Kweli mwanaume hela, njemba imeumbuka mbayaaaaaaaaa!

ndyoko

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,971
1,650
Tukiwa ndani ya gari (daladala-naomba msinizodoe jamani) kutoka nkuhungu kuja jamatini mjini dodoma, ghafla tukaona njemba inamshushia kipondo mpenzi wake. Ilibidi tusimame tukihofia huenda jambazi linampora mdada au huenda ndo suala zima la ubakaji. Baada ya kuwaamua, mwanamke akaamua kupanda gari kurudi zake ipagala-nadhani hamu ya sex ilimuishia baada ya kupata kile kipondo.

Mwanaume kwanza alimzuia asipande gari kutoka four ways, lakini mdada akakomaa kwa kusaidiwa nasi abiria, akapanda gari kuja jamatini. Kuona vile ile njemba nayo ikatinga garini. Kasheshe ilianza wakati wa kulipa nauli. Kumbe njemba ilikuwa inamtegeme mpenzi wake eti ndo amlipie nauli, na mwanamke alipogoma kumlipia kasheshe ikawa kati ya konda na njemba. Mwanamke kuona hivyo akashuka zake njiani kabla ya kufika mwisho wa safari.

Ile mwanaume anataka kushuka konda akamkwida shati na kumtaka alipe nauli. Kwa kuwa mwanaume hakuwa na hela, akataka kuleta ubabe, abiria wote tukamchenjia ndipo konda alipomshushia kipondo cha haja hadi jamaa akalegea huku nundu zikianza kumtoka kichwani. Kwa kujua kuwa tukimshusha pale aliposhuka mpenziwe angeweza kwenda kumaliza hasira kwa mpenziwe, konda akaenda kumshushia mbele zaidi kama umbali wa kilomita moja hivi toka aliposhuka mpenzi wake.

My take: Jamani vidume tusiwe tunajifanya 'vibesi' kwa mademu hasa kama unajua akibonyeza kitufe chekundu, we unakuwa kwishney! Na mapenzi ni zaidi ya huo ubabe wako ndani ya nyumba
 
  • Thanks
Reactions: ral
ndyoko na visa vya daladalani sikuwesi.

Jamani si mlinikataza nisipande tena gari ya jirani? Mnataka nitembee kwa miguu? Ndo maana niliweka angalizo pale la kutaka msinizodoe nilijua tu, itakula kwangu. Nimeamua daladala ndo usafiri wangu hivyo sehemu kubwa ya vijambozi vinakotokea si unajua tena status ya watumiaji wengi wa huu usafiri wa umma?
 
"ham ya sex ilimuuishia" vinaingilianaje hapo? punguza nyongeza at!:crazy:
 
Ila tatizo lako na wewe ukishapanda daladala macho yako ni kwa wanawake tu pamoja na masikio yako,unaangalia wanafanya nini na kusikiliza story zao. Uwe unanunua hata gazeti la jiti mzee ukishapanda daladala jikip bize.
 
Huwa nafanya hivyo ndugu yangu lakini wapi bwana! Ni sawa na uwe umelala ndani halafu unasikia 'vilio' vya mahaba toka chumba cha mpangaji mwenzio unadhani usingizi utakuja kweli hapo, thubutuuuuuuuuuu!
 
Sauti za mahaba zikizidi nawewe kula wako

Si mpaka uwe naye, manung'a embe dizani yangu kila unapotuma maombi unaishia kuambiwa huna mvuto basi unakuwa mpole tu ili maisha yaendelee!
 
Jamani si mlinikataza nisipande tena gari ya jirani? Mnataka nitembee kwa miguu? Ndo maana niliweka angalizo pale la kutaka msinizodoe nilijua tu, itakula kwangu. Nimeamua daladala ndo usafiri wangu hivyo sehemu kubwa ya vijambozi vinakotokea si unajua tena status ya watumiaji wengi wa huu usafiri wa umma?

Ndyoko kwa kweli siipendi hiyo avatar yako maana huwa nahisi kuwa kweli unakunywa hayo maji taka ya hicho kingedere.
 
Usishangae kesho ukiwakuta pamoja tena wakiwa wamekumbatiana kwa Mahaba..................Wanawake utawaweza!
 
Ndyoko kwa kweli siipendi hiyo avatar yako maana huwa nahisi kuwa kweli unakunywa hayo maji taka ya hicho kingedere.

Jamani sasa niweke ipi, ile ya mtoto wa kwenye sinia mkanionea gere mkawaambia mods wakaiondoa, na hii nayo hamuitaki, mweeeeee!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom