Kweli Tambwe Hiza kilaza!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kweli Tambwe Hiza kilaza!!!

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by PatriotMzalendo, Apr 7, 2011.

 1. P

  PatriotMzalendo Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimesoma maoni mengi sehemu tofauti tofauti kama kwenye mitandao na kwenye magazeti machache kwamba mtu wa propaganda wa CCM,Tambwe Hiza, ni mweupe kabisa kichwani. Nilikuwa sijaamini sana lakini leo nimeamini kwamba huyu bwana ni mweupe kuliko weupe wenyewe kichwani kutokana na maoni aliyojaribu kuyatoa kuhusu nini cha kuwemo kwenye katiba mpya.Huyu bwana ni mjinga kwa sababu:-
  • anapinga hoja za kupunguzwa kwa mamlaka makubwa ya rais ya kuteua watendaji mbalimbali wa umma akidhani kuwa mamlaka hayo yanayoshauriwa yapunguzwe ni ya Jakaya Kikwete wa CCM wakati wenye akili wanapendekeza hivyo kwa kuzingatia yeyote anaweza kupenya penya hadi kupata urais hata mpumbavu fulani au katili fulani kama vipengele vingine vya katiba vitatoa mwanya wa kuwezesha hilo, endapo hatutakuwa makini kuandika katiba nzuri.Ikitokea hivyo, rais huyo atafanya uteuzi wa ukichaa kichaa kwa hasara ya taifa.
  • anapinga hoja hiyo bila kujali uteuzi wa rais unarudisha nyuma maendeleo ya watu wa vyama vyote vya siasa kwani wateuliwa hao huwajibika kwa mteuzi na si kwa watu wakiwemo wana CCM.
  • anapinga hoja hiyo bila kufahamu kwamba CCM haitakuwa madarakani milele na hivyo kuna siku rais atatoka upinzani.
  • hana uwezo hata mdogo wa kusoma alama za nyakati kujua kuwa watanzania wa sasa wanataka mabadiliko na hawawezi kumvumilia mjinga yeyote anayejaribu kuturudisha nyuma.Angekuwa na uwezo huo asingetoa hoja ya kijinga na alipoanza kupewa kwa vitendo taarifa na watanzania wenzake kwamba alikuwa anaboa, angenyamaza mara moja badala ya kukomaa kijinga na kuadhirika vibaya.
  • hajui kwamba maoni yaliyokuwa yanatolewa yalikuwa ya wananchi binafsi licha ya baadhi kuwa viongozi wa vyama vya siasa.Kwa ujinga wake yeye eti alikuwa akitoa maoni hayo kama mwakilishi wa CCM! CCM kama entity haipaswi kuwa na maoni mamoja kuhusu nini cha kuwemo kwenye katiba bali watu binafsi ndiyo wenye maoni binafsi hata kama baadhi ya maoni hayo yatavipendelea vyama wanavyoongoza,wanavyokuwa ndani yake au wanavyoshabikia.
  • hajui kwa nini alizomewa! Angekuwa na akili kidogo tu asingeshanga kuzomewa sana na kutakiwa atoke kwa upupu aliokuwa akiongea
  CCM wote nitawaona bogus kama watatoa maoni kichama ya kulaani kilichomkuta bogus Tambwe Hiza.Kweli Tambwe Hiza kilaza!!!
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hakuna mtu bogus kama huyu jamaa...analalamika kuzomewa hajui kuwa ni nguvu ya umma? Hiyo ni dalili na ujumbe tosha kwa hao wezi kuwa watu wamewachoka na CCM..akapeleke ujumbe kwa wakubwa wake...

  Message send....
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  i heard it on bibisi
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ila aibu,maana hata watoto zake watamuona on media,na wakwe je?du

  tumbo hli!!
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,690
  Trophy Points: 280
  Aliongelea wapi upupu huo manake nimemwona TBC akikumbana na nguvu ya umma
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Huyu naye si ni gamba la nyoka mwenye sumu kali kwa watanzania(CCM) nafikiri wakati wa molting atabaki kwenye machaka ili joka lenye ngozi mpya likiwa na sumu ileile litokomee na kuendelea kuwamwagia sumu ya umasikini watanzania
   
 7. Lyceum

  Lyceum JF-Expert Member

  #7
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Tambwe hajui anaongea na watu wa aina gani. Hajui anaongea na wasomi na watu waliochoka maisha magumu. Hajui watz wenye njaa na matatizo lukuki hawana cha kupoteza. Tambwe anaongea kana kwamba amekatwa kichwa. Tabula rasa
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  STD VII, tusimlaumu sana sometimes.
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Na ndio miongoni mwao washauri wa rais wa kutegemewa sana baada akina Sheikh wa Magomeni hao.
   
