Kwanini watu wengi wanalichukia jeshi la polisi na si majeshi mengine?

zinc20

Member
Dec 4, 2014
25
7
Habari zenu wana JF!

Mh yeah, well! Nimekaa chini nikawaza sana nikakosa majibu jinsi wananchi wanavyolichukia jeshi la polisi. Wananchi hawawapendi askari polisi, wanawachukia kupita maelezo, ikitokea askari kapata janga, ndio furaha yao hulipuka na kushadadia kwa maneno ya staha. Wengine husema, 'bora afe', wapigwe tu, mara wengine huwaita kwa jina lingine jipya 'Policcm'.

Sasa mimi nashangaa sana, Kwanini chombo cha dola kinahusishwa na mambo ya siasa? Kwa Ninavyofahamu mimi, chombo cha dola ni mali ya serikali, na serikali na siasa ni vitu viwili tofauti. Sasa Kwanini kulituhumu jeshi la polisi kuwa ni la chama cha CCM? Kwani CCM ina chuo cha kuzalishia Polisi? Chuo chao kiko wapi?

Kwa Ninavyojua mimi ni kwamba serikali ndio inachuo chakuzalisha askari kilichopo Moshi, na askari ni kwa ajili ya wananchi, sasa kwanini raia wawachukie watu ambao wamewapa kwa hiari yao kulinda usalama wao na mali zao? Chuki Za nini juu ya jeshi la polisi?
 
Umemaliza lini depo afande polisi? Kawauliza wakubwa zako wanajua kwanini mnachukiwa na raia.
 
zinc20

Naona kipigo walichokupa hadi kuandika unaweweseka mimi mbona nawapenda sana polisi.Ukiwaona kaa mbali nao usijitie kuwazomea au kuwaletea siasa.
 
Last edited by a moderator:
Umemaliza lini depo afande polisi? Kawauliza wakubwa zako wanajua kwanini mnachukiwa na raia.

Ndugu Makamee Mm Ni Raia Wakawaida,hata Jeshi Sijasomea,ila Nilitaka Kujua Kwann Sisi Raia Tunawachukia Sana Hawa Askari Wetu Ambao Wanatulinda Sisi Na Mali Zetu?Tunalala Usiku Na Wake Zetu Na Watoto Wetu Kwa Amani Mpaka Kunakucha Bila Ya Tatizo Lolote.Wewe Unafikiri Bila Hawa Watu,ungeweza Wewe Kula Ugali Ukashiba Tena Kwa Utulivu Wa Hali Yajuu Bila Ya Hawa Watu Kuwapo?
 
tatizo raia tunawadharau sana sasa wao wanawaoneshea ubabe pia kuna ujinga wa kutokujua sheria sehemu ya 8 ya Kanuni za adhabu, sisi hatujui sheria ndo maana tunalalamika pia ujue anayewalalamikia polisi kuna jambo ovu analifanya au ana nia ya kulifanya.

kuna kitu katika sheria za jinai kinaitwa " mala prohibita" yaani acts prohibited by the law in a certain place mfano mirungi kenya ruksa lakini Tanzania ni kosa so vitu kama hivyo ndo vinawakosanisha polisi na raia.

pia sometimes na askari wasitumie ubabe uliopitiliza kiasi kwamba mda wote anaogopwa kama mtu fulani mbaya.
 
Habari zenu wana JF!

Mh yeah, well! Nimekaa chini nikawaza sana nikakosa majibu jinsi wananchi wanavyolichukia jeshi la polisi. Wananchi hawawapendi askari polisi, wanawachukia kupita maelezo, ikitokea askari kapata janga, ndio furaha yao hulipuka na kushadadia kwa maneno ya staha. Wengine husema, 'bora afe', wapigwe tu, mara wengine huwaita kwa jina lingine jipya 'Policcm'.

Sasa mimi nashangaa sana, Kwanini chombo cha dola kinahusishwa na mambo ya siasa? Kwa Ninavyofahamu mimi, chombo cha dola ni mali ya serikali, na serikali na siasa ni vitu viwili tofauti. Sasa Kwanini kulituhumu jeshi la polisi kuwa ni la chama cha CCM? Kwani CCM ina chuo cha kuzalishia Polisi? Chuo chao kiko wapi?

Kwa Ninavyojua mimi ni kwamba serikali ndio inachuo chakuzalisha askari kilichopo Moshi, na askari ni kwa ajili ya wananchi, sasa kwanini raia wawachukie watu ambao wamewapa kwa hiari yao kulinda usalama wao na mali zao? Chuki Za nini juu ya jeshi la polisi?

polisi wanachukiwa kwa sababu mambo makuu haya

1) kubambikia kesi watu
2) uonevu
3) rushwa
 
Tatizo kubwa limeanza kutokea kipindi hiki cha uongozi baada ya wao kukubali kuwa ni watetezi wa ccm, hapo zamani ilikuwa ukisikia polisi ameuawa na majambazi wananchi mnasikitika sana ila kwa sasa ni tofauti watu wanashangilia!! Siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu ni askari akasema kwa kweli kwa sasa tunashida sana kwani serikali imetukosanisha na jamii kutokana na mambo ambayo hayana msingi, watu wanaandamana kudai haki zao ambazo na cc polisi zinatuhusu ila mtatumwa kwenda kuwapiga!!! Na ndio maana Tibaigana alitoa rai kwa viongozi wa jeshi la polis kuwa watumie taaluma zao na sio kuongozwa na wanasiasa!!na hata jwtz nalo siku hizi sio kama zamani tokea wajiingize kwenye mzozo wa gesi mtwara kuwaua raia wanao pigania rasilimali yao, lakini yote haya yanatokana na kuwa na katiba mbovu, rais ndiye awe anateua karibia kila mtu unategemea nini?? Ila nyie polisi hasa wa vyeo vya chini maisha yenu tunayajua sisi jinsi mnavyoishi kwa shida.Na mtaendelewa kuchukiwa sana tu hadi hapo mtakapo acha kutumika kama ccm b.
 
