Kwanini watu hulala bila kufumba macho?

Daktari wa Manchester

JF-Expert Member
Jun 1, 2020
350
401
Habari za mda huu.

natumaini wote ni wazima wa afya Kama sio Mungu akusaidie upate afya njema

Watu wengi huzoea kwamba tunalala huku tumefumba macho,ila asilimia 13-14% ya watu dunian hulala bila kufumba macho ,inawezekana hatupo aware kwamba tunalala huku tumefumba macho au la kwa sababu hatuwez kujiona wenyewe tukiwa tumelala. Muda mwingine ukiona unamka asubuhi na kuona macho yanauma ,macho kuwa makavu,macho kuwasha huenda ikawa unatatizo Hilo.

Fahamu sababu,dalili ,madhara, na jinsi ya kutibu tatizo hili

sababu zinazosababisha mtu kulala huku macho yakiwa waz
Tatizo la watu kulala macho waz wenzetu wanaliita NOCTURAL LAGOPTHALMOS

1.jeraha .jeraha katika uso,jicho au nerves ambazo zinacontrol uwezo wa kope kumove wakati unavyoangalia hususani mwanga mkali unavyomulika au ule muda mwanga unapokua hafifu Mana lens ya jicho diameter yake huongezeka ili kuweza kupitisha mwanga kwa urahisi pia jeraha hili Mda mwingine husababishwa na matumizi ya vipodozi(cosmetics) kutokana tatizo hili hupelekea uwezo wa kope kushinda kujifunga

2.Surgery karibia na mishipa ya fahamu
images (3).jpeg

3. Uvimbe
uvimbe katika jicho pia unaweza ukasababisha jicho kutoweza kufunction vizuri wakat ukiwa umelala au la Mana mishipa inayo control nerve itashindwa kuratibu vizur movement za kope na kupelekea tatizo Hilo.

4. Mwisho tatizo Hilo huweza husababishwa na stroke
Kwa Nini inabidi ulale huku umefumba macho
Kulala huku macho yakiwa closed kunahakikisha usalama wa macho na parts nyingine ambazo ziko ndani ya macho Kama cornea pia hulainisha macho ukiwa umelala na ndio maana watu wengi wakilala macho wazi huamka macho yakiwa makavu

Jinsi ya kutibu hili tatizo
Ili kutibu hili tatizo ni kuenda katika kituo Cha afya kilicho karibu nawe ili uweze kupata solution ya hili tatizo

..SOURCE.Healthline.com
321517_1100-1100x628.jpg
 
Kilindi niko chuo niliamka majira ya saa tisa usiku, ile kumwangalia roommate wangu aliyekuwa analala kitanda cha juu nikaona yuko kimya amelala ila macho yako "ON" nikaamini amekufa nikawashitua wadau. Katika kumwangalia angalia na kumgeuza akashituka kumbe mzima wa afya ila alikuwa na tatizo la kusinzia huku macho yakiwa ON.
Mawazo mengi husababisha tatizo hili.
 
Kilindi niko chuo niliamka majira ya saa tisa usiku, ile kumwangalia roommate wangu aliyekuwa analala kitanda cha juu nikaona yuko kimya amelala ila macho yako "ON" nikaamini amekufa nikawashitua wadau. Katika kumwangalia angalia na kumgeuza akashituka kumbe mzima wa afya ila alikuwa na tatizo la kusinzia huku macho yakiwa ON.
Mawazo mengi husababisha tatizo hili.
Mda mwingine huwa inasababishwa na stress
 
Na wenye macho makubwa ya duara wengihawafumbi macho.

Kuna mtu yeye akilala macho yanakuwa wazi kama yanaelea yaani kiini kinazunguka..

Hospital wanasema ni maumbile so ugonjwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom