Kwanini wanamuziki wa Bongo hawana mafanikio?

Kwanini wanamuziki wa Bongo hawana mafanikio?

Wengi wamekacha shule. Hivyo uelewa wao wa mambo ni mdogo. Wakisha pata hela wanadharau wenye shule. Wanadahani hela kazi yake ni Mademu, Pombe na Show Off (e.g. Very expensive Cars, Renting very expensive houses, dressing expensive jewelleries, clothes, nk incomparable to their incomes) wakati hela zenyewe za madafu!! Ushauri: Ukiwa msanii ukapata hela-(make wao wana opportunity kubwa ya kupata hela nyingi kwa wakati mmoja) ajiri business Manager: This should be in charge of other businesses apart from music. Huyu ata ajiri hata Docta wako. Msanii unakufa na Madawa ya kulevya Tumboni!! Tatizo lao wamezoea MANAGER wa music/Mauzo na PROMOTER TU.
 
Mara ya mwisho ulinunua album original ya msanii lini?
 
Kwa sababu hawa si wanamuziki ni wababaishaji tu. Mwanamuziki anatembea na cd mfukoni, toka lini?
 
Fleva ni muziki wa mapito tu. Wasanii wanaokotwa na Ruge mitaani then anawabebesha unga kwa kupewa ahadi ya free air time. Akikataa basi anatafutwa punda mwingine abebeshwe. Mtu hana shule ukimtajia milioni 20 presha juu na anajiona tayari kawa msanii wa kimataifa. Mwisho wa siku utasikia kapasukiwa na madawa South na muokoaji maiti aidha Kinje, Jo Kusaga, au Ruge.
 
Mara ya mwisho ulinunua album original ya msanii lini?


Mkuu, wasanii wa fleva hawana album original kwani nyimbo/beats zao ni za watu wengine hawa ma Big G wanawekewa sauti tu tena inachujwa weeee ili mtu apate kusikika vizuri. Ukitaka kujuwa ukweli nenda kamuone Diamond au msanii yeyote wa fleva live uone wanavyotokwa na mishipa shingoni utafikiri mtu anataka kuzimia.
 
Secret Service umepotea sana huku jf siku hizi kama fb mada zingine kama hizi tuwe tunazisusia
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, wasanii wa fleva hawana album original kwani nyimbo/beats zao ni za watu wengine hawa ma Big G wanawekewa sauti tu tena inachujwa weeee ili mtu apate kusikika vizuri. Ukitaka kujuwa ukweli nenda kamuone Diamond au msanii yeyote wa fleva live uone wanavyotokwa na mishipa shingoni utafikiri mtu anataka kuzimia.

ukweli mtupu
 
Issue ya upeo wao mdogo na shule ni mojawapo tu ya sababu. Lakini tatizo la wanamusic kufilisika ni tatizo la dunia . Kwa wanaojua music na wafuatiliaji.......alifiriska michael jackson, toni braxton, eddie murphy, chriss xross ......na wengineo wengi sana tukiwataja wote tutajaza pages. Achana na walio kufa na drugs . So plz mleta thread kama hujui vitu au hujafanya utafiti ni bora ukae kimya au uulize. Pia wanamusic waliofirika kwa tz sio wa bongo fleva tu wapo akina Remi ongala, gurumo, marijani ....etc. Je nao walikuwa watu wa swaga na brings? Wa tz tunapenda sana kulaumu na kutoa kasoro ya vitu hata tusivyovijua.
 
Hawafanikiwi kwasababu ya mfumo mbovu wa soko la kazi zao.
 
Unazungumzia mafanikio gani ? ya umaarufu au ya kiuchumi ?.....na hiyo "nje" unayoizungumzia ni Ulaya, America, Asia au sehemu nyingine ya Africa ?

Hata mafanikio ya wanamuziki wa kiafrika nje ya nchi zao ni mmoja mmoja sana, na huwezi kulinganisha na wanaofanyia shughuli zao Marekani....unachokifanya Marekani ni rahisi kuonekana duniani kutokana na ukubwa wa Marekani....hata Ulaya, Asia na America kusini nao wanatoka mmoja mmoja sana na mara nyingi wanalazimika kuhamia Marekani kwa mafanikio zaidi.

Kwa kuwa tu unaangalia muvi za Hollywood haimaanishi dunia iliyobaki imeacha kutengeneza filamu la hasha, ukweli ni kwamba Ulaya na Asia wapo mbali sana na wanazalisha filamu kila kukicha na zinakidhi masoko yao...ila linapokuja suala la kidunia, Hollywood ni level nyingine.

Sasa je, unawalinganisha wasanii wetu na wale wa Marekani na ulaya ? na kama ni mafanikio ya kikazi kibongobongo mbona tulishakuwa na akina Marehemu Marijani, Remmy, Ngurumo n.k ingawa kiuchumi ndio hawakufanikiwa.
 
Na hata kama ni mafanikio ya kiuchumi, ni vigumu kupima kwa wasanii wetu kutokana na uchanga wa kiwanda plus ulimbukeni unaotokana na background ya wasanii wengi.

Na hata huko nje sio wasanii/wanamichezo wote wana uwezo unaofanana wa kuendesha shughuli zao nje ya kile kipaji alichonacho.....hata ukikusanya watanzania elfu moja na kuwapatia milioni hamsini kila mmoja, amin amin nakuambia ukirudi mwaka mmoja baadae utakuta ni mmoja tu ndiye amepiga hatua.

Hata Mr Nice pia alipata pesa nyingi tu...sasa je tumuweke Mr Nice kundi la wasio na mafanikio kwa kuwa tu zile pisa zimemuishia ?, labda tofauti yake na Diamond ni jinsi ya kutumia pesa alizopata, aidha kwa kuuendeleza muziki wake (kutoka nje ya Tanzania, kufanya colabo, kutengeneza video zenye hadhi ya kimataifa n.k) au kibiashara nje ya muziki....So kupima mafanikio kwa mazingira haya ni mtihani.
 
Back
Top Bottom