Kwanini wanawake ni wagumu kuomba radhi wanapokosea?

Kwanini wanawake ni wagumu kuomba radhi wanapokosea?

Bismack

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2018
Posts
387
Reaction score
496
Hivi nyinyi wadada tunaowapenda na kuwathamini sana kwanini hampendi kuomba radhi mnapotukosea?

Unakuta umemkosea boyfrend wako lakini huwezi kusema neno nisamehe, hivi hiki kiburi mnakipata wapi?

Au nikwamba mnajiona wazuri kiasi kwamba huwezi kujishusha kwa mpenzi wako? Mbona sisi tukiwakosea tunaomba radhi, tena wakati mwingine kosa ni lako ila unakuja juu mpaka mwanaume ndo anakuomba msamaha.

Hivi nyinyi viumbe tuwafanyeje? Yaani mimi kukupenda ndo kiburi kinapanda kiasi kwamba huwezi kujishusha kwangu?

Halafu tukishawatema mkaenda huko mkakosa mwelekeo ndo mnarudi kuomba radhi, sijui hapo ndo unafahamu unakua umewarudi.

Wadada unapokua kwenye mahusiano jaribuni kubadilisha fikra na kuacha dharau.


Ahsanteni.
 
Wako ndiye hakuombi msamaha na nijinsi mlivyokutana wanaume mlivyo wababe hivi mnaombaga msamaha kweli au wewe tu mkuu?
 
Pole sana...

Usimlaumu huyo mdada/mpenzo wako...

Laumu wazazi wake... tabia zinaanzia kutoka kwa wazazi...

Nashukuru Mungu sana mahondaw wangu hana tabia kama hizo...

Ni mwepesi wa kukiri makosa na kuomba msamaha...


Cc: mahondaw
 
tehteehh.....[emoji12] [emoji12]
Mdomo wangu umebaki wazi wallah.....[emoji47] [emoji47]
 
Kuomba msamaha ni tabia ya kiungu...kama ana shetani hawezi aisee mana shetani ni baba wa kiburi..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom