Kwenye hili nahitaji ‘Critical Thinking' tafadhali kama unajijua huna au hujabarikiwa nayo usipoteze muda wako

Nachokiona JPM anakosa watu wakumwambia ukweli kuhusu matendo na matamko yake, waliokaribu wanamwogopa na kumpa ushauri mbaya( mfano Uchaguzi wa serikali za mitaa). Ambao wako mbali na hawawezi kumfikia ( niwaite wapinzani, wengi tumewapa jina hilo hata kama sio wanasiasa) ambao wanaweza kumweleza ukweli wenye furaha na mchungu, ni wanasiasa wapinzani na baadhi ya viongozi wa Dini. Mbowe kajisogeza nafikiri kupata nafasi ya kumpa ukweli wa ukweli kuhusu utawala wake na hali halisi ya watanzania. Wameona JPM haguswi na wala habadiliki kwa kuambiwa ukweli kwenye media( kama zipo). Akifanikiwa CHADEMA Kitasimama imara.
 
Mbowe, Lowassa, Sumaye, na kundi lao ni waumini wa dini zinazohubiri kusamehe wamekuwa wakihubiri kusamehe, ng'ambo ya pili naye Mfalme anahubiri kusamehe, hivyo basi imefika mahali wote wamejitambua kuwa wanachokuhubiri sicho wanachokitenda, yawezekana dhamira zimewasuta wakaamua kutazama maslahi ya nchi badala ya mizozo na kuumizana.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Sababu za Chadema kuazimia kuhudhuria kwa maoni yangu ni kama zifuatazo;

1. Hoja za Chadema kukosa nguvu.
Hii ni kutokana na Chadema wenyewe kuanza kukosa uhalali wa kuhoji suala zima la demokrasia.
Wengi walikuwa na hamu kuona jinsi Chadema kinavyokuwa mstari wa mbele kuonesha demokrasia ya kweli lakini umekuwa kinyume chake.Sababu zipo na mifano ipo wazi.
Hoja kama ya kupinga ufisadi imekufa na siyo agenda ya Chadema tena.CCM wameiteka na tunaona wanavyoifanyia kazi kwa spidi kama askari wa miavuli.

2. Kuonekana wazi kwa maendeleo ya miundo mbinu kama barabara,reli,nishati na kuimarika kwa usafiri wa anga na maji.Hii inafanya iwe vigumu sana kuwashawishi wananchi wasione na waanze kufikiri chama mbadala.Pamoja na kuwepo ugumu wa maisha lakini dalili zilizopo zinawapa matumaini wananchi wakiamini huenda huu ni mwanzo tu na hali itakaa sawa.

3. Kuimarika kwa nidhamu ya kazi serikalini ikiwa ni pamoja na kupungua sana kwa uonevu,kutotoa haki kwa waliopewa dhamana,na urasimu usiokuwa na sababu.Hata kama kuna sehemu bado hazijakaa sawa lakini ile hali ya mh.Magufuli kuchukua hatua za haraka kukemea na kuonya mara agunduapo 'madudu' ya jinsi hiyo yanafanywa,kunawafanya wananchi wawe na matumaini sana.Na zaidi pale wananchi wanapoona safu aliyonayo ikiongozwa na mh.Kassim Majaliwa jembe jingine hatari sana.

4. Faida za Chadema kuhudhuria ni nyingi na zinafanya wananchi waone kwamba kumbe ni wastaarabu licha ya kukutana na changamoto nyingi katika utendaji wao kisiasa.Hasara ya wao kutohudhuria ingekuwa kubwa zaidi kwani wananchi wengi hawaguswi sana na maumivu wanayoyapata wao Chadema na hivyo wangebaki wakiwashangaa tu kwa nini wanasusia ili hali Rais akitekeleza mambo mengi ya kimaendeleo na yanaonekana.

5. Mh.John Pombe Magufuli licha ya mambo ya maendeleo,ameonesha kuwa yeye ni binadamu mwenye huruma na mwenye msamaha.
Kuna mambo kama ya kusamehe wafungwa ambao walihukumiwa kunyongwa tangu enzi za Utawala wa awamu ya kwanza hadi leo yameleta hisia sana kwa wananchi na kumuona mtu huyu ni mwenye moyo wa pekee sana.
Kwa mambo kama hayo amejipatia wafuasi wengi sana na hivyo wanamchukulia kama mzazi hata kama atateleza katika kauli,watanzania wengi walishamsamehe pia

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Nachokiona JPM anakosa watu wakumwambia ukweli kuhusu matendo na matamko yake, waliokaribu wanamwogopa na kumpa ushauri mbaya( mfano Uchaguzi wa serikali za mitaa). Ambao wako mbali na hawawezi kumfikia ( niwaite wapinzani, wengi tumewapa jina hilo hata kama sio wanasiasa) ambao wanaweza kumweleza ukweli wenye furaha na mchungu, ni wanasiasa wapinzani na baadhi ya viongozi wa Dini. Mbowe kajisogeza nafikiri kupata nafasi ya kumpa ukweli wa ukweli kuhusu utawala wake na hali halisi ya watanzania. Wameona JPM haguswi na wala habadiliki kwa kuambiwa ukweli kwenye media( kama zipo).

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Mkuu GENTAMYCINE unawatisha wachangiaji.

Critical thinking inatofautiana Kati ya mtu na mtu.

Waache watu watoe maoni yao.

Tatizo la huyu bwana mkubwa huwa anafikiri wapo baadhi ya Watu hawezi kujadiliana nao na kuwaona kama Takataka flani hivi.Hili ni Jukwaa huru ukisha chora Mstari wa Majadiliano tayari huo ni Ubaguzi wa wazi kabisa.
 
Mliokuwa mnasema kuwa niache kila Mtu ( hata Mapopoma ) kwa mfano mmeona sasa shirima Mathias alivyochangia kwa Dhihaka na Uchokozi dhidi yangu? Siku zingine ninapokuwa nasema kuwa kuna Watu tunao hapa wana ' Upumbavu ' mwingi na ndiyo huwa wananikera hadi nawajibu hovyo muwe mnanielewa tafadhalini sawa? Huu Uzi nimeuanzisha ' Makusudically ' kabisa ili utusaidie kwa vingi na mengi hasa kama ' Great Thinkers ' lakini linatokea tu ' Popoma Jiandamizi ' Moja kama hilo hapo juu linaanza ' Kupopomika ' zake hapa.

Kama Mtu kaandika Upumbavu si unaachana nae Mkuu ,wewe kwa uelewa wako unafikiri Watu wote wanaweza kufikiri sawa sawa ?。
 
Kwa mtazamo wangu naona CDM wameangalia mbali hasa mstakabali mpana wa chama kuelekea uchaguzi mkuu 2020 wote ni mashahidi kikichotokea kwenye Uchanguzi wa Serekali za mtaa ndicho amabacho kitatokea kwenye uchaguzi 2020, wanajua kuwa wanadhibitiwa kila nyanja bungeni, uraini na nk.

Si vema kutumia mbinu zile zile kupambana na JPM ukitegemea kupata matokeo tofauti njia pekee ambayo huenda ikaleta nafuu ni njia ya maridhiano sasa unaanzaje? ndiyo hivyo kushiriki kwenye mialiko ya kitaifa hunda baadaye kutakuwa na mazungumzo ya maridhiano.

Tuache ushabiki wa kivyama tupiganie utaifa zaidi tuache misigano ya kichama ambayo adhari zake ni kibwa kuliko hata faidi za kibinafsi.
 
Tatizo la huyu bwana mkubwa huwa anafikiri wapo baadhi ya Watu hawezi kujadiliana nao na kuwaona kama Takataka flani hivi.Hili ni Jukwaa huru ukisha chora Mstari wa Majadiliano tayari huo ni Ubaguzi wa wazi kabisa.

Na Wewe leo ni wa Kusema haya Mkuu?
 
Kwa mtazamo wangu naona CDM wameangalia mbali hasa mstakabali mpana wa chama kuelekea uchaguzi mkuu 2020 wote ni mashahidi kikichotokea kwenye Uchanguzi wa Serekali za mtaa ndicho amabacho kitatokea kwenye uchaguzi 2020, wanajua kuwa wanadhibitiwa kila nyanja bungeni, uraoni na nk

Si vema kutumia mbinu zile zile kupambana na JPM ukitegemea kupata matikeo tofauti njia pekee ambayo huenda ikaleta nafuu ni njia ya maridhiano sasa unaanzaje? ndiyo hivyo kushiriki kwenye mialiko ya kitaifa hunda baadaye kutakuwa na mazungumzo ya maridhiano.

Tuache ushabiki wa kivyama tupiganie utaifa zaidi tuache misigano ya kichama ambayo adhari zake ni kibwa kuliko hata faidi za kibinafsi.

Hizi ndizo ' Critical Thinking ' ninazozitaka. Asante Mkuu wa Uchambuzi wako ulioenda Shule na kwa Kunielewa vyema kabisa.
 
Ndugu, hizi ni siasa za great thinker and a team of hood planners. Baada ya upinzani kwa muda wa miaka mitatu, na kuona matokea ya plan zao kutozaa katunda, ni lazima kujipanga upya na kujenga mbinu mpya.

