Kweli hili ni ajabu lingine: Jamaa kapora Bunduki kwa kutumia Panga

cdc

JF-Expert Member
Nov 29, 2015
445
419
MKAZI wa Kijiji cha Bisarwi, kata ya Manga, tarafa ya Inano, wilayani Tarime, mkoani Mara, Mwita Nyagosaima (31) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Tarime akidaiwa kuvamia usiku nyumbani kwa Magesa Alphonce na kupora bunduki na Sh milioni 5.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa akiwa na panga, baada ya kuvamia nyumbani kwa Alphonce alimtishia kumkata mlalamikaji baada ya kumdhibiti asiweze kutumia silaha yake kujihami na kumpora bunduki aina ya shot gun na Sh 5,000,000 na kutokomea gizani.

Akisomewa mashitaka hayo jana, mbele ya hakimu wa mahakama ya hiyo Amon Kahimba mwendesha mashitaka wa Polisi, Alois Nguluo alidai alidai kuwa mtuhumiwa Nyagosaima Aprili 3 mwaka huu usiku katika kijiji cha Bisarwi alivamia nyumbani kwa Magesa Alphonce akiwa na panga kwa nia ya kutenda kosa hilo.

Alidai kabla Magesa hajajipanga kupambana na mtuhumiwa alitishiwa kukatwa panga na mtuhumiwa na kisha kumpora bunduki yake aliyokuwa akimiliki kihalali yenye namba CAR 641 / 34160 ya thamani ya Sh 850,000.

Mshitakiwa Nyagosaima alikana shitaka lake na upande wa mashitaka ulidai upelelezi bado haujakamilika na hakimu kuamuru kesi hiyo kutajwa tena Mei 2, 2017 na mshitakiwa kwenda rumande hadi tarehe hiyo ya kutajwa.
Source: gazeti la habari

Najiuliza tu jamaa alijiamini kwa kiasi gani kufanya hili tukio. Sithani kama alipiga mahesabu kama kibao kingegeuka nn kingetokea
 
Ukisha Wekwa ktk Kanyambasiro mbona unatulia tu
Jiulize kwa nini wanajeshi wana jipiga na Matofali
wakati hutumia Chamoto kwenye mapambano!!
Kuna wakati Bunduki haiwezi Faa kila mazingira ya tukio
 
wakurya ni majasiri sana......tatizo mara nyingi hutumia ujasiri huo mahali pasipo sahihi.MURAAA
 
  • Thanks
Reactions: cdc

uwezeokno upo inategemea mazingila
 
Nakumbuka kuna habari ipo humu ndani Wale askari wa tigo waliporwa bunduki kwa kisu na kipigo juu.

Unaambiwa bora upigwe 'binduki' kuliko Panga.
 
Ukisha Wekwa ktk Kanyambasiro mbona unatulia tu
Jiulize kwa nini wanajeshi wana jipiga na Matofali
wakati hutumia Chamoto kwenye mapambano!!
Kuna wakati Bunduki haiwezi Faa kila mazingira ya tukio
Itakuwa poa sana ikikupata hiyo

Ova
 
Yule mama aliwapa kichapo majambazi, na akawanyang'anya bunduki.....
Huyo jamaa itakua hakupitia jando....
 
Back
Top Bottom