Kwanini watu wakifulia huwa na ahadi tam tam? (Nikipata Pesa sitakunywa tena Pombe)

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,398
Ni maajabu sana!
Ujue kuna nyakati tafakarishi anazopitia binadamu zinashangaza sana! kuna watu wakifulia utawahurumia wanavyotia huruma, kuna kipindi kile ambapo mwanaume anapigika na kuishiwa kwelikweli hadi anaongea peke yake... (mzee mmoja alikuwa anatania Kwa kusema ni kipindi ambacho mwanaume Wa miraba minne anapotamani avishwe gauni aolewe)..

INASIKITISHA
Mtu anapesa za kutosha Leo, lakini siku akifilisIka usishangae utamsikia anakwambia " NIKIPATA PESA NITANUNUA BIBILIA/QUR'AN". na siku akizipata Pesa wala hanunui tena hiyo Bibilia!

Kwanini watu wakifilisika huwa wanafiki namna hii!
Kuna wengine Leo akiwa na Pesa wala hajali MKE na Wa watoto wake lakini akifulia utamsikia anakwambia " SIKU NIKIPATA PESA NITATOKA OUT NA FAMILIA YANGU" sasa bahati ikitokea kapata ndo kwanza anaongeza mchepuko!....
Kuna jamaa aliapa kuacha Kabisa Kunywa Pombe endapo akipata Pesa tena! Siku zikasogea akiahidi kuacha kabisa Kwa mkewe na wanae katu katu hatakunywa tena, basi mambo siku ya siku yakatiki tena akapata pesa, ikabidi ajipime Kwa kupita karibu na Bar ile aliyokuwa akinywa hapo zamani!
Akapita Mara ya kwanza shaaaaaah hadi upande Wa pili, akarudi tena akapita shaaaah hadi ng'ambo! Sasa akaona kafuzu ikabidi apite Mara ya Tatu kabisa kumaliza ubishi; alipofika mlangoni ikabidi aingie kabisa kuthitibisha kuwa yeye ni mwamba, alipofika humo akakaa kwenye kiti kwa upolee huku Kwa mbaali akidundisha kichwa na kuimba mziki Wa alikiba uliokuwa ukipigwa kwenye spika... " Nina majina mapya- kila moja amenipa- wananiita kipusa- Ooooh pasua Kichwaah!........Jamaa Kwa furaha akamwita WAITER Alimletee Bia mbili ajipongeze Kwa ushindi !!...
Tubadilike jaman!!!!!
 
Hiyo ndo pesa bwana! Inabadilisha kila kitu

Hata mimi nikipata pesa nita...
 
Ambacho huelewi ni kwamba maisha ni kama siasa! Wakati Wa kampeni ukipita ni mwendo Wa matamko!
 
Heri aliyekosa pesa kbsa kuliko aliefulia, usawa huu ukipata griss ukamwaga hata tone, jiachie au subir itakusaidia kuregeza misumali ya jeneza utoke kupiga chabo watu wakila raha duniani. Mi nahisi ifike mahali ukiajiriwa kwenye usawa huu kitu cha kwanza ni kusaidia ndugu kuchonga jeneza lako na sanda sio tusumbuane, pili utoe rambi rambi kbsa ya mazish yako
 
Heri aliyekosa pesa kbsa kuliko aliefulia, usawa huu ukipata griss ukamwaga hata tone, jiachie au subir itakusaidia kuregeza misumali ya jeneza utoke kupiga chabo watu wakila raha duniani. Mi nahisi ifike mahali ukiajiriwa kwenye usawa huu kitu cha kwanza ni kusaidia ndugu kuchonga jeneza lako na sanda sio tusumbuane, pili utoe rambi rambi kbsa ya mazish yako
Una hoja huenda lakini sijapata point yako iko WAP mkuu
 
Back
Top Bottom