Kweli CRDB ni majanga

Kweli CRDB ni majanga

bigmash

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
416
Reaction score
422
Jamani, kulikuwa na mada humu zikilalamikia makato yanayofanywa na CRDB bank, mpaka wengine kutishia kuhama bank hiyo na kutafuta huduma kwenye mabenki mengine. Kwa kweli leo nimepata fresh na kesho itabidi niende kwenye tawi lao nionane na manager nipate ufafanuzi juu ya hili.

Nisiwachoshe, ilikuwa hivi, niliingiziwa shilling million sita na mteja wangu na niliangalia salio nikakuta kweli zimeingizwa, baada ya muda Kama masaa mawili nilicheki tena salio baada ya kuona Kuna mtu humu amelalamika kuhusu makato, nilivyoangalia salio tena nikakuta zimefyekwa Tshs 25000/, salio lilisoma 5,975,000/ nikaona isiwe tabu labda wamekata makato yao ya mwezi kugharamia hiyo account.

Cha ajabu mpaka nimeaamua kuandika mada hii tena ni kwamba leo jumapili nimeamua kwenda kutoa pesa kiasi cha 5,900,000/, kwa ajili ya shughuli zangu hivyo nikajua zitabaki 75,000/ lakini baada kutoa na kucheki salio nikakuta zimebaki 29,000/ tu hivyo wamefyeka tena sh. 46,000/ hivyo jumla ya makato niliyokatwa kwa sh. 6,000,000/ nilizoingiziwa na mteja wangu ni sh. 71,000/ , inawezekana vipi hii?

Maana sijawahi kuona makato makubwa namna hii, nadhani kuna kitu kinaendelea ndani ya hii bank bila sisi wateja kujulishwa, hatua itabidi zichukuliwe.
 
Kwasababu wamesema wamekomesha ujambazi, next time waambie wateja wakulipe kwa cash kwenye sandarusi, ukaziweke home tu, hamna namna.
 
Duh mkuu pole sana! Mimi nikipokeaga tu pesa kama ni usiku kwenye hizi bank kubwa mbili huwa nalala bila amani, asubuhi kukicha tu naenda kuhamishia kuna bank hawana makato kabisa hata 100.
 
Duh mkuu pole sana! Mimi nikipokeaga tu pesa kama ni usiku kwenye hizi bank kubwa mbili huwa nalala bila amani, asubuhi kukicha tu naenda kuhamishia kuna bank hawana makato kabisa hata 100.
Bank gani hiyo mkuu nijulishe.
 
Hata mm naona kuna makato yasiyo na maelezo crdb ,shv ntakuwa na diary ya kuandika pesa zilizobak benk ilii nijue kinachoendelea
 
Mkuu mimi niliweka laki saba tu ikapita mwezi nikasema ngoja niongeze laki nilivyofika kucheki balance nikakuta wamekata 16000 ikabidi niwatumie sms kwenye kila mtandao waliopo wakanijibu wamekata makato ya account kwa mwaka.

Nikaona isiwe shida nikaachana nao nimekaa muda kidogo tena nikaenda kucheki balance nikakuta wamekata tena 13000 nilichofanya nilienda nikatoa pesa yangu yote nimetunza m pawa paka muda huu natafuta bank yenye unafuu siyo CRDB nikikosa pesa yangu itulie huko huko M Pawa.
 
Kwa hapa mjini EQUITY BANK hawana makato hata kuangalia salio ni bure anatumia mke wangu, ila mimi natumia BANCABC makato ni kuangalia salio TU! Sema shida hawana branch nyingi kama hao majambazi.
BANKABC makato yao ni 0 kwa kila kitu even mwisho wa mwezi!
 
Jamani, kulikuwa na mada humu zikilalamikia makato yanayofanywa na CRDB bank, mpaka wengine kutishia kuhama bank hiyo na kutafuta huduma kwenye mabenki mengine. Kwa kweli leo nimepata fresh na kesho itabidi niende kwenye tawi lao nionane na manager nipate ufafanuzi juu ya hili...
Komba hiyo ilobaki.nenda equity na kitambulisho cha nida na copy yake moja.

Massa machache tayari una account.

Na baada ya siku kumi kadi unapewa.
 
Mimi natumia CRDB kwa muda na sijaona mengi ya yaliyosemwa na wadau hapo juu. Nashauri kwenda Bank iliyo karibu na uongee na Branch Manager au wahudumu.

Ahsante
 
Back
Top Bottom