kiss daniel
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 980
- 2,469
Ubalikiwe sana uwe unadondosha mara nyingi ukipata mdaMlango 58
Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.
2 Walakini wanitafuta kila siku; hupenda kujua njia zangu; kama vile taifa waliotenda haki, wasioacha sheria ya Mungu wao, hutaka kwangu amri za haki; hufurahi kumkaribia Mungu.
3 Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
Kamtuma mtume gani?Yesu alifunga siku 40 usiku na mchana! Nyie hilo andiko linalowaruhusu kula usiku mmelitoa wapi?!
Sisi waislamu ibada zetu zinaendana na maandiko!
Kwahiyo ukisema KULA DAKU NI KUBADILI RATIBA YA KULA !
Ukiona ni hivyo basi ujue huko kubadili ratiba ya kula ni ibada na inampendeza Mungu kwa kuwa katuma mtume aje awafundishe watu kuwa katika mambo ambayo yanampendeza Mungu ni kubadili ratiba ya kula ( kulingana na mtazamo wenu ) katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwahiyo sisi hatujali watu wajinga wanatuchukuliaje bali tunachojali ni kufuata maelekezo ya Mungu na mtume wake!
SASA NYINYI ANDIKO LA KULA USIKU MMETOA WAPI WAKATI YESU ALIFUNGA USIKU NA MCHANA KWA SIKU 40 ?!
Muhammad صلى الله عليه وسلمKamtuma mtume gani?
Niletee andiko kutoka hata kwenye gazeti ambalo linaonesha MUNGU akimpa Muhammad utumeMuhammad صلى الله عليه وسلم
Umeanza ujinga wako dogoKwaresma hii wewe umepumzika kula nini? Mi nimepumzika kula makande wewe je?
Endelea kujitoa akiliKufunga maana yake nini?! Na mtu anafungaje?!
Maana kuna kufunga milango, kufunga madirisha, kufunga tai, kufunga kamba za viatu, kufunga ndoa nk. Sasa nyinyi wakati wa kwaresma mnafunga nini?!
Quran suratu Alfat hu Aya ya 29.Niletee andiko kutoka hata kwenye gazeti ambalo linaonesha MUNGU akimpa Muhammad utume
Nazani anataka Aya ambayo MUNGU anatamka kwa kinywa chake mwenyeweQuran suratu Alfat hu Aya ya 29.
{ مُّحَمَّدٞ رَّسُولُ ٱللَّهِۚ وَٱلَّذِينَ مَعَهُۥٓ أَشِدَّآءُ عَلَى ٱلۡكُفَّارِ
رُحَمَآءُ بَيۡنَهُمۡۖ تَرَىٰهُمۡ رُكَّعٗا سُجَّدٗا يَبۡتَغُونَ فَضۡلٗا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضۡوَٰنٗاۖ سِيمَاهُمۡ فِي وُجُوهِهِم مِّنۡ أَثَرِ ٱلسُّجُودِۚ ذَٰلِكَ مَثَلُهُمۡ فِي ٱلتَّوۡرَىٰةِۚ وَمَثَلُهُمۡ فِي ٱلۡإِنجِيلِ كَزَرۡعٍ أَخۡرَجَ شَطۡـَٔهُۥ فَـَٔازَرَهُۥ فَٱسۡتَغۡلَظَ فَٱسۡتَوَىٰ عَلَىٰ سُوقِهِۦ يُعۡجِبُ ٱلزُّرَّاعَ لِيَغِيظَ بِهِمُ ٱلۡكُفَّارَۗ وَعَدَ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَعَمِلُواْ ٱلصَّٰلِحَٰتِ مِنۡهُم مَّغۡفِرَةٗ وَأَجۡرًا عَظِيمَۢا }
Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wakiinama na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. Alama zao zi katika nyuso zao, kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Taurati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea ulio toa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu, ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, ukawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walio amini na wakatenda mema katika wao msamaha na ujira mkubwa".
Suuratul Alfat hu Aya ya
8
"
{ إِنَّآ أَرۡسَلۡنَٰكَ شَٰهِدٗا وَمُبَشِّرٗا وَنَذِيرٗا }
Hakika tumekutuma wewe (Muhammad ) uwe Shahidi, na Mbashiri, na Mwonyaji",
Hii inatosha.Nazani anataka Aya ambayo MUNGU anatamka kwa kinywa chake mwenyewe
Kuwa Mimi yeye MUNGU nimekufanya Muhammad uwe mtume wangu
Kama ipo wewe mpe tu kisha achana naye
Ni wapi Allah kasema ndo andiko linalohitajika hapaHii inatosha.
Kama Allaah mwenyewe kasema "Muhammad ni mtume wa Allaah" maana yake ni kwamba yeye ndiye kamtuma na kumtuma kwa lugha ya Quran ndiko kumpa utume.
