Kweli CCM Tunachukiwa!

Kweli CCM Tunachukiwa!

Laiser Tom

Member
Joined
Jan 12, 2014
Posts
36
Reaction score
20
Nimeshuhudia majuzi nikisafiri kutoka Moro kwenda Arusha ambapo katika Bus la abiria 60 palikuwa na mjadala mkali sana na wachangiaji wakiongea kwa hisia kali.

Kati ya abiria takriban 25 waliokuwa wakichangia/kujadiliana ni watu wawili tu walioonyesha kuipenda CCM. Waliobaki walikuwa wankiponda chama chetu vibaya sana. Nilijaribu kufurukuta kwa kueleza mazuri ya CCM lakini nilizomewa hadi nikajinyamazia.

Najiuliza ni nini CCM imewakosea Watanzania hata kuchukiwa ghafla hivi?! Inafikia hatua mtu unaona aibu kujitambulishia CCM. Kijana mmoja (abiria) alisema mtu akimfananishia CCM atamshitaki kwa kosa la kumkashifu (yaani akimhusisha na CCM).

Wanachama wenzangu nasi tuamke tukitee chama chetu.
 
Laiser Tom

Wanachama wenzangu nasi tuamke tukitee chama chetu.
unakiteteaje chama bom kama hicho wakati sasa hivi ndio kiko kwenye UBORA WAKE kwa r
ushwa,kulindana na kila aina ya ufisadi???
 
Last edited by a moderator:
si ulikuwa na wamasai, ulitegemea wakuchekee ilhali olaiboni kakatwa.
 
Mtoa mada mmasai,hii post umeiweka kimtego au kiuzushi.
 
Yani wazee wanakichukia chama chako wewe bado umeshikilia pembe lol!
njoo palipo na furaha ukawa
 
Yaani ningekuwepo kwenye hilo basi hakika msingesafiri kabisaaa
 
basi linaloenda arusha obviously weng ni wapenz wa chagadema na lowasa, unategemea wasifie ccm?
 
Back
Top Bottom