Kweli mchawi ni mchawi tu

Mtemikwila

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
1,389
Reaction score
1,066
Yule HR (Jinamizi) alieacha kesi kibao na kufukuzisha kazi watu kule kwenye shirika la World Vision, sasa kaleta tafrani kubwa kwenye shirika la PACT-Tanzania..tayari wafanyakazi zaidi ya 40 wamefukuzwa kazi miongoni mwao wapo walioamua kuacha kazi wenyewe baada ya kuona hakuna namna na wasije haribu CV zao.

Jamaa yeye ni mpiga deal wa kiwango cha rami..lakini sasa hivi anawapekua staff wa Pact na akigundua kakosa kadogo tu umeondoka. Pact Tanzania umekua uwanja wa dhuluma na manyanyaso.

Naamini humu ndani wapo watu wa kazi tunaomba waichunguze PACT-Tanzania.
Bless up...
 
Ukifanya kazi vizuri na kwa weledi hakuna atakayekusumbua mkuu,lazima waliotimuliwa wana tatizo,jamaa amekuja kuwanyoosha mnaanza kumletea uzi wa kumuharibia sifa yake,HR piga kazi,hawa janja janja hawana nafasi awamu hii..
 
Mnamchelesha kumlaza nje ya nyumba Yake basi,,nadhani hatofanya ujinga tena.
 
Huyo dawa yake kumloga tu
 
Pact wafanyakazi wengi hamna ushirikiano na wateja nimewahi kuja hapo mara kibao huduma zenu mbovu sana....hata mkitimuliwa wote ni sawa tu waajiriwe watu wanaojituma na wenye kupenda kazi na taasisi yao....huduma mbovu sana tawi la hapo victoria uporoto area...ningepata namba za huyo hr ningemsaidia kutumbua hayo majipu.
 
Sema hilo shirika liko wapi?, linafanya kazi gani?, linafadhiliwa na nani?, lilianzishwa kwa malengo gani na mwaka gani? Mkono wa serikali umo au ni binafsi direct? Hr kahamia kwenye shirika hilo mwaka gani?, alitoka world vision kwa sababu zipi?, majina ya wanaosumbuliwa na huyo HR, na sababu za kuwazingua. Njoo DM .
 
Ukifanya kazi vizuri na kwa weledi hakuna atakayekusumbua mkuu,lazima waliotimuliwa wana tatizo,jamaa amekuja kuwanyoosha mnaanza kumletea uzi wa kumuharibia sifa yake,HR piga kazi,hawa janja janja hawana nafasi awamu hii..
Wote hao wajifanyao kunyoosha huwa ni wapigaji wakuu,sema huwa ni wabinafsi hawataki watu wapate ila wao tu,km afanyavo tembo na mwanae kwa kigezo cha kutetea wanyonge kimaneno.
 
Uonevu ni Mkubwa sana kwa wa chini sema viongozi wakuu uona mambo shwali tu sababu huwa hawapati nafasi ya kukutana na wa chin
 
Duh! utakua ulipigwa chini WVT nini?ulikua cluster gani mkuu?lakini kumbuka maisha siyo kuajiliwa tu,by the way Malekia mbona yuko poa tu!
 
Duh! utakua ulipigwa chini WVT nini?ulikua cluster gani mkuu?lakini kumbuka maisha siyo kuajiliwa tu,by the way Malekia mbona yuko poa tu!
Cluster ndio nn aiseee???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…