Asante sana Genta, huu uzi ni mfano mzuri wa tabia za wapenda na wapigania demokrasia, haki, utu, kuheshimiana na usawa katika nchi yetu. Wanapambana kila siku kuikosoa serikali na taasisi nyingine kutotenda haki wakati wenyewe hawawezi kuishi demokrasia, haki na yote wayapiganiayo.
Tabia hiyo pia ndio inayomfanya Mbowe hii leo ashiriki sherehe za Uhuru na kuomba suluhu.
Hats kabla ya kuja Lowasa, tayari CDM kulikuwa na kilio cha ndani kuwa tufanye siasa, proper siasa badala ya uanaharakati. Arusha walikuwa na malalamiko juu ya siasa za uchonganishi, za vurugu na zenye kutia hasira za lema kuwa zinaua chama. CDM haikusikia,
Zitto alipozikataa siasa za jinsi hiyo na kina Mwigamba na kuja na kauli nchi kwanza chama baadae, wasimamizi wakuu wa siasa za harakati, zenye kutia hasira, siasa za kujenga mpasuko wakamshughulikia.
Lowasa, baada ya CDM kushindwa uchaguzi akaja na mawazo ya kukijenga chama imara. Wazo likiwa lile like, kufanya siasa proper na kuachana na siasa za kiharakati, siasa za kukosoa zaidi kuliko kujenga mipango mbadala na kuuza sera. Lowasa nae akaonekana ameishiwa na bado ni CCM.
Akiwa ndani ya CDM akakosewa heshima na vijana wenye damu ya kiharakati wenye kuweza kusema lolote iwe laivu au kwenye mitandao. CDM kikawa chama cha Kambale kama alivyojionea mzee wangu Juma Duni Haji. Kila mtu ana mamlaka, hakuna utaratibu, hakuna heshima ili mradi tu uwe mwanaharakati na uwe na hamu ya kukamatwa utiwe jela. Sifa kubwa ya CDM ikawa uwezo wa kumtemea mtu mbovu, kuwa tayari kwenda jela au kupigwa na polisi.
Hali ilivyozidi ikabidi mwenyekiti aseme, gharama ya mahakamani, kuwekeana dhamana na mambo kama hayo ikawa kubwa. Chama kinachopigania demokrasia kikawa tayari kutoheshimu haki za watu na utawala wa sheria. Chuki iliyopandwa miongoni mwao ikawa kali kiasi cha kuwa tayari kuiuza nchi kwa maadui wetu eti kisa tu CCM iko madarakani.
Tabia hiyo ya CDM ikalelewa na kuota mizizi. Bahati mbaya sana mazoea yalipojenga tabia, ikatokea nguvu ya kuwashikisha adabu na kuikomesha tabia hiyo. Tabia ilivyodhibitiwa vilivyo wale waliokuwa wanazikataa siasa za uanaharakati na kukuosoa tu wakaanza kuikacha CDM. Utekelezaji wa madai na urekebishaji wa makosa ukaiacha CDM haina hoja ya kisiasa. Watakosoa nini tena? CDM mara ikageuka, ikaanza kuwatetea iliyokuwa inawatuhumu, wananchi wakawashangaa, CDM ikazidi kupoteza muelekeo, dhamira yao haikueleweka miongoni mwa wananchi.
Madai ya CDM kuwa wasanii yakashika. Ikaonekana yale mamilioni aliyokuwa akipewa Mbowe na akina Kinana na Mkono yakapata uhalali, Majibu ya kuwa na uhusiano nje ya siasa na kufahamiana yakashindwa kujibu swali mipaka ya kufahamianà akina Mbowe na akina Kinana. Inawezekana ushamba was jamaa ndio ukazidisha chuki ya Mbowe kwa awamu iliyokataa kumdekeza na kumhonga ikazidi. Wabunge vijana wa Mbowe wakazidisha matusi kwa viongozi was kitaifa na nchi kiujumla.
Uchaguzi was ndani was CDM umekuwa dalili ya kuthibitisha ugonjwa was kuwepo makundi yanayosigana juu ya namna chama kinavyoendeshwa.
Kundi harakati na vurugu linaelekea kushinda kushika nafasi, lakini kundi siasa proper limeshinda kwa kuwaeleza na kuwaelekeza watanzania nini hasa kinaendelea ndani ya chadema.
Mbowe anafahamu madhara na nguvu ya kundi hili ndani ya chama chake. Anawafahamu wanaopinga siasa za namna hiyo waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki na anawafamu wana mafuriko ambao bado wapo lakini hawaridhiki.
Wale waliokuwepo kabla ya mafuriko ambao mioyo yao haipo kabisa CCM, kuna uwezekano mkubwa wakamfuata Zitto Zitto Act na wale wengine wakarudi nyumbani kwao.
Ajenda kwenye siasa za Tanzania kwa sasa ni sumu haijaribiwi kwa kuonjwa. Hizi ni tuhuma nzito kutolewa na mtu aliwahi kuwa mwenyekiti wa usalama wa Taifa.
Tuhuma za kumuua Chacha Wangwe, kujaribu kumdhuru Zitto, kumpa nafssi ya personal assistant Saanane kisha kumpoteza kutokana na misimamo take na mawasiliano take na Dr Slaa na hata wasiwasi wa kushiriki katika jaribio LA kutaka umuondoa Lissu sio tuhuma kubwa kama kumtia hofu aliyekuwa mwandamizi wa nchi anayelindwa na nchi.
Mbowe hapa anafanya mawili, kusahulisha tuhuma zake na pili kujaribu kunasua chama chake. Kujifanya kaachana na siasa za ulaghai na utapeli, siasa za harakati na vurugu, siasa za kudhuriana na kupotezana na kujifanya muungwana, siasa za Lazaro Nyalandu.
Lema, Jacob, Halima Mdee na viongozi wake, au genge lake kama alivyoliita Sumaye si wa siasa hizo, kamwe hawawezi kubadilika na hawataki kubadilika lakini wamelazimishwa kuigiza kubadilika na upepo wa kutoaminika na kutokukubalika tena, Mbowe anajaribu kubadili gia kuwatoa kwenye matope. So rahisi kufanikiwa katika siasa za Magufuli