Mwalimu, yaani wewe unapaswa ujue kuwa kazi yako kuu shuleni ni KUFUNDISHA mengine achana nayo...kama kuna wapigaji acha wapige siku wakikamatwa wewe hayata kuhusu....istoshe shule ni ya serikali sasa wewe unawashwa wapi? Nchii hii ni kubwa na wapo wengi wanaoifaidi tofauti na huo uongozi wa shule ...hao Jafo na Ndalichako unao waita wanaishi maisha ya kifahari mfano,
1. Wanaishi kwenye nyumba za serikali
2. Wamejenga makasri ya maana ya kuishi familia zao
3. Wana bima za Afya(green card) za kuwapeleka hadi Ulaya na Amerika wao hadi na mahouse maids wao
4. Watoto wao wanasomea shule za Kifahari na za mamilion
5. Wana mishahara ya mamilioni kila mwezi
6. Posho zao kwa saa moja zinazidi mshahara na kiinua mgongo chako baada ya kustaafu
7.Wanalala ndani nje wamelindwa kwa bunduki, cctv camera, mbwa wa kali na electricity fence
8. Akaunti zao huenda hawajui kuna salio kiasi gani hadi leo
9) Mifugo yao (paka, mbwa, kuku nk) inabajeti ya wiki inayozidi mshahara wako wa miez 6
10) Wanatembelea magari ya kifahari japo ni kodi yako pia
*KIBAYA ZAIDI NYOOTE KWA PAMOJA MNAITWA WATUMISHI WA UMMA*
Sasa wewe mwalimu unawashwa nini.
Ushauri wangu
1) Jitahidi utafute pesa
2) Kazi yako kuu shuleni ni kufundisha mengine ni ziada
3) Si lazima kila mtu kufanya kazi za ziada mfn kusimamia mitihani nk
4) Kwenye mkataba wako uliambiwa utafanya pia na majukumu mengine km yatakuwepo ila hawakuyabainisha...
5) Dunia haijawahi kuwa na usawa kamwe.
6) Jifunze kukubali yaishe
7) Kuna watu wanalitafuna hili Taifa kuliko huyo HM wako na SMT yake
8) Usipoteze muda mwingi kuwaza mambo ya umma bali iwaze familia yako na maisha yako.