Kweli Ya kale ni dhahabu

Hahaa hii naikumbuka ilikuwaga ni ujinga sana aise
 
Mkuu kwahy unasibitisha kifuu ukikifuka mweny kigugumiz awez kuongea
 
Mkuu kwahy unasibitisha kifuu ukikifuka mweny kigugumiz awez kuongea


Nimeshasema zamani nilipokuwa mtoto nilikuwa naamini hivyo. Imani ni sawa na dini tu, ukishaweka kitu akilini mwako basi unahisi ni ukweli kumbe ni hulka tu. Ila hata hivi sasa kama unataka kuniudhi na kunipa hasira....we jaribu kutembea na kifuu mbele yangu huku ukinionyesha kwa tambo, hapo ndipo utajuwa kwanini utotoni watu walikuwa wananiita Bud Spencer kwa ubabe wangu. Sipendi vifuu ila nazi nakula.
 
Du mvua ikinyesha tulikuwa tunaomba kufika mchana ikatike na jua liwake. Bila jua kutoka tuliambiwa hakuna chakula cha jioni. Ila ninapotoka mvua zikifika saa nane lazima zikatike na jua litoke. Hapo ndo wakati wa kuokota kumbikumbi. Tulikuwa nunaambiwa na walimu tupileke kila mmoja kumbikumbi tano.
 
Niliaminishwa kuuwa nikikojoa sehemu alipokojoa mwenzagu basi matiti ya mama yangu yatakatika [emoji1787][emoji1787][emoji1787] ni kweli wakuu?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Iyo namba 11 mother kanidanganya sana, nakumbuk ilivyo karibia kujifungua mdogo wangu aliniaga kuwa anaenda kununua mtoto hospital.
Nikaamin ivo, baada siku kadhaa akaja na kadogo kangu ka kike nikamwambia Mama umechagua katoto kazuri alicheka sanaa
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Kasomali
 
bilashaka leo wewe ndiye Scorpion!
 
*sisi vitindamimba tulikuwa tunapewa chumvi na kuinama kuirusha nyuma kupitia katikati ya miguu kwamba unazuia mvua ya mawe.

*tuliaminishwa ukimtukana mzee utaota sehemu za siri kwenye paji

*ili kuepushwa kuchelewa mtoni, mzazi alikuwa akitema mate kwenye jani na kusema mkirudi mate yamekauka mnakufa

*ukisimulia hadithi mchana, hukui au usiku hutosinzia

*....... wengine waendelee maana karibu elimu hii ilikuwa universal.
 
mtoo wa mwisho kuzaliwa aliambiwa agonoke juu ili kama kuna wingu mvua isinyeshe watu waendelee na mishe zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…