Kwanini Zitto nisikuite msaliti?

Niliposikia haya maneno yake niliyapenda sana ''Nitakuwa wa mwisho kuondoka chadema maisha yangu yote ya siasa nimekulia CHADEMA, CHADEMA ina muda wangu na damu yangu'' kwa maneno hayo mazito inakuwaje leo hii ufanye us aliti ubaki salama ?

Mimi nimeanza kuvutiwa na Zitto,naona matumaini mapya kwa Tanzania. MUNGU mbariki ZZK
 
ukiwa ndani ya chadema unakuwa huwezi kufikiria zaidi kwa sababu upo pale kuwafurahisha wafalme wa chama vijana walikuwa na mawazo mazuri wamefukuzwa kama wasaliti bila kujua usaliti wao mnawakumbuka mwampamba na shonza,,,, toka sikuile niliachana na chadema nashukuru sasa tumaini letu lipo ACT nyumbanin kwa fikra huru karibuni naamini sikumoja mkikuwa mtataka kujua ukweli wa chadema na ndipo mtafukuzwa exploit beyond the limit of mbowe na dr slaa
 
Zitto anatumika na CCM,si hapa hapa jamii forum kuna mtu alipost haya......lengo lao ni ujina tu..eti kuwagawa wana ukawa au wale watakao waumga mkono
 
Mkuu,tuwekane sawa
Mambo mengine ni common sense hayahitaji akili kubwa kuyapambanu
Nitakupa mfano huu:
Mwalimu Nyerere alipata kusema "Bila ya CCM imara nchi itayumba",Cha ajabu wana CCM wengi hupenda sana kurudia haya maneno lakini katika mtizamo ambao una maana tofauti na aliyolenga Mwalimu.Wao CCM wanachukulia as if Mwalimu alisema "Bila ya CCM nchi hii itayumba" kitu ambacho ni Very Wrong,Lakini kwa mwenye akili ataelewa na atawapuuzia koz haiingii akilini kwamba kama sio CCM basi nchi hii itayumba,hiyo ni kwa akili ya kawaida tu.
Tunakuja Kwako:
1.YES uko sahihi ZZK aliongea maneno uliyoyanukuu,Lakini ni Dhahiri kabisa aliongea maneno hayo kwa kuamini kuwa If the System in Chadema works properly.Lakini kwa bahati mbaya ni Kinyume,sina haja ya kuelezea kwa nini system haiko sawa koz kila mtu anajua,Pale Zitto alipoamua kuwa Brave enough to challenge the TOP ili system iweze ku-work properly ndio yakaibuka maneno ambayo Wenye chama wakaamua kuwaaminisha na baadhi ya wanachama e.g Msaliti,Mlafi wa madara etc Kwanini mlafi wa madaraka asiitwe Mbowe ambaye amediriki hata kushawishi kubadili kifungu cha katiba bila utaratibu ili tu aendelee kutawala,kwa wenye akili again watapambanua hapo.Sasa at last Chadema walimfukuza ndani ya chama ulitaka ZZK afanye nini,Hes only 39,a politician,ulitaka akalime? akapige debe? unajua wewe.Sasa yuko anaendelea na Maisha yake ya siasa aliyojiamlia ili kuwatumikia Watanzania wewe mtu kama wewe bado uko nae kila kona sijui simwamini,Ndugu tupo tunaomwamini acha tumsikilize,kura hupigi pekeyako tunapiga watazania wote.
 
Kumbe mulimfukuza ilhali mnamuhitaji?

...Oooohhhh, atakayekiuka katiba ya chama hatuna msalia mtume!!!! we kijana vipi??????? Yaani ulikiuka katiba ya kule kuja kusimamia wavunja katiba wa huku?????

Kuna jamaa kaandika hivi, nikacheka sana. Hivi kweli ZZK alisema hivo?
 
Mods unganisheni uzi zote za ACT ili Bavicha wahangaike huko imekua kero sasa
 
utakuwa na mapungufu ya akili kama utakuwa humjuwi zzk ni ccm b na msaliti number moja duniani!
 

Ukiangalia hayo mashtaka kuanzia 4 .... ni ya kuunga ungana na kurudia rudia ili kutimiza hiyo haja ya kumfukuza
 

Kwa hiyo ndo Zito?
 
Mimi nikiwa mkazi wa Urambo binafsi nina maswali mengi sana ya kujiuliza, kulikoni Zzk kuja ktk jimbo ambalo hukua ukitamani hata kidogo kufika, kwa kumbukumbu zangu Zito tulisha kuomba sana uje jimboni kwetu utusaidie kufyeka msitu wa Ccm uliokuwa umestawi lakini kwa mahaba yako na mbunge wa jimbo hili "Mh namba" kamwe hukuthubutu, makamanda wenzio walifika mara kwa mara wakiongozwa na Kamanda Mbowe tumeufyeka msitu tuka panda mbegu wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mavuno tulivuna vizuri sana, ujio wako unanifanya niamini ni kwa ajiri ya matokeo mazuri ya Ukawa kwenye uchaguzi huo,unakuja kutuvuruga Ukawa wetu ili swahiba wako mh 6 apite kirahisi,naomba ni nukuu maneno matakatifu yanayo sema hivi; "Makwazo hayana budi kuja ila ole wake mtu yule yanayo kuja kwa ajili yake" mwisho wa kunukuu, naamini kwa kuwa tulisha dhamilia kufanya mabadiliko hutaweza kuturudisha nyuma, naomba kuwasilisha!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…