Indoraptor
JF-Expert Member
- Aug 30, 2019
- 251
- 508
Habari wanajamvi,
Kazi ya kuendesha bodaboda imekuwa kitega uchumi kwa vijana wengi hapa nchini, lakini hivi sasa jamii inawachukulia madereva wengi wa bodaboda kama wahuni tu hii ni kutokana na mazingira waliyojiwekea wenyewe
Nitatoa mfano mmoja huenda ikawa msaada wenu pia.
Siku moja nilikutana na rafiki yangu wa kitambo akiwa kijiweni na pikipiki yake akisubiri abiria. Lakini mwonekano wake ulikuwa sio wa kuridhisha kabisa.
Niliamua kumwambia ukweli na kumshauri abadilike jambo ambalo limedilisha mwenendo wa kazi yake, mwenyewe amekiri hata kipato chake kwa siku kimeongezeka na pia sio mtu wa kutegemea kusubiri mteja kijiweni. Kwa sasa kazi zake nyingi ni za simu na za uhakika (Tayari ana vichwa kadhaa ambavyo kila siku ni lazima awape ride). Hii kutokana na abiria kumkubali jinsi anavyoifanya kazi yake
Sasa ipo hivi madereva bodaboda embu jaribuni kuzingatia haya;
1. UENDESHAJI WA CHOMBO (PIKIPIKI)
Sio lazima ukimbize ndo uonekane upo fiti kwenye bodaboda.
Endesha mwendo wa kawaida
Endesha upande unaotakiwa kuendesha
Overtake upande unaotakiwa ku-overtake
Bodaboda wengi wanapopata ajali hata kama wao ndo wapo upande wa haki wataonekana wao ndo chanzo cha ajali kutokana na uendeshaji wao
2. IFANYE PIKIPIKI YAKO IONEKANE KWELI INAFAA KWA USAFIRI
Hapa bwana mnazingua sana kucheza na hizo exhaust zinapiga kelele ambazo hata watu hatuzipendi.
Arusha naona kuna mtindo mpya umeanza wa kung'oa taa ya mbele na kuweka taa ndogo mithili ya 'sportlight' ndo itumike kama taa kubwa(head light)
Embu jaribu kuweka chombo chako vizuri hata abiria asiwe na wasiwasi wa kupanda akidhani ni mbovu.
Weka pikipiki yako safi mda wote.
3. DEREVA MWENYEWE JIWEKE 'SMART'
Hata kama unashinda kijiweni isiwe sababu ya kupauka uso mda wote.
Jaribu kuwa na Hair style inayoeleweka
Sawa tunajua pikipiki inahitaji nguo nzito kwa ajili ya upepo basi ziwe safi na sio oversize
Achana na kunywa pombe mida ya kazi
Hayo ni kwa uchache tu, jaribuni kuzingatia hayo mtajenga uaminifu hata kwa abiria awe na moyo wa kukutafuta anapohitaji usafiri wa pikipiki.
Pendeni kazi yenu, itababili pia jamii inavyowachukulia kwa sasa
NIMEMALIZA