Kwanini Watanzania wanashabikia vita sana? Je, ni low IQ au Sadism?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
Dunia nzima kila mtu ana wasi wasi na kuogopa hata Wamarekani wenyewe na Wazungu ni ngumu kukuta wakishabikia vita na kufurahia, lakini sasa hivi Watanzania wamegeuza ni Yanga vs Simba post baada ya post wakishangilia Vita ya USA, NATO vs Islamic Republic of Iran, sasa ni kwa nini?

Je, mnapenda kuona watu wakifa na watoto na wazee wakipigwa mabomu? I mean watu ambao Bara letu la Afrika linachuruzika damu kila mahali tulipaswa kuwa mwisho kushangilia vita.

Je, tatizo ni IQ ndogo ya kushindwa kuelewa mambo au ni sadism tu?

Hivi Tanzania tutafaidika nini kukiwa na nuclear war hadi mfurahie?
 
Barbarosa,

Sio low IQ.
We ndio unaamua watu waseme nini au vipi

Breaking News: Qasem Soleimani kalambishwa mchanga.

Huko alipo atakuwa amekabidhiwa mabikra 72 ambao bikra zao zinarudishwa upya baada ya kutunduliwa. Yuko bize.
Mengine low IQ ma nini jaza mwenyewe.

Unataka wote tuwe kama wewe.
 
wakurochi,

Ni nini sasa? Au ni sadism? Sijawahi kusikia wala kuona watu wakishangilia vita hata Wazungu wenyewe ambao ndio wahusika wakuu.
 
Ni sadism na low IQ.

Kwa watanzania hawa kushabikia vita ni ajabu kwani hawajui athari zake kwenye maisha yao binafsi.Kwa uwezo wao wa kufikiri wanaona vita ni kama tukio la movie tu.
Na hatimae ndio hawa hawa watakaokuja kulalamikia serikali kutokana na athari za vita ambayo imepiganwa mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya yote yameletwa/kusababishwa na fisiemu, watu wanatamani hata jiwe aje apigwe hapahapa wewe unaenda mbali sana huko kwa kushangilia vita ya mbali,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Hata wakihadithia ajali ya gari walioishuhudia, unaweza unafikiri ni sinema iliyowafurahisha. Sijui sababu
 
Barbarosa,

Sio low IQ.
We ndio unaamua watu waseme nini au vipi

Breaking News: Qasem Soleimani kalambishwa mchanga.

Huko alipo atakuwa amekabidhiwa mabikra 72 ambao bikra zao zinarudishwa upya baada ya kutunduliwa. Yuko bize.
Mengine low IQ ma nini jaza mwenyewe.

Unataka wote tuwe kama wewe.
Kiruu!
 
.
Screenshot_20200104-205042-picsay.jpeg
 
Dunia nzima kila mtu ana wasi wasi na kuogopa hata Wamarekani wenyewe na Wazungu ni ngumu kukuta wakishabikia vita na kufurahia, lakini sasa hivi Watanzania wamegeuza ni Yanga vs Simba post baada ya post wakishangilia Vita ya USA, NATO vs Islamic Republic of Iran, sasa ni kwa nini?

Je, mnapenda kuona watu wakifa na watoto na wazee wakipigwa mabomu? I mean watu ambao Bara letu la Afrika linachuruzika damu kila mahali tulipaswa kuwa mwisho kushangilia vita.

Je, tatizo ni IQ ndogo ya kushindwa kuelewa mambo au ni sadism tu?

Hivi Tanzania tutafaidika nini kukiwa na nuclear war hadi mfurahie?
Mzee meko anavyo penda kubambikizia watu kesi ni low IQ au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barbarosa,

Sio low IQ.
We ndio unaamua watu waseme nini au vipi

Breaking News: Qasem Soleimani kalambishwa mchanga.

Huko alipo atakuwa amekabidhiwa mabikra 72 ambao bikra zao zinarudishwa upya baada ya kutunduliwa. Yuko bize.
Mengine low IQ ma nini jaza mwenyewe.

Unataka wote tuwe kama wewe.
Qasem katimiza laws of nature,kwamba ukiuwa nawe utauwawa so kavuna alichopanda kwani ye kauwa wangapi asife?
 
Unajua nini mkuu, ni Kama msiba wa jirani vile. Huwa ni wachache wanaumia. Wengi wanakuja kula tu. Sasa ukifiwa ndiyo unaexperience yale maumivu.
Hata hivyo hii ni social disorder. Mtu anashangilia watu kugombana, wapenzi kuachana,kufirisika,kushindwa na vitu vyote vibaya. Vikitokea vinawafurahisha. Kwanini? Jibu ni selfishness . Yaani huamini katika mema ila mabaya tu.
 
Mi nashauri kila mtu ashabikie anachopenda. Wala asiwepo wa kupangia wenzie cha kushabikia.
 
Back
Top Bottom