Kweli ukoloni mamboleo umetushika......lo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli ukoloni mamboleo umetushika......lo!

Discussion in 'Entertainment' started by only83, Mar 11, 2011.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Nimekuwa nikijiuliza kwanini watanzania wengi wanapenda kushabikia na kushangilia timu za ulaya..utakuta mtu mweusi kutoka kule Musoma amevaa jezi imeandikwa Chacharito,Rooney nk...katika moja ya policy ya kuingiza ukoloni mamboleo ni kuwafanya watu weusi wadharau mambo yao..ni watu wachache sana wanaovaa jezi za timu kama Simba,Yanga,Azam FC,Mtibwa nk.....Tuacheni utumwa huo jamani turudini nyumbani tuone namna ya kukuza soka letu.....
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145

  Broda naona umekosea jukwaa na kuja kututukana wapenzi wa footy ... ila tumekusikia kwa heri, next time ukirudi Njoo mada yenye kichwa na miguu.. katika soccer hakuna siasa, hakuna udini hakuna ukoloni mambo leo.. NUKTA
   
 3. M

  Matarese JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2011
  Joined: Aug 30, 2009
  Messages: 519
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Kama umekosa la kuandika afadhali ukae kimya!
   
 4. l

  lusuadam Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sidhani kama ni vibaya kuvaa jezi hizo za timu ya kizungu. Sio kuwa hatutaki kuzipenda timu zetu za nyumbani, lakini kuna raha gani kuitukuza timu ambayo kila siku inakupa homa kwa migogoro isiyoisha? Ndani ya mwaka mmoja timu inakuwa haijafanya chochote cha maana, zaidi ya uongozi kuvurugana na kutuhumiana mambo mbalimbali. hata hizo jezi za wachezaji wa kibongo zipo kwani? maana wenzetu kila mchezaji ana namba yake, hata timu ikiwa na wachezaji 40, huku timu ina wachezaji 30, jezi 18, jezi za kubadilishana.

  tunachohitaji ni kujitambua kuwa sisi watanzania na nchi nyingine za kiafrika hatuitendei haki sekta ya michezo. hatuna mipango madhubuti ya kuiimarisha, ambapo ingekuwa ni moja ya sehemu ya kutengenezea ajira kwa vijana mbalimbal
  i
   
 5. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mapenzi ya soka hayana mipaka. Ndio maana jamaa wenye hela zao wametoka Umangani, Russia, US etc kwenda kununua timu kule UK.
  Kuhusu kushabikia timu za ulaya na kusahau timu zetu, mmmhhnn...kama zingekuwa zina maendeleo yoyote nina imani watu wangezisupport, lakini timu hizo Sima/Yanga hazina mbele wala nyuma. Kila kukicha migogoro isioisha.
  Hii ni era ya globalization bana!
   
 6. b

  babacollins JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 879
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Umeshawahi kuwauliza kwa nini wanavaa hizo jezi za nje.Halafu kwani umeshajicheki juu mpaka chini umevaa vitu vya wapi THINK BIG.Ati ukoloni ukisikia mjomba ako anatakiwa kwenda juu utaomba asirudi tena.Tafuta mada.
   
Loading...