MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,754
Poleni wadau na mihangaiko ya maisha iliyoambatana na janga hili mtambuka la covid-19
Niende kwenye mada moja kwa moja,
Wakati serikali ya mkoa wa Dar es salaam ikitambua hatari inayoweza kuwakumba wananchi wa eneo hilo kama hawatachukua hatua madbubuti,
iliamua kuidhinisha uvaaji wa barakoa kua rasmi kwa wakazi wa mji huu japo wapo waliojali afya zao na kuvaa barakoa hizi hata kabla ya kuambiwa na makonda
Tatizo linakuja pale baadhi ya watu wanaposhindwa si tu kuzijali afya zao bali na za watu wanaowazunguka kwa kutokuvaa vifaakinga hivi
Ukipanda daladala huku ukiwa unevalia kibarakoa chako safi kilichoshonwa na fundi Joni,
wapo watu unajikuta upo nao siti moja wapo domo wazi tena utakuta wanakohoa bila mpangilio na kutema mate dirishani bila kujali
Watu hawa ni rahisi sana kuambukiza wenzao kwa kua tunapojiziba pua na mdomo ipo hatari ya kuambukizwa kupitia kwenye macho (nacked eye)
Naziomba mamlaka zinazohusika ziweke ulazima na adhabu stahiki kwa hawa wauwaji wasiovaa vifaa hivi hasa kwenye vyombo vya usafiri ambavyo si rahisi kwa watu kukaa umbali wa zaidi ya mita moja na nusu
Nashauri hivyo pia kwakua vitendo vya chafya na kukohoa ni vitu natural na vinakuja bila taarifa na wakati wowote
# Ramadhan mubaarak