Hakuna mwanaume anayemuogopa mwanamke eti kisa kasoma, ana madaraka, fedha au nini!! wanaume wanachoogopa ni ULIMBUKENI unaowakumba wanawake wengi hasa wanapopata vitu hivyo; so they want to play safe. Wanawake wote wenye madaraka, shule, n.k. wana wanaume wanaowapanda kama kawaida. Tatizo kama mwanamke akiwa limbukeni au akiona kuwa madaraka yake, cheo chake, n.k. ndo dili sana akaanza kuonesha dharau, basi Mwanaume husepa mara moja.
Sasa mwanamke akishaona amekimbiwa ataanza kulalama eti kakimbiwa sababu ana shule, fedha au madaraka!! No amekimbiwa sababu ya ulimbukeni wake na si sababu ya vitu hivyo. Hata wanaume wanaozinguliwa na vitu hivyo kiasi cha kuwafanya wawe na dharau sana nao hukimbiwa vile vile na wake au wadada! Huu ni upanga ukatao kuwili.
Kwa hiyo ukiona umesoma, unafedha, cheo au madaraka makubwa, halafu ukaona wanaume wanakukacha, ujue una vijitabia vya kulingia cheo chako, mshiko wako au madaraka yako. Na hiyo tabia ni mbaya tu. Hata ukilingia sana uzuri wako bado wanaume watakukimbia tu!!