GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,429
- 120,789
Hivi ni kwanini kila Mtuhumiwa pindi awapo Mahakamani au hata Polisi akiachiwa tu huru hutoka nduki ( hukimbia mara moja ) kutoka eneo la Mahakama au Polisi huku wengine wakiwa radhi hata kukimbia pekupeku na gari watapandia mbele kwa mbele?
Nini hupelekea hali hii ambayo nimekuwa nikiishuhudia mno pale Mahakamani Kisutu na pale Central Police. Kwa mfano leo hii hii nimemuona Mtu mmoja maarufu sana alipoachiwa tu kutoka alikohifadhiwa tai yake kaja kuifungia Kona ya Stesheni, Kiatu kakivalia Kituo cha zamani cha Mabasi cha Kisutu, Rozari yake kaivalia pale DIT na gari yake kaja kuipandia hapa maeneo ya AMREF / Msalaba Mwekundu na kakumbuka kuwa hakuvaa Soksi tayari akiwa ameshafika Nyumbani Kwake.
Nitashukuru kwa majibu yenu hasa ukizingatia kuwa kila Mtanzania ni Mtuhumiwa au Mfungwa mtarajiwa.