafahamu wanaopinga siasa za namna hiyo waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki na anawafamu wana mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki.

Wale waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao mioyo yao haipo kabisa CCM, kuna uwezekano mkubwa wakamfuata Zitto Zitto Act na wale wengine wakarudi nyumbani kwao.

Ajenda kwenye siasa za Tanzania kwa sasa ni sumu haijaribiwi kwa kuonjwa. Hizi ni tuhuma nzito kutolewa na mtu aliwahi kuwa mwenyekiti wa usalama wa Taifa.

Tuhuma za kumuua Chacha Wangwe, kujaribu kumdhuru Zitto, kumpa nafssi ya personal assistant Saanane kisha kumpoteza kutokana na misimamo take na mawasiliano take na Dr Slaa na hata wasiwasi wa kushiriki katika jaribio LA kutaka umuondoa Lissu sio tuhuma kubwa kama kumtia hofu aliyekuwa mwandamizi wa nchi anayelindwa na nchi.

Mbowe hapa anafanya mawili, kusahulisha tuhuma zake na pili kujaribu kunasua chama chake. Kujifanya kaachana na siasa za ulaghai na utapeli, siasa za harakati na vurugu, siasa za kudhuriana na kupotezana na kujifanya muungwana, siasa za Lazaro Nyalandu.

Lema, Jacob, Halima Mdee na viongozi wake, au genge lake kama alivyoliita Sumaye si wa siasa hizo, kamwe hawawezi kubadilika na hawataki kubadilika lakini wamelazimishwa kuigiza kubadilika na upepo wa kutoaminika na kutokukubalika tena, Mbowe anajaribu kubadili gia kuwatoa kwenye matope. So rahisi kufanikiwa katika siasa za Magufuli

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
1. Mbowe amegundua kwa muda wa miaka minne toka Magufuli aingie siasa za uanaharakati hazijawasaidia zaidi ya kuwadidimiza. Hili lowasa aliwaonya mapema na prof kitila mkumbo aliwahi kuonya mapema.
2. Amegundua Magufuli hana mpango na upinzani na kadiri wanavyosusa na kumpiga mawe ndio wanazidi kujiwekea mazingira magumu kisiasa. Hivyo kujisogeza ni kujaribu kumbadilisha mentality dhidi yao na pengine kujaribu fursa iliyobakia.
3. Amegundua uungwaji wa Magufuli unazidi kuongezeka. Hili utagundua zaidi anapokuwa ziarani. Na hii ni sababu ya jitihada zake za kumkomboa mtu wa chini. Umeme wa REA, maji, vivuko, vituo vya afya kila kona, kwa saaa ofisi za serikali zinaingilika na huduma unapata.
4. Wamegundua Magufuli sio mwanasiasa wa maneno, vijembe na michakato. Ni mtu wa matokeo sasa yaani big results now. Anasema kinatekelezwa. Yupo tayari kazi ifanywe hadi usiku eg. machinjio ya vingunguti ambayo haina hata miezi miwili imefikia 60% toka atoe tamko wakati ilikuwa ardhi tupu.
Ni mengi ika yatosha kusema hayo machache.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
1. Tindu lissu risasi 38
2. Viongozi wa chadema wanasota mahakamani kila siku
3. Wanaharakati wa chadema wanatekwa/kuuwawa
4. Marufuku mikutanao ya hadhara
5. Sheria mpya ya vyama vya siasa lengo kukandamiza upinzani
7. Viongozi wa upinzani kufilisiwa
8. Rafu chaguzi za mtaa
9. Madiwani wa upinzani kuhamia CCM

Uchaguzi mkuu unakuja.......

1. Vyombo vya ulinzi na usalama vipo chini ya makada wa ccm (wakuu wilaya na mkoa)
2. Tume ya Uchaguzi NEC ipo chini ya Rais

Hapo unatokaje kwa mfano MARIDHIANO NI LAZIMA KWA USTAWI WA UPINZANI.

Kama kuna ' Critical Thinking ' ya ' Kipumbavu ' katika Michango yote iliyochangiwa na ' Members ' hii itakuwa inaongoza.
 
Pale Leo aliwahiwa sumaye maana uenda isingetumika mbina ya kuwepo uongozi angepewa airtime aharibu taswira nzuri ya chama kakutana na akil kubwa kaanza kupingeza awamu ya tatu maana lengo lake watu wametibua ni akili tu
 
Wakati wa amani jiandae kwa vita na wakati wa vita jiandae kwa amani. Hakuna kinachodumu milele. Nyakati zimebadilika - kumekuwa na stratejia mpya kwa upande wa CHADEMA. Ninadhani uchaguzi wa serikali za mitaa (kwa jinsi ulivokosa mwamko) umeonekana kama ni upinzani kwa jambo fulani ambalo CHADEMA wanaweza kulitumia kuelekea uchaguzi wa 2020!
 
Nyuma ya pazia hali ya kisiasa ndani ya CHADEMA inashiria siyo "kubadili gia angani", kawaida yao, bali M/Kiti Mbowe anabadili "gia ardhini".

Kimsingi kubadilika huku huenda kukatokana na kutambua kuwa upepo wa kisiasa, kuelekea Uchaguzi Mkuu, 2020, baada ya kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (nguzo muhimu kupata ushindi katika Uchaguzi Mkuu), unaelekea kukitupa CHADEMA nje kabisa.

Isitoshe, wimbi la viongozi wake kukihama chama si dalili njema kabisa kwa afya ya kisiasa, nchini.

Pengine, utendaji wa Serikali ya CCM, chini ya uongozi wa M/kiti wake Rais Magufuli, unaviweka katika mtihani mgumu, vyama vya siasa jinsi ya kuwashawishi wapiga kura ifikapo 2020.

Mbali na hoja hizo, kitendo cha Rais Magufuli kuwapa fursa wao kuongea na WaTz leo kwenye sherehe za Uhuru, kilikuwa ni cha "kitendawili tega". Wahusika badala ya kuwasilisha hoja zenye kugusa WaTz walitumia fursa hiyo kutetea ubinafsi katika kivuli cha kudai "demokrasia" kana kwamba nchini hakuna demokrasia.

Yafuatayo ni maneno yao Mbowe na Lipumba waliyoyasema kwenye fursa hiyo, ambauo kimsingi hayawakilishi mahitaji ya muhimu ya wapiga kura:-

Ninamuomba Mwenyezi Mungu siku ya leo ikafungue milango, tuweze kuishi kama Taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu Demokrasia, tukajenge Taifa lenye upendo na mshikamano na Mh Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika Taifa, kwani kuna wengine wanalalamika, wengine wanaumia, kaliweke Taifa katika nafasi ya utengamano, Mbowe.

Natoa pongezi kwa Watanzania wote, kwa kusherehekea miaka 58 ya Uhuru, mimi nilikua naingia darasa la nne, nampongeza Rais kwa kazi aliyoifanya, namuomba ajue anajukumu la kujenga demokrasia kwenye nchi yetu kuelekea Uchaguzi 2020, Profesa Lipumba.

Back
Top Bottom