 10. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #10
  Apr 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Jamani ukisikia ngome ya CCM ndo kina Tambwe, Makamba, Chiligati, RA, EL, JK, Mkono endelea.
   
 11. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #11
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,132
  Trophy Points: 280
  Tambwe Hiza mkali wa kuigiza.
   
 12. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #12
  Apr 7, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Yaani ilikuwa ni kwa mtindo ule ule kama alivyofanyiwa Bagenda pale UDSM majuzi. Wengine tulimuonya Bagenda kwamba umma hawana furaha na yeye kujiunga kambi moja na mafisadi akadhania kwamba namtania mpaka pale alipokumbana na nguvu ya umma ukumbini.

   
 13. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #13
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Ila mambo mengine ni kujiletea aibu ya bure. Hivi kweli CCM wamekosa mtu wa kuwakilisha maoni yao zaidi ya Bwana Hiza?
   
 14. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mawazo yako sawa na yangu,huwa nawaza sana hivi hawa jamaa hua hawana wazungumzaji wa kujenga hoja?
   
 15. Guyton

  Guyton JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 252
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  kiufupi, NYERERE-Mwinyi+Mkapa-Kikwete(tambwe+makamba+chiligati+RA+EL)=HERO TO ZERO

  NAJENGA HOJA.

  ccm sasaivi kimegeuka na kuwa ni chama cha uswaiba, watu wanapewa vyeo sio sababu ya uwezo wao bali ni ukaribu ulionao na wenye mamlaka kama rais, hivyo Tambwe ni sample tu ila viongozi wengi kama wakuu wa wilaya na mikoa, wakurugenzi hawana uwezo wa kufanya kazi wanazopewa, ila bse ni wana ccm na maswaiba wao basi wanapewa vyeo as if vyeo ni zawadi.

  Tambwe na wenzake baadhi lazima watetee mamlaka ya rais sababu wanajua weakness hizi ndo zinawaweka mjini, na mtaona tu na mafisadi wanaotafuta urais 2015 watafanya mbinu zote(bila kujiusisha moja kwa moja) ili kuhakikisha muswaada unapitishwa hatimaye kulinda mamlaka ya rais kwani haya mamlaka ndio silaha yao ya kuwaahidi UVCCM kama akina Shigela kuwapa nyazifa, ili wawaunge mkono.

  Ndg zangu, watanzania wenzangu tusiweke wazo la kushindwa vichwani mwetu, yaani kwenye fikra zetu kwani ushindi uanzia kwenye fikra zen utekelezaji wa fikra ndo unafata, for sure if we'll be guided by this philosophy we'll reach ze Tanzania that we ar dreaming.
   
 16. Zed

  Zed JF-Expert Member

  #16
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 28, 2009
  Messages: 359
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wananchi waliomzomea Tambwe si chuki tu kwa CCM bali ni hoja potofu pia. Mbona Warioba ni mwanachama wa CCm alisikilizwa na baadaye hoja zake zilipigiwa makofi. Tambwe anajaribu kutetea ujinga na sera zilizofilisika! Huku akijua wazi uwezo wake wa kupanga hoja na kupambanua hali halisia ni mdogo sana! Katiba ndio itaipeleka CCM kaburini kabla hata ya wakati wake. Kwa mtindo huu sioni Serikali ya CCM ikifika 2015! Kuna kila alama watanzania wataingia barabarani siku za karibuni!
   
 17. joellincoln

  joellincoln Senior Member

  #17
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mh kazi ipo mwaka huu yetu macho!
   
 18. n

  nndondo JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 534
  Trophy Points: 280
  nakubaliana na wewe, hawawezi kufika 2015 labda kama dunia hii inatawaliwa na shetani, lakini kwa kuwa mungu wa mbinguni ndio tegemeo letu yeye atatupigania kwa namna ya ajabu, mungu ni mwema sana ile tu kujitokeza kwa watu wengi sana Nkurumah na Dodoma ni ishara kwamba watanzania wanataka nchi yao, hawako tayari kuona watoto wao wanaridhi utumwa wao, twende twende watanzania wenzangu
   
Loading...