Kwanini????

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
Nimekuwa nikijiuliza bila kupata jawabu sahihi. Nikaona leo labda niwaulize wa JF pengine mnaweza kunipa jawabu la hiki ninacho jiuliza.
Nchi hii ilipata uhuru wake miaka 50 iliyopita, na kwasababu hiyo tumekuwa na baadhi ya mikoa na wilaya zilizoundwa kwa muda mrefu zaidi ya miaka 30. Lakini kuna kitu kimoja ambacho hata sasa watu wengi hawajaweza kukitofautisha, na mara nyingi hujichanganya pale wanapoelezea maeneo hayo.
Kwanini baadhi ya makao makuu/miji mikuu ya mkoa hujulikana zaidi kuliko mikoa yenyewe?

Matharani Songea ufahamika zaidi kuliko mkoa wa Ruvuma, Musoma hufahaika zaidi kuliko mkoa wa Mara, Bukoba hufahamika zaidi kuliko mkoa wa Kagera, Moshi hufahamika zaidi kuliko mkoa wa Kilimanjaro.
Kufahamika ninakokuzungumzia mimi ni kuwa ni rahisi mtu kuzungumzia majina ya hiyo miji hata kama alikuwa antoa maelezo yanayojumuisha mkoa mzima.

Mfano, utamuuliza mtu, wewe ni mwenyeji wa wapi? Wengi watakwambia Moshi, hata kama wanatokea Marangu au Machame au Rombo lakini wao wanamahanisha mkoa ambao ni Kilimanjaro. The same kwa sehemu hizo zingine nilizotaja.

Je nini kimechangia hali hiyo ya makao/miji mikuu ya mikoa kubeba dhana ya mikoa hata majina ya mikoa kutopewa kipaumbele.
Je hii imetokana na majina ya miji hiyo kutofautiana na majina ya mikoa?
Miji mikuu ya mikoa mingine ina majina sawa na mikoa hiyo, mfano Arusha, Mwanza, Mbeya, Shinyanga ......

Kwanini baadhi ya makao makuu/miji mikuu ya mkoa hujulikana zaidi kuliko mikoa yenyewe?
 
Hata mi najiuliza sipati jibu, inakuwaje mtu anaenda wilaya ya marangu au rombo anasema anaenda moshi ingali moshi ni wilaya inajitegemea?
 
Back
Top Bottom