kwanini watanzania kila vita wanashindwa?

Nondoh

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
298
478
Imekuwa ni hali ya kawaida kuwaondoa watanzania kwenye hoja ya msingi hasa pale inapokuwa imepamba moto na kuwahamisha kujadili jambo lingine tofauti na hoja iliyopo mezani.

Hali hii ya watanzania kuhamishwa kirahisi rahisi kutoka kwenye hoja ya msingi na kujadili hoja/mambo ya kipuuzi kiukweli inaakisi upeo wa kufikiri wa watanzania walio wengi.

Na hali hii inadhihirisha zaidi kwenye suala la mahitaji ya watanzania. Kiujumla watanzania hadi sasa haijulikani nini hasa wanakihitaji na nini wanapaswa kufanya. Kila nikitafakari huwa sipati jibu watanzania wanahitaji nini hasa ukizingatia akili na matakwa yao hubadilika mithili ya kinyonga anavyobadili rangi yake. Kama ilivyo kwa kinyonga kutojulikana rangi yake ni ipi hadi kufikia wengine wakisema rangi zote ni zake labda hata watanzani vyote vinavyo onekana na visivyo onekana, vibaya na vizuri vyote wanavihitaji.

Ni kazi rahisi sana kuuchezea ubongo wa watanzania kama vile kuichapa pia, huku wenyewe wakibadilika badilika kama kinyonga. Iwe serikali, chama tawala, vyama vya upinzani au hata mtu baki akawazungusha zungusha ka pia na wote wakamuunga mkono hata kama ni upuuzi.

Watanzania wamekuwa wakibadilika badirika kama kinyonga, yaani hawaeleweki nini hasa wanakitaka na kiujumla hawana kipaumbele. Mara wanakomalia wanataka katiba, mara wanataka rais dikteta, mara wanataka maisha bora, mara hawataki rais dikteta, mara hawataki ufisadi, mara mafisadi wanaonewa, mara ...

Watanzania walihitaji maisha bora wakaaminishwa maisha bora kwa kila mtanzania wakaamini, sasa sijui hayo maisha bora waliyapata au ndio wanayaishi kwa sasa manake sioni wakijadili tena. Au kuna mtu aliwazungusha kama pia wakasahau au chunusi aliwapitia wote wakasahau na hawakumbuki tena.

Watanzania waliaminishwa katiba mpya ndio mwarobaini wa matatizo yao hadi wengine wakaanzisha ukawa na wengine wakaendelea kuzitumbua kodi za watanzania kwa mwamvuli wa bunge la katiba. Mwishoni watu wakanunua magari na kujenga majumba kwa fedha za bwerere na wengine kuhamia UKAWA bila kurudisha fedha za dhuluma kodi ya watanzania waliyoipola wakati wa bunge la katiba na baadae kuitwa makamanda baada ya ungo kuchange gia angani.

Watanzania waliaminishwa tatizo la watanzania ni ufisadi hadi ikafika hatua wakaambiwa kuna mapacha watatu wanalitafuna taifa. Chama kikawadhihaki watanzania kwa kusema ndani ya siku 90 kitawafukuza ikawa kimya, baadae ikaongezwa miezi sijui 6 sijui 9 lakini wapi, huku ukweli ukiwasuta hadi leo kimya. Mwisho mmoja akatema ubunge akasepa zake, mwingine akahamia upande mwingine akaitwa kamanda, wa tatu akagoma kutolewa sadaka wakati anajua fika more than 90% wa chama wanaishi kwa ufisadi. Leo kimya hakuna cha rushwa wala mwenza wake ufisadi, ukiuliza wanakwambia fisadi alichukuliwa na wale huku wamemkumbatia NYOKA MWENYE MAKENGEZA MSAKA FEDHA na upande mwingine stori ya ufisadi imekuwa ngumu kumeza.

Vioja haviisha, katiba haiongelewi tena, ufisadi hauongelewi tena, maisha bora kwa kila mtanzania hayaongelewi tena, wameongelea udikteta umechuja, wameongelea hapa kazi tu sasa naona kauli hii inabaki kinywani mwa Ngosha pekee na hata waliomzunguka wakisema sura zao haziakisi wanacho kisema.

Huko nyuma yametokea masuala ya msingi ambayo yalihita mjadala mpana ili kupata ufumbuzi lakini ikionekana ufumbuzi utaathiri upande fulani watanzania wamekuwa wakihamishwa kwenye hoja na kuanza kujadili mambo yasiyo na tija.

Mfano sakata la wafanyabiashara wa Kariakoo na Serikali issue ilipokuwa hoti huku watu wakitaka suluhisho, ukatengenezwa mchezo zikaletwa taarifa za watu wawili wamenatana wakifanya mapenzi na kupelekwa hospitali ya Temeki, watanzania kama mazuzu wakauingia mkenge na kuhamia kwenye hoja isiyo na tija kwa taifa na kuachana na hoja ya msingi.

Mfano mwingine ni pale ulipochezwa mchezo wa kuwahamisha watanzania kutoka kwenye hoja/issue ya msingi na kuhamia kwenye sakata lisilo na tija kwa taifa la viungo vya binadamu vilivyotumpwa kwenye mto mpiji Bunju Dar es Saalam/Bagamoyo na wafanyakazi wa hospital ya IMTU huku wakiachana na hoja ya msingi.

Sasa kimbembe ni hili sakata la madawa ya kulevya ambayo yanaathiri mamia kwa maelfu ya vijana. Yanapoteza nguvukazi ya taifa na kuwacha watumiaji wakivuja mate kama machizi huku wazazi, ndugi au walezi hawajui nini cha kufanya na kuishia kuwalilia vijana wao.

Kiuhalisia Kingpins of drugs kama ilivyotokea kwenye masakata mengine wameshinda vita ya madawa ya kulevya na kuwabwaga watanzania kama walivyobwagwa kwenye masakata mengine yaliyopita

Godfathers of drugs, vikontena wao na wafuasi wamefanikiwa kuwahamisha watanzania kwa kiasi kikubwa kutoka kwenye hoja ya msingi ya kutokomeza madawa ya kulevya na kuwahamisha wajadili elimu na vyeti vya DAUDI ALBERT BASHITE sakata ambalo halina tija kwa taifa kuliko elimu ya BASHITE.

Hivi mataifa wahisani raia wao wanafanya kazi wanakatwa kodi, sehemu ya kodi hizo inaletwa misaada Tanzania, badala ya kujadili mambo ya msingi na hatua zichukuliwe, watanzania wanajadili vyeti vya BASHITE. Hivi wahisani wanajisikiaje.

Mfano ungine .....

Wakati mwingine nawaza naona Mzee Lowasa aliona mbali sana aliposema kipaumbele chake ni "elimu, elimu, elimu," lakini nikiwaza zaidi jinsi nao wasomi wanavyoingia kwenye mikenge hapo nakukumbuka hotuba ya Mwl Nyerere alipokuwa anahutubia chuo kikuu. Mwal alisema tatizo la watanzania ni "TABIA" hasa baada ya wanafunzi wa chuo kikuu kugoma wakati kuna wanafunzi 2 waliokwenda German hawakugoma...

Kutokana na matukio haya na tabia ya watanzania kufuata upepo nashindwa kuelewa nini hasa watanzania wanakihitaji. Vile vyote walivyokuwa wakivihitaji mwanzo hawavihitaji tena wala kuvipigania na hata hatua zikichukuliwa kama kuna pande mbili zinazosigana ya huku huamia huko na ya huko huamia huku yaani +ve hugeuka kuwa -ve na -ve hugeuka kuwa +ve. Yaani totally hawaeleweki.

Jadili bila povu
Picsart2017-05-3--18-56-52.png
 
Back
Top Bottom