Kwenu wadada; sijui nani kawaroga?

Kwenu wadada; sijui nani kawaroga?

nuporo

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2018
Posts
1,534
Reaction score
3,407
➿➿➿➿➿➿➿➿➿➿

🍇KWENU WADADA🍇

🍇Sijui nani kawaroga?

🍇kwann baadhi yenu mnakua na dharau na kiburi kwa waume zenu?
Ni kweli hamjui thamani ya ndoa au dharau tu?

🍇Mumeo ametoka anaenda kibaruani hata humuagi kwa vizuri una uhakika wa kuonanana nae tena?

🍇Anafika kazini anapata misukosuko ya kila aina, kazi yake pengine ngumu sana, anafokewa na kudhililishwa na boss, ana madeni yote ni kwa ajili ya kutafuta maisha yenu a nachopata mnakula wote pengine hata mamake hampelekei na unafurahia.

🍇Anarudi nyumbani amechoka kama punda anategemea akutane na uso wako ulojaa bashahshaa lakini anakuta na uso ulojaa dharau.

🍇Hata ulipo huinuki kumpokea na kumkaribisha anajipokea mwenyewe, wewe unapiga soga, ama uaangalia movie ama unachati, hata hujali kua mume wako ameingia, unasahau kua huyo ni toafutia na yoyote yule kwenye maisha yako, umuhimu wake kwako hauna Mizani.

🍇Anaelekea bafuni hajatengewa maji akafate maji mwenyewe, akirudi ajipakulie ale peke yake.

🍇Ikifika wakati wa kupumzika anahitaji kitanda kilopambwa kwa ajili yake lakini wapi!!!!!Anakutana na shuka lile lile lilotandikwa wiki mbili zilopita hata mtoto alilazwa na kujisaidia hapo.

🍇Mke nae anapanda kitandani hapo mume anategemea kupata maneno matamu na laini kutoka kwa mke wake,anahitaji angalau faraja yake, anahitaji shukran na dua na kupewa moyo na mke wake hapo anakutana na malalamiko na masimango na kudaiwa hiki na kile.

🍇Sio haya tu mke anapanda kitandani ananuka domo na majasho na kikwapa, ama dera linanuka zaziwa, Mume hisia yote ya kua karibu na Mke inamuondoka.

🍇Aliewaroga nadhani alishafariki Hivi akitafuta mke mwengine na akakukimbia wewe utasema mke mwenza amekoroga? Unadhani unaweza kuupata moyo wake?

🍇Jirekebisheni........ ni ushauri tu
Ukipenda uchukue.🍇
 
Pole kwa uliyokutana nayo, ukijua namna ya kucheza na akili ya mwanamke hutopata shida ya akili hivi na kujiuliza kwanini anabweteka hivi na hafanyi kile.

Mie sijaolewa ila nimesikia watu nwakisema, hukufunzwa namna ya kukaa na mke?? Wazee wako walikuacha uje ulalame tuu hewani...!!

Ukijua tabia ya mtu na ukaitafutia nafasi kwenye maisha yako, huyo mtu hakusumbui kuishi nae na wala hakupi jaka moyo.

K' Matata.
 
Siku zote mwanaume usije kujaribu kumtegemea mwanamke kwa namna yoyote ile sababu wengi wao ni vigeugeu na wasio na upendo kwa waume zao.
 
Pole mwambie, tatizo mkioana wakati penzi bado la moto mnadekezana kumbe mkizidi kukomaa
na tabia inakomaa, ongea naye taratibu
 
Sina chochote chakusema kwa maana hujui kama ameoa kilaza au hujui kama alioa mwanamke mchafu asiyeona uchafu sijui kama aliwekewa limbwata ndio akaoa.
Ila kuna wanawake wanachoka mapema sana sana wakiwa na watoto so msaidie .
Kwani ukimuita ukamwambia itakuwa tabu mbona siunasema ukienda nje ndio umesema au??
Acha utoto basi kua umeoa au umeolewa.
Halafu umeshindwa kufua hayo mashuka ukapasi ukatandika kitandani?
Wewe umeshindwa kumuwekea maji nakumtoa out kumnunulia dedorant nzuri na pyhum nakumuomba kiustaarabu awe msafi .
Wewe maisha hubadilika jitume .
Umewahi kupika chakula hata siku moja ukamualika mkala .
Au fitina visa na unafiki unao .
Madharau huanza pale unapokuwa humuoni kachoka .
Amechoka weka house girl au mjigawe kwa majukumu.
Hakuna kazi nzito kama kulea watu mpaka watu wazima kama wewe.
Mwanamke akiwa nawatoto jaribu kumuelewa .
Kuwa sio kazi rahisi anayokuanzia chakula nguo nyumba na bado mlalane.
 
Pole kwa uliyokutana nayo, ukijua namna ya kucheza na akili ya mwanamke hutopata shida ya akili hivi na kujiuliza kwanini anabweteka hivi na hafanyi kile.

Mie sijaolewa ila nimesikia watu nwakisema, hukufunzwa namna ya kukaa na mke?? Wazee wako walikuacha uje ulalame tuu hewani...!!

Ukijua tabia ya mtu na ukaitafutia nafasi kwenye maisha yako, huyo mtu hakusumbui kuishi nae na wala hakupi jaka moyo.

K' Matata.
Hii nayo ni habari njema
Huwa napata shida sana nitakupataje nitangaze ndoa lakini moyoni najikatisha tamaaa kwamba Kasie ameolewa
Kwa mala ya kwanza leo naomba nitamke hadharani kwamba
"I love u Kasie will u marry me? "
[emoji7][emoji8][emoji7][emoji8][emoji7][emoji8][emoji7][emoji8][emoji7]
 
zisiwe tu ndo na tabia zako

Back
Top Bottom