Kwenu woooote mliosoma kigurunyembe sekondari! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwenu woooote mliosoma kigurunyembe sekondari!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by edwinito, Feb 20, 2012.

 1. edwinito

  edwinito JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 211
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari zenu wenzangu wote mliosoma Kigurunyembe Sekondari School, Morogoro.
  Nina hakika kuna ambao mmeshapata hizi habari za kuwa, baadhi ya wanafunzi waliosoma Kigurunyembe, wako kwenye mchakato wa kuanzisha Kigurunyembe Sekondary School ALUMNI!
  Kama huna taarifa hizi, ninachukua nafasi hii kukukaribisha kwenye Kikao chetu cha 4 kitakachofanyika siku ya Ijumaa, tarehe 24/02/2012, saa 12:30 (Kumi na mbili na nusu) jioni, pale Millenium Tower, Mzalendo Pub!
  Nia na lengo la hii Alumni, pamoja na mengine mengi tutakayoyaamua, tumeona ni vema kama siku moja tutakwenda "Shuleni Kwetu" ili kufanya chochote (kupaka rangi jengo/majengo, kuchangia kununua madawati, meza na viti vya waalimu, n.k.).
  Pia tunafikiria kufanya misa maalum ya kuwakumbuka walimu, wanafunzi na hasa kumkumbuka mlezi wetu, Father Kanuti (hapa tunawaalika wale wote ambao waliwahi kuishi hosteli pale mchikichini, ingawa walikuwa wakisoma shule nyingine za jirani, mfano: Forest hill, Jabar Hilal, n.k.)
  Kama u mmoja wapo, tafadhali tuungane ili tuweze kushirikiana katika kuujenga umoja wetu.
  Tunakaribisha pia maoni, ushauri kwa wale walio mbali na TZ.
  Mengineyo unaweza kuni-PM.
   
 2. KILITIME

  KILITIME JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2013
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kuna jambo sikulisikia ni hili hebu nambie kuna linaloendelea?????
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2013
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  .... Mbu nae kasoma kwa mwalimu Magere, Betello, Malima, Mazela, Ally Ali, Mkude na wengi wengineo...na hata hosteli ya Fr Canute alikuwamo pale akitoana mbio na wale jamaa wa band ya Joseph Chai Bado!

  Updates za KNF ndani ya jf?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...