Kweli kuna Magari yanayouzwa kuanzia Milioni 2 na kuendelea? Hebu tujadili wadau

Hii siri hata mimi siijui.....unipe.ufafanuzi kidogo maana gari sio injini na body tu kuna vitu vingi.

1. Mfumo wa mafuta
2. Mfumo wa Umeme
3. Seats.
4. Tyres
5. Deaf

Na kupata Board ambayo ni nzima huku gari imeshakufxa njini ni mtiti mwingine.

Baada ya hapo. Gari ukisha assemble si unatakiw kwenda kuisajiri TRA, Kuikagua TBS? Je bado gharama ni hiyo hiyo?
Mkuu,
1. Mfumo wa mafuta ni ule ule
2. Mfumo wa umeme ni ule ule
3. Seats ni zile zile
4. Deaf pia ni ile,

Hapa ninachozungumzia ni kwamba hubadilishi muundo wa gari, bali unatafuta uimara wa gari (hasa upande wa engine), hata plate namba ya gari itabaki ile ile ya body la gari.

. Body zipo nyingi sana mkuu, ni wewe tu ukiwa tayari mambo yanakaa sawa.
 
Sawa nimekuelewa.
 
🔁 Update:
Nimeona kuna mdau ameibuka na kejeli kuhusu uzi huu – akisema magari ya milioni 2 ni hadithi za kufugia kuku.

Ukweli ni huu: Sio kila mtu ameanza maisha na gari ya milioni 10. Wapo Watanzania wanaotafuta usafiri wao wa kuanzia kwa bajeti ya kawaida.

Magari kama Toyota Starlet, EE90, Suzuki Alto, March ya zamani – bado yapo barabarani. Yanaingia bar, yanapita Mlandizi hadi Chalinze, na wamiliki wao hawajutii.

Lengo la uzi huu sio kushindana na matajiri, ni kusaidia wale wanaotamani kuamka asubuhi kwenda kazini bila kuteseka na mvua au foleni.

Kama una uzoefu wowote wa kweli na gari la bei ya chini, endelea kuchangia – maana ndoto kubwa huanza na hatua ndogo. 🚗💪
 
Mkuu Jackpiano umeshawahi fanya kazi kampuni ta Tanzanice.

Nina jamaa angu mmoja anaitwa Jack amewahi fanya kazi kampuni hiyo na anapiga sana Piano - hata kwenye simu nimesave JackPiano.
 
Hapana mkuu, sijawahi fanya kazi Tanzanice lakini jina la JackPiano ninapenda sana miziki ya piano. Labda tukio la huyo jamaa linafanana na mimi kwa bahati tu
 
Don't worry ma men turudi kwenye mada sasa tupate ukweli
Ndiyo, magari ya milioni 2 yapo, hasa yale ya zamani like:

Toyota Starlet

Corolla EE90 / AE100 (kama imechoka)

Suzuki Alto

Daihatsu Mira

Nissan March

Lakini mara nyingi yanahitaji matengenezo ya laki 5–1M ili yawe roadworthy.

Spear zake zipo, lakini lazima uwe na fundi mzuri na bajeti ya matengenezo ya dharura.

Binafsi bado napambana na Mercedes Benz E Class E200 2014.
 
Kwa uzoefu wangu,kununua gari used kwa mtanzania ni zaidi ya kujitoa mhanga.Watanzania wengi sio waaminifu hata kidogo unaweza ukasema uchukue angalau gari ya 10M but badaye unaanza kutumia utakutana na matatizo mpaka ukome.
Pia,kununua gari used kwa 10M bora uendelee kusave uaagize Japan ya 18M.

Gari ya mkononi usinunue zaidi ya 3M,hapo tenga matengenezo yasiyozidi 3M.Ingawa gari za aina hii nyingi utapata ni namba A,B or C na mengi ni yale magari yenye engine kubwa kuanzia CC 2000 au ya ulaya.
Gari kama verossa,mark x,corona,mark II,carina,unaweza pata kwa bei hiyo.
 
🔥 KWELI KUNA MAGARI YANAYOUZWA HADI MILIONI 2? Hebu Tujadili Wadau! 🔧🚗

Wakuu habari zenu,

Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya magari hapa JF na pia Instagram, nikaona baadhi ya magari yanatajwa kuwa yanauzwa kuanzia milioni 1.5 hadi milioni 2. Swali langu ni moja tu:

👉 KWELI kuna magari ya kueleweka, yanayoweza kutembea, kwa bei ya milioni 2 au chini ya hapo? Au hizi ni porojo za matangazo tu?

Kwa mfano nimesikia magari kama:

Toyota Starlet ya zamani
Corolla EE90 au AE100 (ikiwa haipo vizuri)
Suzuki Alto
Daihatsu Mira
Nissan March
Na mengine ya aina hiyo…

Maswali ya kuzingatia:

1. Kwa anayejua magari: Ni magari gani mtu anaweza kupata kwa milioni 2 na bado akaweza kuyategemea kwa matumizi ya kila siku?

2. Je, upatikanaji wa spea ni rahisi kwa magari ya bei hiyo?

3. Gari la milioni 2 linahitaji matengenezo ya kiasi gani ili liwe “roadworthy”?

4. Ni bora kununua gari la bei hiyo au kuongeza hadi milioni 3–4 ili kupata kitu cha kueleweka zaidi?

5. Kwa mtu wa matumizi ya kawaida (labda boda aliyeupgrade au mwalimu), ni ushauri gani ungempa kuhusu magari ya bei hizi?

6. Je, ununue gari dogo la bei rahisi au uanze na bajaji au pikipiki yenye matumizi madogo ya mafuta?

Bonus: Kama una uzoefu

Tafadhali weka picha ya gari lako kama ulilinunua kwa bei ya chini, na utuambie:

Ulilinunua lini?

Kwa bei gani?

Changamoto gani ulizokutana nazo?

Umeridhika nalo?
🎯 Lengo la uzi huu ni kusaidiana. Sio kila mtu ana uwezo wa milioni 10 ya kununua gari, lakini kuna watu wana ndoto ya kuwa na usafiri wao binafsi, hata kama ni gari dogo, la zamani au la kawaida kabisa.

Karibuni wote, hasa mafundi, madalali wa magari, na wamiliki wa magari ya bei nafuu
kwa hapo gari ni corolla tu
 
Kuna mwamba mmoja kaleta chai ya jioni ety mimi binafsi natumia ...........class £200
 
Dunia ina mambo sana, kuna siku tupo mahali mwanamama akaja na gari yake Vitz new model akaiuza pale pale iwa milioni 2.5 na hapo akalipwa milion 1 kwanza ikabaki 1.5 aliyolipwa ndani ya miezi minne kidogo kidogo.

Gari ilikuwa imenyooka haina shida, shida alkuwa nazo yule mwanamama (mikopo na mume hajui 😂)

Alikuja kumuomba jamaa aimuuzie tena ile gari kwa milioni 5 jamaa akagoma anataka 6 wakashindwana.

Kuna gari zakulenga huwa zina bei za ajabu sana.
 
🔥 KWELI KUNA MAGARI YANAYOUZWA HADI MILIONI 2? Hebu Tujadili Wadau! 🔧🚗

Wakuu habari zenu,

Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya magari hapa JF na pia Instagram, nikaona baadhi ya magari yanatajwa kuwa yanauzwa kuanzia milioni 1.5 hadi milioni 2. Swali langu ni moja tu:

👉 KWELI kuna magari ya kueleweka, yanayoweza kutembea, kwa bei ya milioni 2 au chini ya hapo? Au hizi ni porojo za matangazo tu?

Kwa mfano nimesikia magari kama:

Toyota Starlet ya zamani
Corolla EE90 au AE100 (ikiwa haipo vizuri)
Suzuki Alto
Daihatsu Mira
Nissan March
Na mengine ya aina hiyo…

Maswali ya kuzingatia:

1. Kwa anayejua magari: Ni magari gani mtu anaweza kupata kwa milioni 2 na bado akaweza kuyategemea kwa matumizi ya kila siku?

2. Je, upatikanaji wa spea ni rahisi kwa magari ya bei hiyo?

3. Gari la milioni 2 linahitaji matengenezo ya kiasi gani ili liwe “roadworthy”?

4. Ni bora kununua gari la bei hiyo au kuongeza hadi milioni 3–4 ili kupata kitu cha kueleweka zaidi?

5. Kwa mtu wa matumizi ya kawaida (labda boda aliyeupgrade au mwalimu), ni ushauri gani ungempa kuhusu magari ya bei hizi?

6. Je, ununue gari dogo la bei rahisi au uanze na bajaji au pikipiki yenye matumizi madogo ya mafuta?

Bonus: Kama una uzoefu

Tafadhali weka picha ya gari lako kama ulilinunua kwa bei ya chini, na utuambie:

Ulilinunua lini?

Kwa bei gani?

Changamoto gani ulizokutana nazo?

Umeridhika nalo?
🎯 Lengo la uzi huu ni kusaidiana. Sio kila mtu ana uwezo wa milioni 10 ya kununua gari, lakini kuna watu wana ndoto ya kuwa na usafiri wao binafsi, hata kama ni gari dogo, la zamani au la kawaida kabisa.

Karibuni wote, hasa mafundi, madalali wa magari, na wamiliki wa magari ya bei nafuu
Mkuu shuhuda ni mm hapa..nilinunua premio old Kwa 2m..nikaweka 1.4m gari ikatoka mpya kabisa..nikaitest kama ni nzima kutoka Dom to mwanza na kurudi dom..chuma nzima balaa mpaka Leo ninayo safari popote..
 
Back
Top Bottom