I commend Mbowe and his team, kutafakari nankuanza marekebisho, yatakayo weza kukiokoa na kukijengea hadhi ya chama chao. They need to recollect themselves , heel their wounds, streamline the feuds within and strategize for a way forward.
 
Nimewatazama akina sugu, na Lema wakati mbowe anaenda jukwani. Nyuso zao japo ile kamera haikuwamulika sana, walionekana ni watu ambao wapo pale Kwa amri.

Mbowe kajitahidi kuficha hisia kaongea kiume fulani chenye uchungu moyoni, pale wameenda Kwa amri.

Angalia wakati mheshimiwa anatoka, nao wamejivuta Kwa shida kumpa mkono.

Kama siyo amri wameitikia mwaliko kwamba no way out, tumeshikwa, kesi kila kona.

But si Kwa mapenzi wameenda pale.
 
Ngoja wenye moyo wachangie huu uzi sisi wengine tutasoma na kupita kimya. Ngoja nikasome MOOCS ya critical thinking kwanza.
 
Ni mwanzo mzuri, I mean ni dalili ya moshi mweupe angani...

Tulikuwa tumefika ni pahala pabaya mno kama Taifa...kuwindana kama wanyama wa mwituni.

Let's us pray for.....Tanzania...our mother.
 
Nimewatazama akina sugu, na Lema wakati mbowe anaenda jukwani. Nyuso zao japo ile kamera haikuwamulika sana, walionekana ni watu ambao wapo pale Kwa amri.

Mbowe kajitahidi kuficha hisia kaongea kiume fulani chenye uchungu moyoni, pale wameenda Kwa amri.

Angalia wakati mheshimiwa anatoka, nao wamejivuta Kwa shida kumpa mkono.

Kama siyo amri wameitikia mwaliko kwamba no way out, tumeshikwa, kesi kila kona.

But si Kwa mapenzi wameenda pale.
Acha uchochezi ndugu...
 
Asante sana Genta, huu uzi ni mfano mzuri wa tabia za wapenda na wapigania demokrasia, haki, utu, kuheshimiana na usawa katika nchi yetu. Wanapambana kila siku kuikosoa serikali na taasisi nyingine kutotenda haki wakati wenyewe hawawezi kuishi demokrasia, haki na yote wayapiganiayo.

Tabia hiyo pia ndio inayomfanya Mbowe hii leo ashiriki sherehe za Uhuru na kuomba suluhu.

Hats kabla ya kuja Lowasa, tayari CDM kulikuwa na kilio cha ndani kuwa tufanye siasa, proper siasa badala ya uanaharakati. Arusha walikuwa na malalamiko juu ya siasa za uchonganishi, za vurugu na zenye kutia hasira za lema kuwa zinaua chama. CDM haikusikia,

Zitto alipozikataa siasa za jinsi hiyo na kina Mwigamba na kuja na kauli nchi kwanza chama baadae, wasimamizi wakuu wa siasa za harakati, zenye kutia hasira, siasa za kujenga mpasuko wakamshughulikia.

Lowasa, baada ya CDM kushindwa uchaguzi akaja na mawazo ya kukijenga chama imara. Wazo likiwa lile like, kufanya siasa proper na kuachana na siasa za kiharakati, siasa za kukosoa zaidi kuliko kujenga mipango mbadala na kuuza sera. Lowasa nae akaonekana ameishiwa na bado ni CCM.
Akiwa ndani ya CDM akakosewa heshima na vijana wenye damu ya kiharakati wenye kuweza kusema lolote iwe laivu au kwenye mitandao. CDM kikawa chama cha Kambale kama alivyojionea mzee wangu Juma Duni Haji. Kila mtu ana mamlaka, hakuna utaratibu, hakuna heshima ili mradi tu uwe mwanaharakati na uwe na hamu ya kukamatwa utiwe jela. Sifa kubwa ya CDM ikawa uwezo wa kumtemea mtu mbovu, kuwa tayari kwenda jela au kupigwa na polisi.

Hali ilivyozidi ikabidi mwenyekiti aseme, gharama ya mahakamani, kuwekeana dhamana na mambo kama hayo ikawa kubwa. Chama kinachopigania demokrasia kikawa tayari kutoheshimu haki za watu na utawala wa sheria. Chuki iliyopandwa miongoni mwao ikawa kali kiasi cha kuwa tayari kuiuza nchi kwa maadui wetu eti kisa tu CCM iko madarakani.

Tabia hiyo ya CDM ikalelewa na kuota mizizi. Bahati mbaya sana mazoea yalipojenga tabia, ikatokea nguvu ya kuwashikisha adabu na kuikomesha tabia hiyo. Tabia ilivyodhibitiwa vilivyo wale waliokuwa wanazikataa siasa za uanaharakati na kukuosoa tu wakaanza kuikacha CDM. Utekelezaji wa madai na urekebishaji wa makosa ukaiacha CDM haina hoja ya kisiasa. Watakosoa nini tena? CDM mara ikageuka, ikaanza kuwatetea iliyokuwa inawatuhumu, wananchi wakawashangaa, CDM ikazidi kupoteza muelekeo, dhamira yao haikueleweka miongoni mwa wananchi.

Madai ya CDM kuwa wasanii yakashika. Ikaonekana yale mamilioni aliyokuwa akipewa Mbowe na akina Kinana na Mkono yakapata uhalali, Majibu ya kuwa na uhusiano nje ya siasa na kufahamiana yakashindwa kujibu swali mipaka ya kufahamianà akina Mbowe na akina Kinana. Inawezekana ushamba was jamaa ndio ukazidisha chuki ya Mbowe kwa awamu iliyokataa kumdekeza na kumhonga ikazidi. Wabunge vijana wa Mbowe wakazidisha matusi kwa viongozi was kitaifa na nchi kiujumla.

Uchaguzi was ndani was CDM umekuwa dalili ya kuthibitisha ugonjwa was kuwepo makundi yanayosigana juu ya namna chama kinavyoendeshwa.

Kundi harakati na vurugu linaelekea kushinda kushika nafasi, lakini kundi siasa proper limeshinda kwa kuwaeleza na kuwaelekeza watanzania nini hasa kinaendelea ndani ya chadema.

Mbowe anafahamu madhara na nguvu ya kundi hili ndani ya chama chake. Anawafahamu wanaopinga siasa za namna hiyo waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki na anawafamu wana mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki.

Wale waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao mioyo yao haipo kabisa CCM, kuna uwezekano mkubwa wakamfuata Zitto Zitto Act na wale wengine wakarudi nyumbani kwao.

Ajenda kwenye siasa za Tanzania kwa sasa ni sumu haijaribiwi kwa kuonjwa. Hizi ni tuhuma nzito kutolewa na mtu aliwahi kuwa mwenyekiti wa usalama wa Taifa.

Tuhuma za kumuua Chacha Wangwe, kujaribu kumdhuru Zitto, kumpa nafssi ya personal assistant Saanane kisha kumpoteza kutokana na misimamo take na mawasiliano take na Dr Slaa na hata wasiwasi wa kushiriki katika jaribio LA kutaka umuondoa Lissu sio tuhuma kubwa kama kumtia hofu aliyekuwa mwandamizi wa nchi anayelindwa na nchi.

Mbowe hapa anafanya mawili, kusahulisha tuhuma zake na pili kujaribu kunasua chama chake. Kujifanya kaachana na siasa za ulaghai na utapeli, siasa za harakati na vurugu, siasa za kudhuriana na kupotezana na kujifanya muungwana, siasa za Lazaro Nyalandu.

Lema, Jacob, Halima Mdee na viongozi wake, au genge lake kama alivyoliita Sumaye si wa siasa hizo, kamwe hawawezi kubadilika na hawataki kubadilika lakini wamelazimishwa kuigiza kubadilika na upepo wa kutoaminika na kutokukubalika tena, Mbowe anajaribu kubadili gia kuwatoa kwenye matope. So rahisi kufanikiwa katika siasa za Magufuli
 
1. Mbowe amegundua kwa muda wa miaka minne toka Magufuli aingie siasa za uanaharakati hazijawasaidia zaidi ya kuwadidimiza. Hili lowasa aliwaonya mapema na prof kitila mkumbo aliwahi kuonya mapema.
2. Amegundua Magufuli hana mpango na upinzani na kadiri wanavyosusa na kumpiga mawe ndio wanazidi kujiwekea mazingira magumu kisiasa. Hivyo kujisogeza ni kujaribu kumbadilisha mentality dhidi yao na pengine kujaribu fursa iliyobakia.
3. Amegundua uungwaji wa Magufuli unazidi kuongezeka. Hili utagundua zaidi anapokuwa ziarani. Na hii ni sababu ya jitihada zake za kumkomboa mtu wa chini. Umeme wa REA, maji, vivuko, vituo vya afya kila kona, kwa saaa ofisi za serikali zinaingilika na huduma unapata.
4. Wamegundua Magufuli sio mwanasiasa wa maneno, vijembe na michakato. Ni mtu wa matokeo sasa yaani big results now. Anasema kinatekelezwa. Yupo tayari kazi ifanywe hadi usiku eg. machinjio ya vingunguti ambayo haina hata miezi miwili imefikia 60% toka atoe tamko wakati ilikuwa ardhi tupu.
Ni mengi ika yatosha kusema hayo machache.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom