Kwanini watu wanapenda 'walipotokea' namna hii?

kanyela mumo

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
2,034
2,106
Sijui ni ganja ninazo puliza au ni maruweruwe ya wakati huu ninaopitia!

Let me be honest. Nimenza mwaka vibaya nusu nione nafsi yangu haina thamani japo ina thamani kubwa na wengi huwa wana respect. Jeuri niliyokuwa nayo ilitowekea Gizani ila Mungu ni mwema kwa kila jambo na wakati wote.

Life liliponipiga zaidi nikakosa Pesa ya Tumbaku Ubalozi ikabidi nipige mishe za kuosha magari kwa siku buku tatu. Hiyo ikiwa pamoja na chakula na nauli. Amini nakwambia ilikuwa ngumu lakini ilinijenga zaidi kuujua mtaa maana ni miaka mingi sana sijapitia street road hope.

Wakati naosha Magari nimeona umalaya wa aina yake kwa baadhi ya hawa watu wenye magari, bodaboda, daladala na hata sasa kwa madereva wa Uber. Hakika imeniuzunisha sana na kubaki na maswali mengi kama hili: Je, kwanini watu wanapenda walipo tokea?

Kwanini baadhi ya Wake kwa Wanaume sio waaminifu kiasi hiki? Na ni idadi kubwa sana.

Vibinti vinatumika kama Big G na vipo bize kupita maelezo kupost picha za kuashiria umalaya na kuomba namna watu wanavyoweza ku-share picha zao za kikahaba kahaba, kweli?

Nafikiria mpaka nachoka! Wazazi tuamke na jamii nzima tuamke; maadili ya kitaifa ni kitu muhimu, hivi sasa si salama kwa taifa letu linalokwenda kwa speed katika uchumi wa kati.

Simu ni kitu kinachotuingiza tusipo tarajia iwe kwenye matatizo au furaha, ni wakati wako kutumia simu kwa ajili ya future yako. Kama wewe ni mrina asali, jitaidi kusoma kuhusu uvunaji wa asali au pengine namna nzuri ya kuweka mizinga au kuchonga au hata namna ya kuwavutia nyuki sehemu zenye mizinga.

Au kama una ndoto ya kuwa bondia penda kutazama mabodia waliopita, namna wanavyo sukuma ngumi au kukwepa ngumi, hii itakusaidi kuondokana au kupunguza namna ya kupenda ulipo toka na pia itakusaidia kujua zaidi kuhusu kile kinacho kuletea kipato na hata kuongeza kipato.

Tusipende sana tulipo toka bora tupende KAZI na kwa mbali "Msuba" na kuwa mjinga. Kama huu ujinga nilioandika mimi, maana mimi ni mjinga mpaka natamani niwe limwehu.

Weekend njema Waungwana wangu. Mwana kaishanyonga, ngoja nile paf-paf-paf nipate utulivu wa karne hii namna gani nitaleta heshima kwa familia na jamii yangu ya Kitanzania.

One love kwa wote. Baharia wa zamani natokomea ki-Shaba Ranks, Buyaga buyagaaa maaaan!




Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuna ukweli hapa mkuu
ukishajitambua bora upige mishe zako kulikon upakomalie alaf ukishafilisika unaanza kupita makaburin et ONE DAY YES!!
Haha hahahahaha sentence ya mwisho imenivunja mbavu..

Sure watu wakishafilisika ndo utasikia.... Oohh nmekukimbilia wee Bwana wa mwajeshi
 
Kuna watu ukiwaambia unapenda vitu vitatu usipoweka wanawake atakushangaa, yani wao ngono ndo namba moja asee, mfano napenda

.kucheza game na movies
.kucheki mpira na marafiki wengine wanywaji sana
.kusafiri na kuwa na marafiki

usipowekana wanawake watu hawakuelewei kabisaaa ,hasa sijui shida iko wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ipo hivyo, nafikiri kwasababu imegawanywa kwenye makundi mawili kwa fikra zangu

1. Ngono imekuwa starehe kama starehe zingine

2. Wanawake wamekuwa kama bidhaa
siku hizi, ndoa siyo chanzo cha utulivu na heshima. Unakuta mtu ana familia lkn anawabadlisha kama nguo. Waache kujirahisisha na kuwa kama bidhaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom