Kwanini Wananchi walimkataa na watamkataa Slaa

Nani kakutuma kumchafua slaa?kwa akili yako nani wa cc unaona anafaa?hivi unaweza kuuona udini ulivyotawala uteuzi na ajira za utawala awamu ya nne? Hivi wenzenu wakiamua kufanya kama mnavyofanya kwenye hii nchi wengine mtapona?
 
Nampenda Slaa kwa kuwa hawezi ku-compromise na mafisadi kama hawa watawala wa CCM. Anao msimamo unaoeleweka na kuthibitishwa. 2010 Watz walimchagua ila tu CCM walichakachua! Kama UKAWA itamsimamisha kuwawakilisha, CCM itakuwa na kazi nzito ambayo hawatauweza mziki wake!
 

itarahamwe bwana hiyo 2010 gamba c ndo liliiba kura mshindi alikuwa slaaa kama huamini na umejitoa ufahamu nakurudishia tena kumbukumbu ndio mwaka ambao magamba yalijitangazia yamepata asilimia 63 toka 85 za mwaka 2005 ni nani aliyezishusha kama co slaa???
 
sasa umefurahi neno padri mods wamefuta.


Suala siokufrahi, Ushauri wangu kwako jenga hoja nje ya uchochezi wa kidini na hila za kuamsha chuki za kidini miongoni mwa wasomaji na wachangiaji utaeleweka.

Kumbuka na elewa wazi Tunahitaji rais bora wa Taifa la Tanzania hatuhitaji kujuwa imani yake maana kila mmoja wetu

anayakwake, kufanya hivyo nikulipeleka Taifa Kaburini. Unapenda tuelekee huko?

Kuingiza udini na kashifa za kidini nikuharibu hali ya hewa ya michango na mada kadha wa kadhaa hapa jukwaani

Isitoshe uchochezi huu unaweza kutawanyika mpaka mitaani nakuharibu mshikamano na utulivu wa watanzania

wanaoishi kwa kupendana bila kujali tofauti za dini zao.
 
Kama Dr Slaa ataahidi kuwakamata akina baba Ritz haki ya mungu mimi binafsi nitampigia kampeni kuhakikisha anaingia ikulu.Kwa hali hii tuliyofikia Tanzania tunahitaji rais mwenye sifa kama za General Paul Kagame WA Rwanda, hatuhitaji watu laini laini kama akina Pinda au Makamba.Hapa ni TL tu.
 

hahaha.. UMEUA
 
Huwezi Kuwa na ndoto ya mabadiliko kwa kuendelea kuongozwa na watu wenye fikra na utendaji ule ule, et mtu anasema aah slaa atafunga viongoz wastaafu, aa cjui hatakuwa mchesh kama yule mwingne, mwenye akili timamu kabsa na hukudondoshwa chn ukiwa mchanga, utakubali kabsa tunahtaj mtu anayefikr na kutenda kitofauti
 
hutaki kuchangia ondoka sio unawalilia mods km VP pandisha Uzi WK hu upotezee si lazm ukoment

Naona kama vile unaweweseka tu,subiri hapo october umuone gr slaa anavyotinga magogoni.tunajua wachumia tumbo wote,wezi,wahujumu uchumi,wala rushwa,wauza unga na majangili mnamuogopa sana dr slaa kwani mnajua akiingia ikulu tu,wote mtakuwa wafungwa watarajiwa.
 
Taifa hapa lilipofikia ambapo rushwa na ufisadi ndio mtindo wa maisha ya viongozi tuliowapa dhamana linahitaji kiongozi asiyecheka na mafisadi,wala rushwa,majangili na wauza unga. Tunahitaji rais kama dr slaa ili ashughurikie hayo mafisadi,arudishe uwajibikaji na maadili kwa viongozi wa umma.AIDHA TUNAHITAJI KIONGOZI ATAKAYEPELEKEA TUPATE KATIBA BORA YA WANANCHI,YENYE MIIKO NA TUNU ZA TAIFA KAMA TULIVYOTOA MAONI YETU KWENYE RASIMU YA PILI.HATUTAKI RAIS ALIYESHIRIKI KUCHAKACHUA MAONI YETU KWENYE KATIBA YETU NA KUSHABIKIA KATIBA YA KIFISADI. Dr Slaa anatosha na ndiye mtu sahihi kwa sasa.
 
Mzee slaa hafai kuongoza hata kundi la bawacha kiujumla siyo kiongozi hafai kwa lolote lile hachaguliki na hatachagulika.

Ni kweli hafai kwa sababu atauvunja mfumo fisadi unaokuweka mjini,aidha akiingia madarakani wazembe mnaoishi kwa kuramba miguu ya mafisadi,majangili na wauza unga mtakufa njaa hivyo dr slaa si mtu mzuri kwa hayo magenge yenu ya uhalifu.
 
kujua mnadepend on ignorance of some people angalia sehemu ulizo taja halaf linganisha uelewa wao na hali ya maendeleo na sehemu nyingine za tz! Still bado wamewashtukia kwa hyo siku zenu zinahesabika
 
Upinzani wakitaka kuingia magogoni kiulaini, waitishe kura ya maoni ili kumpata mgombea mwenye soko.Sio kukaa vikao vya ndani
then maamuzi yanatolewa na kikundi fulani cha watu......wakae chini, watafakari washirikishe wapiga kura wao mijini na vijijini hakika
Safari ya magogoni itakuwa rais kama urais
 
kuanzia ulivyo anza uandish wa hoja yako, na namna ulivyo jaribu kutengeneza hoja yako dhaifu,inaashiria nafsi na ubongo wako havna ushirikiano.
Magamba mmefuga wez,wauza unga,majangil,n.k kwa kutowawajibisha [sabab ndo utamadun wenu].sasa mnaofia utawala mpya nje ya chama chenu KWA MADHAMB YENU,subir hukumu za hak na za kwel kutoka kwa viongoz [makin nje ya magamba]
 


Mkuu wazo lako nizuri, isipokuwa huu ndio utakuwa mwanzo wa uchochoro wa mivutano, matamko nakila aina ya fujo.

Hili laweza kuwasambalatisha kirahisi kabisi ikizingatiwa kutakuwa na ufa ambao CCM watapenyeza Rupia na

kufanyakazi
kwa ufanisi mkubwa wakuitekeza UKAWA.
 
walimkataa dhidi ya msHindi aliyepata kura kiasi gani kiasi cha tume ya uchaguzi wenyewe hawajui! raisi alipita kimiujiza bila idadi kamili ya kura
 
Mmezoea kuomba net tu hamfikirii maendeleo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…