Quran , Taurati, Zaburi na Injili yote ni maneno ya Allaah aliyoyateremsha kwa mitume wake Muhammad, Musa , Daudi na Issa kwa nyakati tafauti na maeneo tafauti na siyo maneno ya wazee wa kiarabu kama unavyoandika.Ni wapi Allah kasema ndo andiko linalohitajika hapa
Yeye hahitaji andiko ambalo wanazungumza wazee wa kiarabu anataka andiko ambalo Allah yeye mwenyewe anazungmza
Lilete hapa
Mussa ni nabii mandiko yapo yanathibitisha hilo(kumbukumbu la torati 18:15-18)Quran , Taurati, Zaburi na Injili yote ni maneno ya Allaah aliyoyateremsha kwa mitume wake Muhammad, Musa , Daudi na Issa kwa nyakati tafauti na maeneo tafauti na siyo maneno ya wazee wa kiarabu kama unavyoandika.
Kusema Quran ni maneno ya wazee wa kiarabu ni hoja ya kipumbavu nami sipo tayari kuendelea kuwaelewesha wapumbavu ambao hawana nia ya kuelewa haki iko wapi!
Hao mitume wako unawatoa wapi wewe? Huyo DAUDI ni mtume kuanzia liniQuran , Taurati, Zaburi na Injili yote ni maneno ya Allaah aliyoyateremsha kwa mitume wake Muhammad, Musa , Daudi na Issa kwa nyakati tafauti na maeneo tafauti na siyo maneno ya wazee wa kiarabu kama unavyoandika.
Kusema Quran ni maneno ya wazee wa kiarabu ni hoja ya kipumbavu nami sipo tayari kuendelea kuwaelewesha wapumbavu ambao hawana nia ya kuelewa haki iko wapi!
Kulingana na mafundisho ya Quran ni kwamba Daudi na mwanae Suleymani walikuwa manabii , mitume na pia walikuwa wafalme.Hao mitume wako unawatoa wapi wewe? Huyo DAUDI ni mtume kuanzia lini
Daudi alikuwa MFALME WA Israel kama nyetanyahu leo hii alivyo waziri mkuu wa Israel (1 samweli 16) hapo MWENYEZI MUNGU anamwinua nabii wake samweli anamwambia nenda katika familia ya yesse nimejipatia MFALME katika familia hiyo ambaye atamrithi MFALME shauri, MFALME huyo ndo daud
Sasa kuanzia lini daud tena Kawa nabii?
Ndo maana nimekwambia wewe unaishi kwenye maneno ya waarabu, wewe huishi kwenye maneno ya MWENYEZI MUNGU AllahKulingana na mafundisho ya Quran ni kwamba Daudi na mwanae Suleymani walikuwa manabii , mitume na pia walikuwa wafalme.
Narudia Daudi na mwanae Suleymani walikuwa manabii , mitume , na wafalme na Allaah alimpa Nabii Daudi kitabu kinachoitwa Zaburi.
Usimlinganishe Nabii , Mtume na mfalme Daudi na nguruwe wa kiyahudi kama Nyetanyau sijui nani vile.
Mimi pia nikitaka naweza sema hiyo kumbukumbu la torati ni maneno ya wazee wa kifarisayo au wazee wa kiyahudi ili twende sawa au vipi?! Wewe una uwezo gani wa kuthibitisha kuwa biblia ,agano la kale na agano jipya siyo maneno ambayo watu walikaa na kutunga na kudanganya kuwa ni maneno ya Mungu, wewe ulikuwepo wakati biblia inaandikwa au unamjua nani aliandika biblia?! Unaanzaje kuamini kuwa kumbukumbu la torati ni maneno ya Mungu wakati hata humjui alieliandika?! Je unajua kuwa Kuna tafauti ya torati aliyopewa Musa na kumbukumbu la torati lililoandikwa na mafarisayo?!Mussa ni nabii mandiko yapo yanathibitisha hilo(kumbukumbu la torati 18:15-18)
Tunaomba mandiko ambayo Allah anatamka kwa kinywa chake kwamba Muhammad ni mtume wake
Mbona huleti unatuletea mandiko ambayo wazee wa kiarabu wanazungumza wenyewe au hao wazee wa kiarabu ndo akina Allah hao
Usikimbie njoo na mandiko
Lakin kaa ukijua YESU KRISTO anakupenda sana
Wewe ni mpumbavu sugu na sioni faida ya kujadiliana na mtu kama wewe!Ndo maana nimekwambia wewe unaishi kwenye maneno ya waarabu, wewe huishi kwenye maneno ya MWENYEZI MUNGU Allah
Siku zote Allah huzunguma mwenyewe pasipo kulishwa maneno na mtu, sasa wewe waarabu wamekuzid akili
Nioneshe katika Quran MWENYEZI MUNGU akimpa daudi unabii, nioneshe kwenye Quran MWENYEZI MUNGU akimpa utume Muhammad
Acha kuishi kwenye maneno ya waarabu ishi katika NENO LA MUNGU
Sasa sisi katika biblia takatifu tumezuiwa kutukana watuWewe ni mpumbavu sugu na sioni faida ya kujadiliana na mtu kama wewe!
Ikiwa unaendelea kusema Quran ni maneno ya waarabu sina uwezo wa kukusaidia zaidi ya kumuachia Allaah akuongoze ikiwa ataona kuwa wewe ni katika watu wanaofaa kuongozwa au akuachie katika upotevu kama alivyomuacha ibilisi katika upotevu.