Kweli Dunia Ndogo....

Kweli Dunia Ndogo....

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
60,418
Reaction score
139,275
2010:London, UK
Ilikuwa jumamosi fulani hivi amazing summer, niliamua kumtembeza rafiki yangu ambae alikuwa mgeni mjini. Ikabidi tufanye mambo ya double date.
Mimi nilikuwa na gf yeye hana kwahio nilimwambia gf ajiandae na rafiki yake nawatoa out, tunaenda movie then clubbing akasema sawa.
Saa mbili mbili tukawapitia kwahio tukawa pair mbili moja kwa moja showcase cinemas. Tukacheki movie tulivotoka movie tukaingia bar/club Brannigans. Tukajirusha humo mpaka saa nane taa zikawashwa tukatoka.
Rafiki yangu na date wake waliconnect immediately basi tulivyotoka pale mimi moja kwa moja nikadrive mpaka geto kwangu nikashuka na gf wangu nikamkabidhi jamaa gari nikamwambia utaniletea asubuhi endeleeni kula bata. Kesho yake mpaka saa sita mchana kimya,nikampigia jamaa akaniambia kalala kwa demu,jana hio hio alimaliza kila kitu. Hawa watu waliendelea ku-date mpaka nilipopotezana nao kwasababu za kimaisha.

2015😀ar JMT
Rafiki yangu,kaka yangu,yaani kama ndugu kaja Dar from USA kuja kuoa. Jumapili moja kanialika rasmi nimjue bibi harusi, aliniita Slipway for dinner. Basi nikajizoazoa nikaenda, nilipomuona bibi harusi nikahisi namjua mpaka jamaa akashtuka vipi mnajuana nikapotezea wala hatujuani, ila nilikuwa sijui huyu dada nimemuona wapi. Tukala tukaongea sana tukaagana, mimi kichwani najaribu ku recall huyu bibie nimemuona wapi,mara paap nikakumbuka ndio huyu tulieenda nae double date akawa demu wa rafiki yangu mwengine.
Nikampigia simu yule ex e bhana nimekutana na fulani anaolewa, jamaa likaniambia aah najua. Nikamuuliza umejuaje akasema bado napiga hata kesho nikitaka napiga! Nikamwambia sikiliza, wewe ni rafiki yangu sana, na anaemuoa ni rafiki yangu mkubwa naomba acha huo ujinga, wewe umeoa ungejisikiaje mkeo akifanyiwa hivyo? Jamaa akasema eti nilishapanga akiolewa naachana nae! Mwezi uliofuata ndoa ikafungwa.
Sikuwahi kumwambia yule dada(nahisi yeye alinikumbuka siku ile ile) wala kumwambia huyu rafiki yangu kama nilikuwa namfahamu mkewe kabla, hivi tunavyoongea wana mtoto wa mwaka na nusu I guess. Kweli dunia ndogo!
 
ukitaka kujua dunia ni ndogo zaidi jamaa aje agundue hana uwezo wa kuzalisha na wakati huo ana watoto wawili... utaona dunia kisoda....!!!
haaaaaha daahh hapo patakuwa hapatoshi tena udogo wadunia utaongeza na kuwa namuonekano kama wa kidonge cha panadol
 
Mimi nilikuwa nagonga Demu wakati nipo Chuo huyu Demu alikiwa kanizidi Mwaka Mmoja, sasa kuna Baba yangu mdogo ambaye kiumri si wa makamo siku moja alinipigia simu niende kwake nikapafahamu ile kufika akanambia Kijana leo umefika lakini Mama yako katoka sasa usiondoke hadi arudi nikamwambia poaa, Mara paap, getini nasikia oni ya gari..housgirl akaambiwa nenda kafungue mlango Mama karudi, hapo sie tumekaa sebuleni nikiwa na hamu ya kumfahamu Mama Mdogo..Dah..si akaingia Demu ambaye nilishagonga Longtime wakati nipo chuo! Dunia kweli ni ndogo sanaa...
 
Sasa ilikuwaje? Ulimuamkia mama yako mdogo au?
 
manina duuhh .eenheee hamkuendelea kupasha kiporo lbaada ya kukutana tena ..?
 
Back
Top Bottom