Kweli huyu mpenzi wangu ananipenda kwa dhati?

Ikiwa unampenda na yeye kasema anakupenda INATOSHA. Hilo la kuwa pamoja naye litazidisha mapenzi yenu, lakini tafadhali, jaribu kumwamini bila ya kumchunguzachunguza, si katika simu yake, mkoba wake wala emails zake. Kumbuka kuwa "atafutaye hakosi" na wewe kama utaanza kumtafutafuta hutakosa kasoro zake, lakini yoyote utakayoyaona yatatokana zaidi na kutomwamini kwako kuliko ukweli wenyewe. Kumbuka kuwa kutoaminiana na wivu ni adui wa mwanzo wa mapenzi. Kadiri atakavyohisi kuwa unamwamini ndipo atazidi kukupenda kuliko kuanza na mguu mbaya tangu mwanzo kwa wivu na upekuzi wa kipuuzi. Mwachie uhuru wake ili kulinda uhuru wako na nyote lindeni mapenzi yenu.

:tea: Nimeweka kijiko ki 1 cha sukari
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom