Kweli CCM hawakujua uovu uliokuwa unafanywa na serikali ya awamu ya nne?

VIVIANET

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
2,129
2,918
NDUGU ZANGU MM NI MTANZANIA AMBAYE NIMEKUWA NA UCHUNGU SANA NA NCHI YANGU
SIJAFANIKIWA KUWEPO KWENYE UCHAGUZI KUTOKANA NA MAJUKUMU YA MASOMO HAPA COLUMBUS OHIO.

NIMEONA NILETE MADA HII KWENU NDUGU ZANGU KUTAKA KUJUWA KAMA KWELI VIONGOZI WA CCM PAMOJA NA WABUNGE WAKE HAWAKUJUWA UBADIRIFU ULIOKUWA UNAFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA 4?

MAANA SIKU ZOTE WAPINZANI NA WATU WENGINE WALIPOJARIBU KUWEKA WAZI MADUDU YALIYOKUWA YANAFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU 4 WALIONEKANA HAWAFAI NA NIWAONGO NA WAZUSHI KABISA.

JE, HAYA YANACHOTOKEA LEO CCM WANATAKA KUTUAMBIA HAWAKUYAJUWA? NA KAMA WALIJUWA KWANINI LEO WANATAKA KUONYESHA KWAMBA WAMEKUWA WATETEZI WA WATANZANIA WAKATI HAYA YOTE YAMESABABISHWA NA ILE SERIKALI WALIOKUWA WANAISIFIA SANA?
 
Last edited by a moderator:
Baadhi ya viongozi wa serikali ya awamu ya NNE pamoja na madudu yao wameaminiwa na upinzani......

CDM imekuwa sawa na CCM
 
Baadhi ya viongozi wa serikali ya awamu ya NNE pamoja na madudu yao wameaminiwa na upinzani......

CDM imekuwa sawa na CCM
Kaka yangu hujanisaidia kujibu swali langu....Can you read again the heading?
 
NDUGU ZANGU MM NI MTANZANIA AMBAYE NIMEKUWA NA UCHUNGU SANA NA NCHI YANGU
SIJAFANIKIWA KUWEPO KWENYE UCHAGUZI KUTOKANA NA MAJUKUMU YA MASOMO HAPA COLUMBUS OHIO..NIMEONA NILETE MADA HII KWENU NDUGU ZANGU KUTAKA KUJUWA KAMA KWELI VIONGOZI WA CCM PAMOJA NA WABUNGE WAKE HAWAKUJUWA UBADIRIFU ULIOKUWA UNAFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU YA 4? MAANA SIKU ZOTE WAPINZANI NA WATU WENGINE WALIPOJARIBU KUWEKA WAZI MADUDU YALIYOKUWA YANAFANYWA NA SERIKALI YA AWAMU 4 WALIONEKANA HAWAFAI NA NIWAONGO NA WAZUSHI KABISA. JE HAYA YANACHOTOKEA LEO CCM WANATAKA KUTUAMBIA HAWAKUYAJUWA? NA KAMA WALIJUWA KWANINI LEO WANATAKA KUONYESHA KWAMBA WAMEKUWA WATETEZI WA WATANZANIA WAKATI HAYA YOTE YAMESABABISHWA NA ILE SERIKALI WALIOKUWA WANAISIFIA SANA?
ccm ni ile ile milele...
 
Bunch of nonsense!
 
from your angle of view, this is VERY PARADOXICAL kweli! One must like have a confession of faith, to belive the facts. Nachoweza kujibu ni kwamba, zipo mbinu zilizominya uhuru wa kuyaweka madudu haya wazi au it was the order of the day. Ni dhahiri, kinachoonekana sasa, ni kwamba, wengi tulijua lakini hatukua na pakusemea. Imechukua REGIME CHANGE ili tupate pakusemea. Ni wakati wako sasa, ikiwa unajua ukweli wowote wa jambo fulani, liweke wazi, litashughulikiwa. Yaliyopita sasa yametufundisha la kufanya. Kwa sasa hatutaki ku dwell kwenye yaliyopita, bali tu concentrate katika kujenga Taifa la sasa!! Asante
 
Sithani CCM au watanzania walijua kuna majipu sugu na makubwa kiasi hiki. Kwa watanzania ilikuwa part of life na hawakuona ni kosa kutoa au kupokea rushwa, kuiba, kutokuwajibia. Watanzania walio jua ukweli walipigwa na kutosikilizwa.
 
from your angle of view, this is VERY PARADOXICAL kweli! One must like have a confession of faith, to belive the facts. Nachoweza kujibu ni kwamba, zipo mbinu zilizominya uhuru wa kuyaweka madudu haya wazi au it was the order of the day. Ni dhahiri, kinachoonekana sasa, ni kwamba, wengi tulijua lakini hatukua na pakusemea. Imechukua REGIME CHANGE ili tupate pakusemea. Ni wakati wako sasa, ikiwa unajua ukweli wowote wa jambo fulani, liweke wazi, litashughulikiwa. Yaliyopita sasa yametufundisha la kufanya. Kwa sasa hatutaki ku dwell kwenye yaliyopita, bali tu concentrate katika kujenga Taifa la sasa!! Asante
well said. let's concentrate on building. we corect what has been done wrong to build a new Tanzania
 
Ni ukweli usio pingika kuwa madudu yote yalikuwa yanajulikana ila, nani wa kukemea ili hali wakubwa wote walikuwa wanajua, mfano kontena zote hizo zitapoteaje bila usalama, polisi na idara zote kutokujua. Zilikuwa ni dili za watu hizi
Mungu atusaidie sana
 
Hata haya yanayoibuliwa bado na madogo sana, kuna madudu ya mgodi wa kiwira, kuna madudu ya kuuza nyumba za serikali utafikiri wanauza nyumba za urithi, kuna madudu ya ESCROW, MEREMETA,RICHMOND pengine na mengi zaidi ila hayatakaa kuguswa maana kuyagusa ni kuigusa mizizi ya CCM, so ndugu huko ulipo ukae ukijua kuwa ccm ni ile ile daima........mengine utayasikia siku upinzani wakichukua Nchi.
 
kama ulikuwa hujui fahamu kuwa ndani ya ccm kuna makundi. kundi ovu lililoshika hatamu za uongozi ndilo lililozaa serikali legelege ambayo uozo wake tunaushuhudia.
bahati nzuri sasa kundi adilifu ndilo limeshika hatamu za uongozi ndani ya ccm. imezaliwa serikali yenye dhamira ya kweli ya kuwatumikia watz.
viongozi wa ccm na wabunge walifahamu uozo wa serikali ya awamu ya nne lakini fahamu neno hili- kushika hatamu. hata uwe mzalendo kiasi gani, ni vigumu kubadili mambo kwa sababu kundi ovu lilijenga MFUMO ambao haikuwa rahisi kuuvunja. viongozi wa MFUMO wameondoka na MFUMO umesambaratika. tuna ccm mpya ndani ya ccm ile ile. ccm mbele mbele.
 
Kwa vyovyote vile sitotoa siri za baraza la mawaziri.....hiyo kauli ina maana kubwa sana, ni kiapo ambacho kila waziri anatakiwa kukitamka hadharani. Wanaoyasema maneno hayo wanatofautiana katika mambo mengi sana, kuna wale wenye urafiki na wafanyabiashara wachafu kuna wale ambao wanatanguliza shida za wananchi kabla ya wao kuanza kuufikiria utajiri binafsi... wote hao wanaapa na kuahidi kutotoa siri za kazi. Upo uwezekano rais wa awamu ya tano alikuwa akiumia moyoni kwa sababu ya kulazimika kuyakubali mambo mengi yaliyooza kwa sababu tu ya ule utii wa ufanyaji kazi ndani ya kiapo cha usiri. Kila zama na kitabu chake lakini hulka za watu haswa viongozi huwa hazibadiliki, mawaziri wanajikuta wakilazimika kuishi kinafiki ili mkate wa kila siku uweze kupatikana. Usishangae waziri mkuu alikwenda bandarini na kuwaonyesha maafisa wa TRA na TPA orodha ya makontena na magari yaliyobeba mizigo ambayo haikulipiwa kodi, data zipo lakini kuna ule usiri wa sitotoa siri za baraza la mawaziri. Yote hayo kwa ujumla wake ndio yanayozitofautisha awamu mbalimbali za uongozi wa CCM.
 
Ni Kama Maajabu Kwa Ndani Kuona Hao Hao Ccm Wakija Na Kusema Yule Mbaya
Ila Kuna Majibu Ambayo Kwasasa Tungesema Serikali Ili Iwe Ya Uwazi Na Uwajibikaji Kwa Watu Wote Bila Kujari Cheo:-

1 . Uongozi Wa Awamu Iliyopita Upo Uwe Na Sababu Kusaidia Kupata Ukweli Juu Ya Haya Ya Sasa

2 . Taarifa Ya Bandari Iwekwe Wazi Kwa Yale Majina Yaliyopelekwa Kwa PM Ambayo Inasemekana Ndiyo Ya Waandika Vimemo

3.Yatajwe Majina Ya Viongozi Waliokuwa Wanatoa Vimemo Kwenda Bandari Kutoa Mizigo

4.Watajwe Viongozi Na Makada Wa Ccm Wakitumia Mwamvuli Wa Kutisha Vyombo Kama TISS, PCCB
 
Mkuu
Philip Bukililo
Naungana Nawe Hayo Maneno Ndiyo Yanatumaliza
Nitamshauri Rais Kwa Busara, Hekma Na Wakati Wangu Wote Sitatoa Siri Za

Rais
Bunge
Baraza La Mawaziri
TISS
PCCB
POLISI
MAGEREZA
UHAMIAJI
JESHI
 
Baadhi ya viongozi wa serikali ya awamu ya NNE pamoja na madudu yao wameaminiwa na upinzani......

CDM imekuwa sawa na CCM
Kwahiyo hata ndio majibu ya hoja iliyowekwa? Sasa nimeamini kuwa watu walikuwa wanakusingizia kuwa no zzk, ZZK pamoja na yote hawezi kuwa this much low hata kidogo. Wewe ni wewe tuu na umbulula wako. Maana hata kama ni utetezi kwa ccm hauwezi kuwa wa kijinga namna hii
 
Back
Top Bottom