Kwanini watu hawasahau penzi lao la kwanza?

an alpha male

JF-Expert Member
Mar 28, 2022
828
1,746
Kuna mtu aliwahi kusema, "kama hautojipenda mwenyewe basi, hauwezi kumpenda yeyote kwasababu hauwezi kutoa upendo ambao hauna". Hauwezi kufanya mtu akupende ikiwe wewe mwenywewe hujipendi. Maisha ni kama ndoto, tunacheka, tunalia,tunaishi na kufa.

Kila binadamu anatafuta anachohitaji, kwasababu binadamu wana hatima za kung'arisha ndoto zao. Ila mapenzi ni kitu kinachotuunganisha, binadamu wote tunahitaji upendo.

Yalikuwa ni maneno ya kuelezea mapenzi (upendo). Unajua kiukweli kila binadamu anatafuta mtu wa kumpenda ila tunaogopa kuwapokea kwenye mioyo yetu. Kitu kibaya ni kwamba uogope au usiogope utateseka tu.

Kwahiyo kuogopa ni kuteseka na kutokuogopa ni kuteseka pia. Chagua moja uteseke kwakougopa mapenzi, au uteseke kwa kuwa kwenye mapenzi. Acha turudi kwenye mada, nilkua nataka ujue kitu kidogo kuhusu nacho taka kuzungumzia(mapenzi).

Lets go. Kuna vitu vingi vya kwanza kwenye maisha yetu, kama kumiliki gari kwa mara ya kwanza, siku ya kwanza shule. Kitu cha kwanza ndio kumbukumbu kubwa katika maisha yetu, ila inategemea na hali, inaweza kutupa hisia za furaha au kuhisi maumivu (ecstasy or sense of devastation), ila kitu ambacho watu wanakumbuka sana ni penzi lao la kwanza. Mapenzi ni kitu maalumu, ila penzi la kwanza huwa linakuwa ni la kipekee.

Lina kutambulisha hisia ambazo haukuwahi kuwanazo kabla, kwa mazuri au mabaya na huwa inausisha hali ya kushangaa, (intrigue and excitement). Pia penzi la kwanza huwa haliishi litakuwa ni sehemu, ya vile ulivyo muda wote wa maisha yako.hizi ni baadhi Sababu kubwa ya kufanya watu wasisahau penzi lao la kwanza

(1) Penzi la kwanza linanguvu; ghafla unahisi, na unakubali kwamba unamjali mtu, katika hali ambayo hauelewi vizuri kwanini, ni mara yako ya kwanza unapata hisia za mapenzi, milango yako ya ufahamu inafungua, dunia ya uwezekano na furaha, pia na hisia za uoga, ni kitu ambacho haujawahi kupitia kabla. Mtu kupitia hali hii inamtengenezea ratiba ya kudumu kwenye kumbukumbu zake, na kumfanya iwe ngumu kumsahau mpenzi wake wa kwanza.

(2) Penzi la kwanza huja na vitu vingi vya kwanza; sio kwamba penzi lako la kwanza lilikufanya ukutane na mtu aliye uteka moyo waku tu bali, inawezekana pia alikushawishi ufanye vitu vipya, au alikupitisha kwenye changamoto mpya, tena nyingine zikasaidia hata kwenye kukufanya uwe mtu bora.pia mara nyingi penzi la kwanza huja na vitu physical vya kwanza, labda siku yako ya kwanza kukiss, au ulipoteza bikra yako, haya matukio ya kimwili huwa pia yanaishi kwenye kumbukumbu zetu za maisha.

Mwisho; kwasababu penzi lako la kwanza ni ngumu kusahau, haimaanishi kwamba yalikuwa ni mapenzi ya kweli(Truelove) ambayo hautakuja kuyapata,hapana, ila ni ujue Mapenzi yanakuja na kuondoka,ila hakuna aliyekuambia, jinsi gani ya kujifunza kuyaacha yaende..
 
Nice topic...
Alikua akitoka kazini lazima apitie kwetu kuniona...
Na alikua akija lazima aje na tunda au card,
I felt loved,
And this is what we want..
To feel loved,wanted,supported,sexy
Isn't it??
Its true, everybody needs those staffs
 
Sitokusahau Sarah, tulipendana nahis ni zaid ya Romeo and Juliet, mapenz yalianza nipo form2 nayey yupo darasa la sitA. TUKATOANA UBIKIRA

mapenz yetu yalidumu kwa miaka almost 7-8 ivi. tulipendana sana ata Mungu anajua na wazaz wa upande wote walijua tunaoana hatukuwai kuchokana. Lol Yule meneja wa benk fulani apa mjin kanipokonya tunda langu kwa ushawishi wa pesa na ndinga kali za kijeruman.

MAPENZ YALIKUFA ATA SIJUI YUKO WAPI, MUNGU AMBARIKI SANA. kwakwl uchawi wa mwanamke ni pochi na ndinga kali tu hasa.

namuombea maisha maref siku tuonane ajionee maisha yangu kwasasa yalivyobadirika
 
Sitokusahau Sarah, tulipendana nahis ni zaid ya Romeo and Juliet, mapenz yalianza nipo form2 nayey yupo darasa la sitA. TUKATOANA UBIKIRA

mapenz yetu yalidumu kwa miaka almost 7-8 ivi. tulipendana sana ata Mungu anajua na wazaz wa upande wote walijua tunaoana hatukuwai kuchokana. Lol Yule meneja wa benk fulani apa mjin kanipokonya tunda langu kwa ushawishi wa pesa na ndinga kali za kijeruman.

MAPENZ YALIKUFA ATA SIJUI YUKO WAPI, MUNGU AMBARIKI SANA. kwakwl uchawi wa mwanamke ni pochi na ndinga kali tu hasa.

namuombea maisha maref siku tuonane ajionee maisha yangu kwasasa yalivyobadirika
Hypergamy doesn't care where you come from bro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom