Kwanini walinzi wa getini wakijua unaenda kuomba kazi wanakuwa wakali sana?

Mr kikulachoChako unanichekesha sana

Ila muache kusoma bahasha za watu, maana ni siri za watu.
 
Nilitolewa baruti na mlinzi pale bonite bottlers pale Moshi nikiwa natafuta sehemu ya kufanyia practical training.
 



Wengi mnawadharau sna walinzi ndo mana unajistukia ukiingia ktk ofis husalimii mala umpigie mahoni mengi kapokea maagizo usimruhusu mtu yoyote kuingia ndani had kwa kibali maalumu anafanyaje?
 
Walinzi wengine wanafata maagizo ya wenye kampuni, sasa kwa sababu yeye ndo yuko mlangoni basi yeye ndo ataonekana mbaya.
 
Hahahhaa...mlinzi wa pale NYANZA CONSTRUCTION kitangiri mwanza ni JIPU... yaani kama boss... mwaka juzi alituzingua tunaenda kuomba nafasi ya field pale... dah hadi nilicheka badala ya kulia... yaaani alikuwa mkali kama boss vile...
 
Wale walinzi wa nini wewe?
Unakosea mwenyewe kutojiamini.. Wewe pita tu choma ndania
 
Ila walinzi sio sana na sio wote, wanaoleta vikwazo ni wale wadada wa receiption, huwa vina nyodo mara ooh sasa hivi kampuni haiajiri, mara oooh mpaka tutoe tangazo
 
Ila kweli na wadada wa reception wana vyodo balaa, kwanza wanajifanya wanaongea kiswahili lafudhi ya English vile au sometime havijui kiswahili vizuri.
 
Ila kweli na wadada wa reception wana vyodo balaa, kwanza wanajifanya wanaongea kiswahili lafudhi ya English vile au sometime havijui kiswahili vizuri.
hao dawa yao nao unawatemea ung'eng'e mwanzo mwisho.kipindi flan cna mchongo wowote kitaa nikawa nasambaza cv yangu kwenye makampuni,nikapeleka kwenye kampun flan ya wamarekan,dada wa mapokez akawa ananletea ucku na kiswa english yake ya form 4,basi me nikautumia huo udhaifu wake nikawa naongea kiingereza chenye lafudhi ya kimarekani afu natoa misamiati migumu hatari,mwishowe nikamuona mdada kawa mpole akaniambia pass this way u wil see door of boss.nikacheka tu..
 
Customer service si nzuri kwa asilimia kubwa katika nchi yetu kwa kiwango kikubwa kila mtu anajifanya mbabe katika kitengo alichokamatia.
 
Nakumbuka miaka ya ya nyuma nilikuwa mwanachuo kulikuwa na jambo la muhimu sana iatakiwa nionane na katibu mkuu wa wizara fulani... na shida yenyewe ilikuwa lazima nimwambie yeye tu!nilipoenda secretary wake akaniangalia juu chini...nikahisi ntakwama, ubongo ukawa tayari kwa lolote! Akaniambia " Nieleze shida yako au kama ni binafsi nenda nyumbani kwake"! ... nikatabasamu, nikamwambia mie ni ndugu yake amwambie kuwa ndugu yake alie mwambia aje ofisini kwake kaja leo....! Simu ikapigwa.... nikaambiwa niingie! Nilipoingia. ..nikamwambia K.M samahani mie si ndugu yako ni mwanachuo wa chuo fulani...ni na shida kadhaa kadhaa kadhaa... !! KM acheka saana!! Akanisaidia kila nilichohitaji ! Akaniambia siku yoyote niende....akanitoa nje akamwambia secretary. ...mtoto wa dada yangu huyu!!! ..... Nawashauri vijana wa kisasa pia msikatishwe Tamaa na mijitu yenye roho mbaya!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…