Tangi Tomofu kibiki
Senior Member
- Mar 31, 2015
- 118
- 74
UNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.
Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishinamagari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.
Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.
1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.
2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.
kibikiwoods@gmail.com
Don't take it personal against him, amezungumzia mtazamo wake...ambao kwangu mimi naona yuko sahihi.Kwanza ningependa kuelewa maana yako ya usomi. Halafu, ni usomi kwenye fani zote au baadhi? Halafu kwako wewe utajiri unaupima vipi? Na umaisikini unaupima vipi?
Je kwako wewe ukisikia 'information is power' na "knowledge is light" hauamini misemo hii?
Halafu mashuleni na vyuoni tunafundishwa kushirikiana kwani mara nyingi tunapewa group assignments, tunafanya group discussions. Pili mitihani inapima learning outcomes at individual level na sio group level.
Hivi hao matajiri wameajiri wafanyakazi wote ambao hawajasoma? Kodi wanalipa? Halafu wangekuwa wasomi hasa wale wa 'mabasi malori' (mabasi ambayo yanaundwa bongo, na kwenye ajali yanaua asilimia kubwa ya abiria) wasingeyafanyia biashara mabasi hayo.
Kwa kifupi, naona kama wewe upendi shule, au shule ilikupa shida sana!! Halafu hatuendi shule ili tuwe matajiri bali kuweza kuishi vizuri katika nyanja zote kuanzia afya, biashara, uchumi, kilimo katika ngazi zote - mtu mmoja mmoja, familia, mtaa, kijiji mpaka dunia nzima.
Kusema maskini unawaonea kabisa.. Ungesema ni wa kiwango cha kati.. Hakuna msomi mwenye huo umasikini unaousema.
Naona unajitahidi justify kushindwa kwako na kuandika mambo husiyoyaelewa. Wanaolalamika maisha magumu humu ni wasomi au? Kimbia shule uone mwisho wake. Mwl Nyerere mwenyewe alisema elimu ndio mwanzo wa maendeleao. Elimu pia ni Zaidi ya darasani kuna formal na informal education. Waweza kuwa na elimu na ukafanya yote. Maelezo marefu ila hautambui unajenga hoja gani hasa. Cases chache zilizoshindwa ku-achieve kwa sababu zao zisikufanye uka generalize maisha ya wasomi woteUNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.
Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishinamagari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.
Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.
1⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.
2⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!
Sasa nisikilize:- Simaanishi kusoma hakuna maana, isipokuwa ninataka uelewe jambo hili: Kama ukipata nafasi ya kusoma, soma kwa bidii; lakini usibebe kila wanachokulisha madarasani; ukakileta huku mtaani. Mtaani panahitaji akili ambayo ni tofauti na hiyo iliyopimwa kupitia kukariri ya vitabuni, mwishoni wanakuzawadia makaratasi yaitwayo vyeti.
kibikiwoods@gmail.com
Alafu wasomi wengi wanaongozaa kwa ubishiiAliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro anawakilisha wasomi wengi sana.Wasomi ukiwaondoa makazini ni sawa na kutengeneza mstari wa umaskini wa kutopea.Usomi haujawasaidia kitu zaidi ya kufunga tai na umardadi tu.
Masikini ni yule anaetumia chini ya dola moja kwa sikuUNALETA USOMI MTAANI? UTAKUFA MASIKINI..!!
Ukichunguza katika jamii, utabaini kuwa sehemu kubwa ya matajiri ni wale ambao wana elimu ndogo ama hawakusoma kabisa. Katika miji na maeneo yote; wenye majengo ya maana, wenye makampuni makubwa, wenye utitiri wa malori na mabasi, wenye maduka makubwa ni wale wa "darasa la saba” au wale ambao hawakuingia darasani kabisa.
Wasomi wengi wana maisha ya kawaida yaani yale ya kiwango cha kubadilisha mboga, wakijitahidi sana wanaishia kujenga nyumba za kuishinamagari mawili ya kutembelea (tena kwa mikopo!). Wapo wasomi wengi tu wanaoishi kimasikini, kwa lugha ya kistaarabu tunasema wana maisha ya kuungaunga. Kiukweli idadi ya wasomi walio matajiri ni ndogo sana.
Lakini Umasikini wa wasomi wengi umeanzia huko shuleni na vyuoni wanakopatia usomi wao. Madarasani kuna mambo mawili wanafundishwa wasomi ambayo ndio yanayowaroga.
1️⃣ Wameelimishwa na kuaminishwa kwamba yule anaepata maswali yote kwa usahihi ndio anaonekana amefaulu. Ukikosea unahesabika kuwa u mjinga na wenyewe wanaita umefeli. Hata hivyo katika maisha ya kawaida hasa kwenye mchakato wa kutafuta hela, kujaribu na kukosea ni sehemu ya mafanikio. Kadiri unavyojaribu na kukosea mara nyingi ndivyo unavyojifunza na ndivyo nafasi ya kutajirika kwako inakuwa kubwa! Wasomi wengi kwa sababu ya "mentality" ya kuogopa kukosea huwa hawapendi kujaribu biashara kwa hofu ya kushindwa kuiendesha, na huamua kufa kimasikini wakitegemea mishahara pekee kwa sababu mishahara ndio pato lao la uhakika.
2️⃣ Madarasani kunahimizwa ubinafsi badala ya umoja. Angalia namna mitihani inavyofanyika. Kila mwanafunzi anafanya mtihani peke yake, na ukikutwa unaangalizia ama mnasaidiana na mwenzio ndani ya chumba cha mtihani mtapata adhabu kali ikiwemo kufutiwa mtihani! Katika maisha ya kawaida hasa ya kusaka fedha, unahitajika ushirikiano mkubwa sana, baina yako na wadau, wateja, wafanyakazi wenzio, marafiki n.k. Kwa kifupi unatakiwa kuwa na Networking ya kutosha. Huwezi kufika mbali kiuchumi kama utakuwa na "mentality" ya ubinafsi unaosisitizwa madarasani!