Hanari wana JF, ni muda mrefu hatuja jadiliana hapa lakini hii ni kutokana na mambo mengi ambayo tumekuwa tukijaribu kufanya. Mengi yemefanikiwa na machache yamekuwa kama changamoto kwetu kuendelea kujifunza.
Kwa siku ya leo nilikuwa naomba wadau wenye muda wa kutoa maoni kuhusu tovuti hii mpya ya Kwenye.Bio tovuti hii ni kama ilivyo Linktree lakini hii ikiwa na vitu vingi zaidi na uwezo wa kufanya mambo mengi zaidi. Ningependa yoyote mwenye muda ajaribu tovuti hii kisha atoe maoni anaonaje au kitu gani kibadilike kwenye tovuti hii. Kwa sasa bado yapo marekebisho kadhaa yanayo endelea hivyo popote utakapo shindwa kutumia tovuti hii unaweza kuwasiliana nasi hapa.
Tunasubiri maoni yenu. Tuna tanguliza shukrani za dhati.
Hii ni tovuti ambayo itasaidia watu kulink kwenye vitu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii kama Instagram, Tiktok au mitandao yote ambayo inaruhusu kuweka link moja tu kwenye sehemu ya bio. Mbali ya kufanya kazi kama link ya kwenye bio pia unaweza kutumia kuuza bidhaa mbalimbali kuonyesha kazi zako, na pia hata kukusanya maoni mbalimbali, namba za simu, kuruhusu giveaway na mambo mengine mbalimbali. Pia unaweza kuruhusu watu kutumia bio page yako bila kutoka kwenye ukurasa mmoja unaweza kuona mfano hapo chini.
Tanzania tech ni tovuti ya habari za teknolojia zinazohusu simu, programu, kompyuta, michezo, televisheni pamoja na mambo mengine ya teknolojia.
kwenye.bio
Link hii pia inaweza kupatakina kupitia Google na ina uwezo wa kutengeneza knowledge panel kama ile inayo onekana kwa watu maarufu uk google jina la mtu.