Kwenu Pro-UKAWA na wapenda mabadiliko

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Wadau,tambueni tu humu mitandaoni kuna watu ambao wamo humu kwa kazi maalumu na wanalipwa kwa hiyo kazi maalum hivyo chochote kinachofanywa na waajira wao watakitete tena kwa nguvu kubwa.

Watu hawa hata siku ikitokea mwajiri wao kaamuru mtu apigwe risasi hadharani watamtetea na wanaweza hata kukupa mfano wa viongozi wengine waliokuwa wanatoa amri za aina hiyo na kukwambia huyu si wa kwanza.

Watu hawa hata ikitokea anaewapa ajira kauza sehemu ya nchi wao watatete na watakwambia katiba inamruhusu na kipengele watakutajia kwa kutumia tafsiri wanazozijua wao.

Humu kuna wengine wameweka mbele ukabila kiaai kwamba wako radhi kuhalalisha makosa hata kama ya kinyama kwa kutumia makosa kama hayo yaliyotangulia au yaliyotendwa na watu wengine.

Hawa ndio wale watakaokwambia mambo haya mnayolalamikia hayakuanza leo na wanajisahaulisha kwa makusudi ukweli kuwa hata huko nyuma matendo haya yalipingwa vikali na kumbukumbu zipo.

Humu wamo baadhi ni wanufaika wa mfumo uliopo either kwa kupewa vyeo wao wenyewe,ndugu zao au jamaa zao hivyo lolote linalofanyika wao kwao ni sahihi tu na mnaoumizwa shauri yenu.

Mfano mzuri ni yule alietetea tukio la mtu kupigwa risasi kwa kusema ni jambo la kawaida tu kwani hata katika nchi za wenzetu mambo haya yanafanyika.

Vile vile humu kuna watu ambao ni wahanga wa yaliyotokea au waliyokuwa wakiyafanya wakati wa kampeni.

Hawa ni wale waliounga mkono watu fulani wakati wa kampeni na sasa wanaona aibu kukuri kuwa walifanya makosa kuwapigia kampeni na badala yake sasa wanaishi kwa kuvizia vitukio fulani fulani ambavyo wanaamini wanaweza kuvitumia kusema mtu fulani ni sahihi hata kama atafanya mambo mabaya mengi kiasi gani.

Pia humu kuna baadhi ya watu wana chuki tu na watu wa upinzani bila sababu yoyote na hivyo lolote analotendewa mpinzani wao wanafurahia na kulitetea hata liwe la kikatili kiasi gani.

Kwahiyo ndugu zangu ni lazima muelewa kuwa binadamu wa leo baadhi yao hawana tofauti kabisa na wanyama mradi tu wao ni wanufaika wa mfumo uliopo hivyo matatizo wanayopata wengi wao hayawahusu.

Chuki iliopo leo hii ni ya kupitiliza na imeondoka kabisa ubinadamu. Tushukuru tu tunaishi katika dunia ambayo leo hii ni kama kijiji vinginevyo hali ingekuwa mbaya sana.

Msisahau pia wale wote waliotesa na kuua binadamu wenzao siku za nyuma hawakukosa watetezi kama tunavyosoma katika vitabu vya historia hivyo hata nyakati hizi watetezi wa ouvu hawawezi kukosekana mradi wao kuna chochote wanapata kutoka kwa hao wanaowaunga mkono.
 
Natumain usha jiandaa kwa tar 26/4 na baada ya sku hiyo natumaini nyuzi kama hizi hazita kuwepo.
 
Wapo wengi humu ambao wamo kwenye payroll ya Lumumba

Mfano halisi ni akina jingalao, YEHODAVA, GUISSE,yule mdada cocochanel and the like
 
Wadau,tambueni tu humu mitandaoni kuna watu ambao wamo humu kwa kazi maalumu na wanalipwa kwa hiyo kazi maalum hivyo chochote kinachofanywa na waajira wao watakitete tena kwa nguvu kubwa.
Hapa unajiongelea wewe kama unavyolipwa na Acacia na kuongelea bombardier
 
Wapo wengi humu ambao wamo kwenye payroll ya Lumumba

Mfano halisi ni akina jingalao, YEHODAVA, GUISSE,yule mdada cocochanel and the like
Hao hata mwajiri wao akiagizwa upigwe risasi watakuja humu kutetea na vifungu vya katiba watakutajia hata kwa kupotosha.
 
Back
Top Bottom