Stori za wadada wawili ndani ya basi:
Dada 1: Je, ungependa mume wa aina gani?
Dada 2: Awe bilionea.
Dada1: Ukimkosa Je?
Dada 2: Awe milionea.
Dada 1: Je, kama hotopatikana?
Dada 2: Basi mwenye milioni anaweza kunifaa.
Dada 1: Na kama hutofanikiwa kumpata huyo?
Dada 2: Mwenye laki tano.
(Jamaa mmoja alikua siti ya nyuma amelala akamnong'oneza jirani yake)
"Oya wakifika kwenye jero niamshe"