Habari zenu wana JF!

Mh yeah, well! Nimekaa chini nikawaza sana nikakosa majibu jinsi wananchi wanavyolichukia jeshi la polisi. Wananchi hawawapendi askari polisi, wanawachukia kupita maelezo, ikitokea askari kapata janga, ndio furaha yao hulipuka na kushadadia kwa maneno ya staha. Wengine husema, 'bora afe', wapigwe tu, mara wengine huwaita kwa jina lingine jipya 'Policcm'.

Sasa mimi nashangaa sana, Kwanini chombo cha dola kinahusishwa na mambo ya siasa? Kwa Ninavyofahamu mimi, chombo cha dola ni mali ya serikali, na serikali na siasa ni vitu viwili tofauti. Sasa Kwanini kulituhumu jeshi la polisi kuwa ni la chama cha CCM? Kwani CCM ina chuo cha kuzalishia Polisi? Chuo chao kiko wapi?

Kwa Ninavyojua mimi ni kwamba serikali ndio inachuo chakuzalisha askari kilichopo Moshi, na askari ni kwa ajili ya wananchi, sasa kwanini raia wawachukie watu ambao wamewapa kwa hiari yao kulinda usalama wao na mali zao? Chuki Za nini juu ya jeshi la polisi?

Tatizo lako umekulia kambini, hujuwi kero za Polisi. Polisi wanakera we ndugu yangu!
 
Mi siwapendi polisi. Siku za uchaguzi wanapiga watu hovyo, hawachagui mzima, mgonjwa wala mtu mzima sawa na mamaake na babaake. Wao ni kupiga tu, tena wanapiga ile mirungu yao minene kama mkono, na hawachagui pa kupiga. Siwapendi haswa
 
Mi siwapendi mapolisi badala ya kulinda raia wao ndo baadhi wana shirikiana na wahalifu uonevu kwa RAIA hasa wakidai haki zao mfano Mwangosi badala ya Kumlinda wakamwua kinyama pia rushwa kwao ni kawaida
 
Ugomvi wangu na hao jamaa ulianza tangu waliponikamata na kunitandika marungu ya ugoko mpaka nikalazwa kwa ambalo mpaka leo sijalifahamu.....kwa kuwa mimi mnyonge nimemuachia MUNGU kilio change.......huwa nafurahi sana nikiona askari kapatwa matatizo au kafa kabisa................
 
Nikuombe radhi mkuu, huenda ni mimi niliyekupa za ugoko
 
Kwani mleta mada, hujawahi hata kukamatwa na askari wa usalama barabarani?
Watu wanalichukia Jeshi la Polisi kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo:-
(1) UONEVU: Askari Polisi wengi hupenda kuwaonea raia. Wanachotafuta huwa ni sababu tu ya kutenda kosa halafu wanakushughulikia bila huruma. Hata mahali ambapo pangehitaji angalau busara kidogo hawakubali.Kwa Mfano hata Usalama barabarani siku hizi akikukamata hata kwa kosa dogo analoweza kukupa warning anakomaa na kukuandikia faini na hakupi muda wa kujieleza.Labda kama chance inaruhusu kukudai rushwa.
(2) RUSHWA:Askari, wakiwemo wale wa pikipiki maarufu kama tigo wanazunguka mtaani siyo kulinda raia bali kutafuta ni wapi mambo hayako sawa ili wachukue pesa
(3)KUBAMBIKA WATU KESI: Askari wana tabia ya kubambika watu makosa wasiyofanya. Unaweza ukawa na chuki na mtu fulani ukaenda kula dili na askari wakamkamata na kumbambikia kesi.Wakati mwingine hata kukuua kabisa kama tukio lililotokea Arusha la Mwanamke mmoja kugombana na jamaa akawapigia askari wakaja na kumtwanga risasi, sijui hata hiyo kesi iliishia wapi.
(4) DOUBLE STANDARDS: Unaweza ukaibiwa, ukaenda kuripoti polisi na kumtaja suspect wako. Wanachofanya polisi ni kutafuta pesa kwako ikiwa ni pamoja na usafiri wa kumfuatilia mtuhumiwa na wakishampata wanaanza kutafuta pesa kwake pia. Mwishowe wanaiua kesi kiaina au wanaipeleka mahakamani ikiwa haina mashiko.
(5) UHUNI: Sasa hivi ni jambo la kawaida tu kukamatwa na Askari kama wa Usalama barabarani akakuandikia faini halafu ukimwambia pesa unayo kwenye tigo pesa mfano anakupatia namba yake umrushie kwenye simu yake.
YAPO MENGI MNO, KWA LEO NAISHIA HAPA MENGINE WADAU WATAENDELEZA !
 
wengi wamejiunga sio kwa sababu ya elimu yao bali kujuana ,na wameriti mitaala ya kikoloni kukandamiza raia hawana kabisa utu,marekani ukitaka kujiua wanakubembeleza huku ndio wanaweza kukuua kabisa ,wengi shule hamna wanatumia nguvu kuliko akili
 
Hao polisi mnaowachukia hivi wasipofanya kazi masaa machache unadhani kitatokea nn......
 
Back
Top Bottom